Watoto wa Lemutuz walikataa kumsamehe baba yao...

Sasa utajuje kama Lemutuz hakuomba kwa dhati,kuna watu wana mlaumu kaomba kirahisi rahisi,kwenye macho yao wanaweza kuona ni kiurahisi ila mbele za Mungu inaweza kuwa tofauti,same kwa wale wezi yule mmoja aliomba ila ilikuwa simple,yule mwengine hakusadiki ndio tofauti. Halafu maswala ya kiroho hayahitaji swaga,wala mbwembwe issues nikusadiki tu.

Sasa wanaosema kirahisi rahisi, wao walikuwa wanataka afanye nini ndio waone yupo sawa.
Angeendelea kumuelewesha binti yake na sio kumuonesha kuwa alishinikizwa hata kumtumia text..
Kwangu mimi kwenye zile texts, yule binti alionesha maturity kuliko le mutuz na ilihitajika busara ndogo sana kusuluhisha hilo tatizo
 
Angeendelea kumuelewesha binti yake na sio kumuonesha kuwa alishinikizwa hata kumtumia text..
Kwangu mimi kwenye zile texts, yule binti alionesha maturity kuliko le mutuz na ilihitajika busara ndogo sana kusuluhisha hilo tatizo
Kwa akili ya yule mkewe ingekuwa sawasawa na mmoja (malechela) anajaza maji kwenye pipa (mtoto) mwengine (mkewe) anamwaga.
 
Ukiangalia maisha ya le mutuz aliisha vile alivyotaka yeye aliishi kwa kuipa furaha ya moyo wake kwa gharama yeyote

Jamaa alikuwa na nyumba nzuri tu Tabata lakini kamwe alikataa kukaa nje ya mji hata mimi ashampoo ni moja ya wadau ambao napenda kukaa Posta

Jamaaa alikuwa na marafiki wengi wenye vipato hasa hela chafu nikisema hela chafu naamanisha chafu hela za deal za kimafia lakini hakushawishisika kuingia huko aliendelea kuishi na kipato chake cha kawaida na kile kigari chake mimi nimemuona nacho miaka mingi kinomahhivi hakuwa na tamaa ovyo.

Alipenda sana starehe alifanya kazi jioni unamkuta kwenye starehe zake na mabebez watu wanalalamika ila hela alikuwa anajitafutia mwenyewe so matumiz yake

Kwenye siasa yeye huko ndo alikuwa ana marafiki wa kila aina alijaribu ila siasa sio za wote..... japo za chini wana sema jamaaa usalaama(TISS) we huoni kesho anaagwa pale karimjee pale huwa haagwi kajamba nani

Mzee wake malecela kapoteza kijana wake RIP POLE MZEEE

Hapa mwishoni le mutuz alikuwa kama gari la mkaa safari moja kijijini safari nyingine gereji.... mwishoni afya ya lemutuz ilianza kumsumbua hasa moyo alikuwa analazwa sana pale Muhimbili kitengo cha jakaya mambo ya moyo

Baaada ya kuona hali hiyo alijua mwisho wake hauko mbali miaka ya nyuma aligombana na mke wake na watoto sasa aliwatumia meseji kuwaomba msahamaha pia kuwaambia anaumwa hivyo anaomba msamaha.

Yale matoto yana roho ngumu yakamtumia zile meseji Mange Kimambi akapost kwenye ile app yake na Mange alifurahi maana watu hawa ni maadui akalipua hewani zile meseji.

Ila nadhani Le Mutuz alikuwa anaomba msamaha akijua tu huu mwisho wake umefika mara nyingi watu hupenda kuomba msamaha kabla ya mauti.

Watoto wa Lemutuz kama mnasoma ujumbe huu msameheni baba yenu aande kwa amani aliwakimbia marekani labda maisha yalikuwa magumu ....ASHAMPOO hapa.
Lemubebezi,,APKA
 
Usiombe mkeo akakushitakia kwa wanao, hasa wa kiume. Huo ugomvi hatapatikana muamuzi. Maana wamama wanajua kuchomekea, utakuta anasema "huku analia" nilipokuwa na mimba yako alinipiga teke la tumbo, nusura mimba yako itoke. Nilianguka chini, akaniacha palepale wasamalia wakaniokota, yeye huyo kwa mwanamke wake.
Bro hapo huchomoi.
Hakuna mwanamke iwe kichaa au ana akili timamu, anayeweza kumdanganya mtoto kwa kiwango hicho. Kama kweli ulimpiga teke la tumbo kuna ubaya gani akisema? Kama ulimtelekeza baada ya kuanguka, kuna ubaya gani akisema?
 
Dah kumbe tupo wengi,hawa akina mama ambao wako na watoto wetu always ni wagomvi na washari. Yaan unajiuliza, tatzo hasa ni nini? Huyu wa kwangu hata nikituma pesa ya mahitaji ya mtoto,hatoi mrejesho wowote.. muda wote ni mkali,
Usikae kiboya ohooo
 
Sema nini wanaume mkiamua kuharibu mnaharibu kiasi kwamba MTU anabaki na kidonda kisichofutika...mnaomba msamaha wakati MNA changamoto tu
Sasa si mtuzoee na kutusamehe tu!
yaani unatakikwa mwanamke unapoingia kwenye mahusiano ujue kabisa kwamba mwanaume huyu ipo siku atakuumiza kwakuwa atapitiwa na shetani kwenda kusikojulikana sasa anaporudi kutoka walikokwenda baada ya kuachwa na shetani ninyi mnawafukuza wanajikuta wanatoka nje kisha shetani anapita tena anawapa lift wanapostuka ninyi mnawakataa kisha hao wanaondoka moja kwa moja unabaki na vidondo kwenye nafsi yenu vya kudumu acheni hizo bana!
Duniani tunapita hivyo tujifunze kutoziba njia wakati wenzetu muda wao wa safari unapofika.
R.I.P William
 
Hakuna mwanamke iwe kichaa au ana akili timamu, anayeweza kumdanganya mtoto kwa kiwango hicho. Kama kweli ulimpiga teke la tumbo kuna ubaya gani akisema? Kama ulimtelekeza baada ya kuanguka, kuna ubaya gani akisema?
Then what unamsimulia hayo mtoto!?

Lengo hasa ni??? Fikrieni kipi cha kumwambia mtoto kipi cha kutomwambia.

Sio kila mnalofanyiwa na wanaume zenu kibaya mkifikishe kwa watoto,ugomvi ni wako na mwanaume unamuongezea na mtoto iliiii?!?!?! Muache akue ayaone mwenyewe mabaya na mavu ya baba ake sio umsaidie,what if alikudunda baada ya kumtukana na kumtamkia maneno yakumuumiza pakubwa?

Wanawake Ki ufupi,wengi wenu malezi ni SIFURI.
 
Unaweza usimkubali mzazi wako na usitake ukaribu nae ila kumtukana ni laana. Kama ni kweli itawatafuna sana
Good! siku hizi ushaanza kuwa Maadamu! karibia utaanza kuwa na fellowship mbili kwa wiki kwa yale makanisa yetu pendwa! bia na nyama choma tupa kulee! ni mwendo wa sadaka kwa mtumishi tena sadaka ya kujimaliza kisha unatembea kwa miguu toka Dodoma mjini mpaka Hombolo
 
Mitoto ikishalelewa au kuwa upande wa mama watakiwa iacha usiiweke karibu maana inakuwa na akili za kike

Akili za kike ndio nini. Hebu tuheshimiane kwanza!!!

Halafu issue ya watoto wa lemutuz na mtoto mwingine yoyote kumheshimu mzazi ni amri sio ombi. Na ni amri pekee yenye ahadi na baraka tele... kumheshimu baba na mama ni amri, haijalishi wana makosa au laa

Baraka za Mungu zinapita kwa baba kwenda kwa mtoto, Huruma ni kwa mama wa hao watoto. Hiyo ni laana ya kizazi na kizazi

Kutoka 20:12 “Waheshimu baba yako na mama yako, ili uishi maisha marefu katika nchi ninayokupa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako.
 
Good! siku hizi ushaanza kuwa Maadamu! karibia utaanza kuwa na fellowship mbili kwa wiki kwa yale makanisa yetu pendwa! bia na nyama choma tupa kulee! ni mwendo wa sadaka kwa mtumishi tena sadaka ya kujimaliza kisha unatembea kwa miguu toka Dodoma mjini mpaka Hombolo
Mimi ni madame kitambo 😂😂
Ila hapo kwenye fellowship na makanisa pendwa not me Aisee.
Naamini pombe sio dhambi so nitaacha siku nikiona inaathiri afya yangu.
 
Kwa akili ya yule mkewe ingekuwa sawasawa na mmoja (malechela) anajaza maji kwenye pipa (mtoto) mwengine (mkewe) anamwaga.
😁😁😁 kama unaamini mtu mwenye miaka zaidi ya 25 anaweza kushikiwa akili kiasi hicho, bhasi mkuu naona umeamua kusimama na lemutuz kwa lolote ila ukweli utabaki palepale, uwezo wa kufix mahusiano na binti yake ulikuwa kwa asilimia zote kutokana na yule binti alivyojielezea
 
Back
Top Bottom