Je, hii inaweza kuwa ni kwa sababu za kisiasa, imani za kishirikina au ustaarabu?

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
9,076
12,328
Tukiwa kwenye kampeni, walikuwepo wagombeaji wa kike na kiume. Katika baadhi ya maeneo huko vijijini, sehemu za kulala zilikua chache ukilinganisha na wingi wa wagombeaji na waongoza msafara.

IIilazimu mahali fulani wagombea zaidi ya moja kulazimika kulala chumba kimoja. Na hii haikua tabu kwa wanaume. Lakini kwa wanawake hakuna aliekubali kulala chumba kimoja na mwamamke mwenzie.

Mpaka wa leo najiuliza, hivi inaweza kuwa ni kwasababu za kisiasa, imani za kishirikina au kuchawiana, ustaarabu miongoni mwao, uchafu au usafi, magonjwa au maradhi, au hofu ya kuibiana fedha na vitu mbalimbali walivyonavyo, maana hali ya uchumi huwa ngumu kwenye mambo haya?

Maana vyumba ni vichache na hakuna namna nyingine ya kila moja kujisitiri kwa kujinafasi kwa siku hiyo, bali kusitiriana katika halil na mazingira hayo magumu kwa kuvumiliana tu :BASED:
 
Back
Top Bottom