Watanzania msipoteze pesa kwa kuendelea kuamini imani za kishirikina. Ni upumbavu na umaskini wa kujitakia

Habari za uzima wakuu?

Kabla ya mwaka kuisha mwaka jana mwezi wa 11 rafiki yangu mmoja alinifata akaniambia passion ndugu yangu biashara kwa upande wangu sasa imekuwa haiendi kabisa, nimepokea ushauri kutoka kwa ndugu yangu mmoja kaniambia anipeleke kwa mtaalamu nikajisafishe.

Nikamuuliza wewe unaonaje huo ushauri akaniambia naona sawa tu biashara imekuwa ngumu sana, nikamwambia sasa kama unaona sawa kwangu unataka niweke nini wakati ulishasema sawa? Akasema nishauri unaonaje nikamwambia achana na huo ujinga vinginevyo utapotea na kuua mtaji wote uanze kuokota makopo kama mwehu.

Alinicheka tu akaniambia wewe umezaliwa mjini haya mambo huyajui, Nikampa stori yangu nilipokuwa advance huko kusini nilipoenda kushona kiatu changu yule babu akanipandishia bei tofauti na tuliyokubaliana nikamwambia babu hio pesa sina kama unachukua hii chukua kama hutaki sema yule babu akasema kama unaamini unaweza kunitapeli usinipe hio pesa, nikachukua ile pesa tuliyokubaliana nikaondoka nayo. rafiki yangu akasema leo hutoboi nikamwambia yule babu umri umeenda hivyo ule ni ugonjwa.

Nilipomuadithia rafiki yangu huyu alicheka sana akasema sawa, hapo tulikuwa raha mitaa ya kariakoo kuna ki restaurant huwa nakulaga.

siku zikaenda, akawa analalamika nikienda ofisini kwake simkuti namkuta tu Mke wake anasema yupo kwenye mishe zingine kumbe tayari alishaenda kupikwa kama alivyoniambia, lakini mara hii nilipoenda nikaangalia ofisi ilivyo na miezi ya nyuma niliona utofauti mkubwa sana wa mzigo uliokuwepo mwanzo na uliobaki.

Nikamwambia sawa shemeji maana najaribu kumtafuta simpati, tangu hapo tukawa hatuna mawasiliano ya mara kwa mara na hata tulipokuwa tunakula wote nikawa simuoni, Mimi nikapotezea.

mwezi wa 12 mwishoni ndio tukaanza kuongea lakini alionekana kuwa na stress zaidi maana anasema daah kodi inaisha hapa mzigo sina wa maana na ndio huu mwezi wa biashara, nikamwambia ndugu yangu wewe ni rafiki yangu niambie tu nini kinakusibu. Akaniambia mimi sina shida ila majukumu tu na masuala ya kifamilia, nikaitikia tu sawa.

Leo ndugu yangu huyu ameua biashara baada ya kuja kuniambia ukweli yeye mwenyewe, kanipigia kaniambia passion najua jumapili unapumzika nije tuongee ndugu yangu. Nikasema karibu, alipofika akaanza kusema ndugu yangu niwe mkweli mimi nilienda kwa mganga kama nilivyokuambia kipindi kile lakini tangu nilipoenda naona nazidi kupoteza zaidi nikaanza kuchukua mpaka pesa ya mtaji kwa maneno ambayo mganga alisema kwamba nyota yangu ilikuwa imefichwa mbali sana na watu wenye nia mbaya na wewe.

Lakini niliendelea kuwa kule kwa mganga nimelala pale kwa mganga nikichanjwa usiku na kupakwa madawa ya kila aina. Ndugu yangu naomba unisaidie laki4 nianze tena mdogo mdogo, nikasema pole sana ndugu mimi binafsi kwa sasa hiyo pesa sina ila ongea na ndugu wajaribu kukupa pesa kwa mkopo sababu tayari una uzoefu au wakuchangie hapo nilikuwa nacheka maana huwa anapenda sana mambo ya ushirikina.

Anagombana na Mke wake sana kuhusu haya mambo, lakini bado haelewi, Mimi binafsi nimegoma kumpatia na nilipomchunguza sana nikajua kuna muha pale pale karibu yake ndio anamshawishi wafanye hivyo akiona mwenzake anauza sana.

Ndugu zangu naomba tu niwaambie biashara haiitaji dawa za kumwaga mbele ya mlango au kwenye kimeza chako, biashara ni sayansi, mwaka 2024 kataa kuharibu kutoa pesa zako kwa waganga wanaojinadi insta, FB kwamba wanaweza kukupa dawa za kuongeza mauzo na kuvuta wateja. Hili linaambatana moja kwa moja na manabii wanaotaka uende kuwaona ati kwamba watakupa mibaraka.

Huku wakikupa appointment Halafu unafikia kwenye hotel yake unalala na gharama za hapo zote unalipia.

mwaka 2024 kuwa mjanja utaendelea kutajirisha watu kwa kusubiri miujiza. Hakuna mafanikio ya miujiza ni kufanya kazi tu.
Waganga acha bana, mchana wanashinda kwenye nyumba za msonge, usiku wanakwenda kulala kwenye majumba yao mazuri. Wanawapiga watu hela balaa.
 
Hapa shida sio mganga,shida ni mwanaume aliyesimuliwa Siri na mwenzie na yeye kuja kumwaga hadharani
Embu tutumie picha ya huyo siri zake zilizomwaga madam joannah?

Au aliyemwaga Siri hizi unamjua?

nilikuwa nafikiri ni mtu unawaza zaidi ya hapa au ni kwanini nimeleta hapa.

Hongera kwa kuwaza umbea tu.
 
Humu kila mtu anajifanya hajui uchawi, hapendi waganga eti mtakatifu. Nampa chimbo rafiki yako.
Mwanza pale usagara kuna mlima mmoja kuna babu yuko pale aulizie malenga au kwa yule mganga wa waswezi gharama haifiki hata elfu aone dawa zinavyfanya kazi na hio laki nne utampa. Chimbo la pili aende bariadi kwa bibie Holo gharama yake ni nauli tu na akitoka hapo atakapofanikiwa ndo anatuma gharama za matibabu. Hao wabunge wenu mawaziri mpk hayati mbona machimbo wanayaelewa Sana.
Sasa badala ya kumsema rafiki yako hebu muelekeze na ww ukae na imani yako.
 
Habari za uzima wakuu?

Kabla ya mwaka kuisha mwaka jana mwezi wa 11 rafiki yangu mmoja alinifata akaniambia passion ndugu yangu biashara kwa upande wangu sasa imekuwa haiendi kabisa, nimepokea ushauri kutoka kwa ndugu yangu mmoja kaniambia anipeleke kwa mtaalamu nikajisafishe.

Nikamuuliza wewe unaonaje huo ushauri akaniambia naona sawa tu biashara imekuwa ngumu sana, nikamwambia sasa kama unaona sawa kwangu unataka niweke nini wakati ulishasema sawa? Akasema nishauri unaonaje nikamwambia achana na huo ujinga vinginevyo utapotea na kuua mtaji wote uanze kuokota makopo kama mwehu.

Alinicheka tu akaniambia wewe umezaliwa mjini haya mambo huyajui, Nikampa stori yangu nilipokuwa advance huko kusini nilipoenda kushona kiatu changu yule babu akanipandishia bei tofauti na tuliyokubaliana nikamwambia babu hio pesa sina kama unachukua hii chukua kama hutaki sema yule babu akasema kama unaamini unaweza kunitapeli usinipe hio pesa, nikachukua ile pesa tuliyokubaliana nikaondoka nayo. rafiki yangu akasema leo hutoboi nikamwambia yule babu umri umeenda hivyo ule ni ugonjwa.

Nilipomuadithia rafiki yangu huyu alicheka sana akasema sawa, hapo tulikuwa raha mitaa ya kariakoo kuna ki restaurant huwa nakulaga.

siku zikaenda, akawa analalamika nikienda ofisini kwake simkuti namkuta tu Mke wake anasema yupo kwenye mishe zingine kumbe tayari alishaenda kupikwa kama alivyoniambia, lakini mara hii nilipoenda nikaangalia ofisi ilivyo na miezi ya nyuma niliona utofauti mkubwa sana wa mzigo uliokuwepo mwanzo na uliobaki.

Nikamwambia sawa shemeji maana najaribu kumtafuta simpati, tangu hapo tukawa hatuna mawasiliano ya mara kwa mara na hata tulipokuwa tunakula wote nikawa simuoni, Mimi nikapotezea.

mwezi wa 12 mwishoni ndio tukaanza kuongea lakini alionekana kuwa na stress zaidi maana anasema daah kodi inaisha hapa mzigo sina wa maana na ndio huu mwezi wa biashara, nikamwambia ndugu yangu wewe ni rafiki yangu niambie tu nini kinakusibu. Akaniambia mimi sina shida ila majukumu tu na masuala ya kifamilia, nikaitikia tu sawa.

Leo ndugu yangu huyu ameua biashara baada ya kuja kuniambia ukweli yeye mwenyewe, kanipigia kaniambia passion najua jumapili unapumzika nije tuongee ndugu yangu. Nikasema karibu, alipofika akaanza kusema ndugu yangu niwe mkweli mimi nilienda kwa mganga kama nilivyokuambia kipindi kile lakini tangu nilipoenda naona nazidi kupoteza zaidi nikaanza kuchukua mpaka pesa ya mtaji kwa maneno ambayo mganga alisema kwamba nyota yangu ilikuwa imefichwa mbali sana na watu wenye nia mbaya na wewe.

Lakini niliendelea kuwa kule kwa mganga nimelala pale kwa mganga nikichanjwa usiku na kupakwa madawa ya kila aina. Ndugu yangu naomba unisaidie laki4 nianze tena mdogo mdogo, nikasema pole sana ndugu mimi binafsi kwa sasa hiyo pesa sina ila ongea na ndugu wajaribu kukupa pesa kwa mkopo sababu tayari una uzoefu au wakuchangie hapo nilikuwa nacheka maana huwa anapenda sana mambo ya ushirikina.

Anagombana na Mke wake sana kuhusu haya mambo, lakini bado haelewi, Mimi binafsi nimegoma kumpatia na nilipomchunguza sana nikajua kuna muha pale pale karibu yake ndio anamshawishi wafanye hivyo akiona mwenzake anauza sana.

Ndugu zangu naomba tu niwaambie biashara haiitaji dawa za kumwaga mbele ya mlango au kwenye kimeza chako, biashara ni sayansi, mwaka 2024 kataa kuharibu kutoa pesa zako kwa waganga wanaojinadi insta, FB kwamba wanaweza kukupa dawa za kuongeza mauzo na kuvuta wateja. Hili linaambatana moja kwa moja na manabii wanaotaka uende kuwaona ati kwamba watakupa mibaraka.

Huku wakikupa appointment Halafu unafikia kwenye hotel yake unalala na gharama za hapo zote unalipia.

mwaka 2024 kuwa mjanja utaendelea kutajirisha watu kwa kusubiri miujiza. Hakuna mafanikio ya miujiza ni kufanya kazi tu.
Hizo imani Watanzania wengi wanazipenda sana na ukiwaambia huo ni ujinga unaweza kugombana nao.
 
Humu kila mtu anajifanya hajui uchawi, hapendi waganga eti mtakatifu. Nampa chimbo rafiki yako.
Mwanza pale usagara kuna mlima mmoja kuna babu yuko pale aulizie malenga au kwa yule mganga wa waswezi gharama haifiki hata elfu aone dawa zinavyfanya kazi na hio laki nne utampa. Chimbo la pili aende bariadi kwa bibie Holo gharama yake ni nauli tu na akitoka hapo atakapofanikiwa ndo anatuma gharama za matibabu. Hao wabunge wenu mawaziri mpk hayati mbona machimbo wanayaelewa Sana.
Sasa badala ya kumsema rafiki yako hebu muelekeze na ww ukae na imani yako.
Mkuu Leo dada,

Umeandika maneno mengi ila unaruhusu tujadili?
 
Back
Top Bottom