Watanzania milioni 19.9 wajiandikisha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Mtaa mmoja uko Mburahati kitabu kizima kina sahihi moja yaani huyo mama kashindwa ata kubadilisha kidogo hiyo sahihi yake.......Mjingha sana hyuyo Mama
 
Hii ripoti imepakwa mafuta.
Ni sawa na kujitekenya na kujichekesha mwenyewe.
Yajayo yanafurahisha.
Wia ini ze laiti tiraki
 
SERIKALI imesema idadi ya watu waliojiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa imefikia asilimia 74. Hayo yalibainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo, jijini Dodoma jana.

Akizungumzia hali ya uandikishaji, Jafo alisema hadi kufikia juzi, umefikia asilimia 74 ambapo watu milioni 16.9 wamejiandikisha huku Halmashauri ya jiji la Arusha ikiwa chini ya asilimia 50 na kuwataka viongozi wake kujitathmini. “DC (mkuu wa wilaya), DED (Mkurugenzi wa Halmashauri), msimamizi wa uchaguzi na watendaji wana jambo la kujitathmini kwa kuwa hadi jana (juzi) wana asilimia 37.

Pia kwa Manispaa ya Moshi wao wapo juu ya asilimia 50 ambapo wana asilimia 51 wamejitahidi kidogo na Korogwe mji asilimia 5,” alisema. Alieleza kuwa anaamini Arusha watajipanga vizuri siku kwa muda uliobaki kufanya hamasa ili idadi iongezeke.

Jafo alisema Mkoa wa Dar es Salaam unashika nafasi ya kwanza kwa kuandikisha kwa asilimia 89, ukifuatiwa na Pwani 86%, Tanga 81%, Mtwara 80% na Lindi 77%. Hata hivyo, alisema pamoja na kwamba mikoa yote imevuka asilimia 50, lakini mikoa ambayo kasi yake hairidhishi ni Kigoma ambao umeandikisha kwa asilimia 57, Kilimanjaro 58%, Arusha 66%, Shinyanga 66%. Jafo alisema ofisi yake haijatoa maelekezo yeyote ya kuwanyima huduma za msingi wananchi wasiojiandikisha kwenye orodha ya daftari la wapigakura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, mwaka huu.

Kauli hiyo aliitoa baada ya kusambaa kwa ‘clip’ ikionesha mmoja wa maafisa akiwataka wananchi wajiandikishe kwa kuwa mtu yeyote ambaye hatajiandikisha hatatambulika kwenye huduma zote za msingi. Jafo alisema kuna watu wanasema watu wanalazimishwa jambo ambalo si kweli na kwamba kanuni zipo wazi hakuna mtu anayelazimishwa.
Hii takwimu ni zaidi ya upepo wa kisulisuli ndani ya siku 3 za nyongeza,wakati kituoni hatuwaoni wanaokuja kujiandikisha
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Selemani Jafo amewapongeza viongozi na wananchi wa Mkoa wa Dar es saalam kwa kuitikia kikamilifu zoezi la uandikishaji katika orodha ya wapiga kura na kuongoza kwa zoezi hilo katika orodha ya mkoa.

Waziri Jafo ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya uandikishaji katika daftari la orodha ya wapiga kura mara baada ya kufikia hitimisho siku ya Jana Octoba 17.

Amesema Mkoa wa Dar es saalam mwanzo ulianza kwa kusuasua lakini baada ya kuanza kupeana hamasa wameweza kufanya vizuri, amesema viongozi wa kazi zote na wananchi kwa ujumla hatimaye kufanikiwa kwa kuandikisha kwa asilimia 108.

"Niwapongeze Mkoa wa Dar es saalam wakati natangaza kwa mara ya kwanza Mkoa ulikuwa na hali mbaya lakini viongozi wa ngazi zote wamehamasishana halikadhalika wananchi kwa kiwango kikubwa hadi kuongoza niwapongeze sana" amesema Waziri Jafo.

Aidha amesema kwa mujibu wa Ofisi ya Takwimu wananchi wenye sifa ya kupiga kura ni 26,960,485, lakini walijiwekea lengo la kuandikisha wapiga kura milioni 22,916,412 ambao ni sawa na asilimia 85, ya wananchi wenye sifa ya kupiga kura (wanaume 10,924,479) na wanawake 11,991,933.

Amesema baadhi ya maeneo yalikumbwa na changamoto mbalimbali ikiwamo mvua na baadhi ya vituo kuwa mbali na makazi ya watu, hivyo baada ya siku ya mwisho waliamua kuongeza siku tatu kwa ajili ya kuhakikisha kila mtu anapata fulsa ya kujiandikisha.

Ameongeza kuwa "hadi kufikia Octoba 17 jumla ya wapiga kura 19,681,259 walikuwa wamejiandikisha katika orodha ya daftari la wapiga kura kwa mwaka 2019, Kati ya hao wanaume 9,529,992 na wanawake10,151,267, sawa na asilimia 86, ya lengo la wapiga kura 22,916,412, na huu ndio uandikishaji wenye mafanikio zaidi ukilinganisha na mwaka 2014" amesema.

Licha ya kila Mkoa kuvuka lengo lakuandikisha kwa asilimia 50, Mkoa mitano iliyoongoza ni Dar es saalam 108%, Pwani 96%, Mwanza 95%, Tanga 90% na Singida 90% na wote wamezawadiwa kikombe maalamu.

Huku Mikoa mitano ya mwisho licha ya kuvuka lengo lakini imeshika nafasi tano za mwisho, wa mwisho kabisa ni Kigoma 65%, Njombe 75%, Simiyu na Shinyanga 76%, ambayo jumla ya Mkoa yote ni 86%.

"Kwa upande wa halmashauri zilizofanya vizuri ni Mlele 152%, Ngorongoro 129%, Kibiti 126%, Temeke 122% na Monduli 122% ,na halmashauri zenye wapigakura wengi zaidi ya laki tisa 90,000 iliyoongoza ni Temeke MC 122%, Ilala MC111%, Mwanza CC 105%, Ubungo MC 103% na Kinondoni MC 96%" amesema.

Aidha amewapongeza wananchi wote waliojitokeza, na viongozi wa ngazi zote kuanzia mikoa na vitongoji kwa kuhamasisha katika kujiandikisha kwenye daftari la orodha ya wapiga kura la uchaguzi wa serikali za mitaa
IMG-20191018-WA0016.jpeg
 
Wajinga ndio waliwao, watu 19m kwa idadi ya watanzania 60+, ni sawa na kusema kila watanzania watatu mmoja kajiandikisha. Sasa tuchukulie kuwa watu wazima ni nusu ya hiyo 60m. Kwa mantiki hiyo 30m ni watu wazima, kwa idadi hiyo ya Jafo Ni kuwa kila watu watatu, wawili wamejiandikisha, je hiyo ni kweli? Kuna mtu yoyote kaona misururu ya kujiandikisha kama ile ya 2015 ambayo wapiga kura walikuwa 22m?

Halafu kwa upikaji huo wa data mtu unayejitambua unaweza kwenda kupiga kura? Hapo nadhani kila mtu kajionea ni jinsi gani data hupikwa na serekali hii ili kuhadaa umma.
 
Hizi data zina mushikeli. Hebu linganisha paragraph hizi mbili:

"Aidha amesema kwa mujibu wa Ofisi ya Takwimu wananchi wenye sifa ya kupiga kura ni 26,960,485, lakini walijiwekea lengo la kuandikisha wapiga kura milioni 22,916,412 ambao ni sawa na asilimia 85, ya wananchi wenye sifa ya kupiga kura (wanaume 10,924,479) na wanawake 11,991,933."

NA

"Ameongeza kuwa "hadi kufikia Octoba 17 jumla ya wapiga kura 19,681,259 walikuwa wamejiandikisha katika orodha ya daftari la wapiga kura kwa mwaka 2019, Kati ya hao wanaume 9,529,992 na wanawake10,151,267, sawa na asilimia 86, ya lengo la wapiga kura 22,916,412, na huu ndio uandikishaji wenye mafanikio zaidi ukilinganisha na mwaka 2014" amesema."

Lengo la 22,916,412 lingekuwa 85%.

Wameandikisha 19,681,259 (pungufu) ikawa 86% wapi na wapi? Hesabu gani hiyo??
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Selemani Jafo amewapongeza viongozi na wananchi wa Mkoa wa Dar es saalam kwa kuitikia kikamilifu zoezi la uandikishaji katika orodha ya wapiga kura na kuongoza kwa zoezi hilo katika orodha ya mkoa.

Waziri Jafo ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya uandikishaji katika daftari la orodha ya wapiga kura mara baada ya kufikia hitimisho siku ya Jana Octoba 17.

Amesema Mkoa wa Dar es saalam mwanzo ulianza kwa kusuasua lakini baada ya kuanza kupeana hamasa wameweza kufanya vizuri, amesema viongozi wa kazi zote na wananchi kwa ujumla hatimaye kufanikiwa kwa kuandikisha kwa asilimia 108.

"Niwapongeze Mkoa wa Dar es saalam wakati natangaza kwa mara ya kwanza Mkoa ulikuwa na hali mbaya lakini viongozi wa ngazi zote wamehamasishana halikadhalika wananchi kwa kiwango kikubwa hadi kuongoza niwapongeze sana" amesema Waziri Jafo.

Aidha amesema kwa mujibu wa Ofisi ya Takwimu wananchi wenye sifa ya kupiga kura ni 26,960,485, lakini walijiwekea lengo la kuandikisha wapiga kura milioni 22,916,412 ambao ni sawa na asilimia 85, ya wananchi wenye sifa ya kupiga kura (wanaume 10,924,479) na wanawake 11,991,933.

Amesema baadhi ya maeneo yalikumbwa na changamoto mbalimbali ikiwamo mvua na baadhi ya vituo kuwa mbali na makazi ya watu, hivyo baada ya siku ya mwisho waliamua kuongeza siku tatu kwa ajili ya kuhakikisha kila mtu anapata fulsa ya kujiandikisha.

Ameongeza kuwa "hadi kufikia Octoba 17 jumla ya wapiga kura 19,681,259 walikuwa wamejiandikisha katika orodha ya daftari la wapiga kura kwa mwaka 2019, Kati ya hao wanaume 9,529,992 na wanawake10,151,267, sawa na asilimia 86, ya lengo la wapiga kura 22,916,412, na huu ndio uandikishaji wenye mafanikio zaidi ukilinganisha na mwaka 2014" amesema.

Licha ya kila Mkoa kuvuka lengo lakuandikisha kwa asilimia 50, Mkoa mitano iliyoongoza ni Dar es saalam 108%, Pwani 96%, Mwanza 95%, Tanga 90% na Singida 90% na wote wamezawadiwa kikombe maalamu.

Huku Mikoa mitano ya mwisho licha ya kuvuka lengo lakini imeshika nafasi tano za mwisho, wa mwisho kabisa ni Kigoma 65%, Njombe 75%, Simiyu na Shinyanga 76%, ambayo jumla ya Mkoa yote ni 86%.

"Kwa upande wa halmashauri zilizofanya vizuri ni Mlele 152%, Ngorongoro 129%, Kibiti 126%, Temeke 122% na Monduli 122% ,na halmashauri zenye wapigakura wengi zaidi ya laki tisa 90,000 iliyoongoza ni Temeke MC 122%, Ilala MC111%, Mwanza CC 105%, Ubungo MC 103% na Kinondoni MC 96%" amesema.

Aidha amewapongeza wananchi wote waliojitokeza, na viongozi wa ngazi zote kuanzia mikoa na vitongoji kwa kuhamasisha katika kujiandikisha kwenye daftari la orodha ya wapiga kura la uchaguzi wa serikali za mitaaView attachment 1237484
Kwanini lengo lilikuwa kuandikisha watu 85% badala ya 100% au 99%?
 
Wajinga ndio waliwao, watu 19m kwa idadi ya watanzania 60+, ni sawa na kusema kila watanzania watatu mmoja kajiandikisha. Sasa tuchukulie kuwa watu wazima ni nusu ya hiyo 60m. Kwa mantiki hiyo 30m ni watu wazima, kwa idadi hiyo ya Jafo Ni kuwa kila watu watatu, wawili wamejiandikisha, je hiyo ni kweli? Kuna mtu yoyote kaona misururu ya kujiandikisha kama ile ya 2015 ambayo wapiga kura walikuwa 22m?

Halafu kwa upikaji huo wa data mtu unayejitambua unaweza kwenda kupiga kura? Hapo nadhani kila mtu kajionea ni jinsi gani data hupikwa na serekali hii ili kuhadaa umma.
Sawa sawa
 
Mimi nilijiandikisha Jana Tarehe 17 October 2019 Mvua ilikuwa ikinyesha... bado sijaelewa dar ina idadi ya watu wengi hivyo? last time i checked kura za Raisi ilikuwa 5m sasa hili ongezeko la watu wa Dar wametoka wapi? 26M
 
Wale wapiga zumari wa mtaa ule wanatafuta chorus ya kabadilisha. Kamati ya fitina kupitia whatsap group zao walikuwa wanapika propaganda na kueneza kwenye magroup mengine eti watanzania wamegoma sababu hawautaki utawala huu!

Walifanikiwa kuwadanganya wasiofikirisha akili. Ukweli ni kwamba chaguzi za serikali za mitaa miaka yote huwa 'baridi' tofauti na uchaguzi mkuu. Walishupaa kusema watu wamegoma bila kulinganisha na statistics za miaka ya nyuma.

Sasa Magu kathibitisha kwamba inawezekana watu wengi kujiandikisha. Uzuri wa utendaji wa Magu unaacha alama zisizofutika katika historia. Ni rekodi hiyo, itadumu hata mpige propaganda vipi.
 
Mimi nilifikiri kwa kuwa 2014 waliandikishwa wapiga kura milioni 22,basi sasa hivi 2019 baada ya kupita miaka mitano basi wangeandikisha wapiga kura milion 30.

Kwa kuwa wale ambao walikuwa hawana sifa ya kuandikishwa,waliokuwa chini ya miaka 18 ni wengi mno na ni ongezeko kubwa sana, lakini badala yake tunashuka chini,yaani tunarudi nyuma kwa kuandikisha wapiga kura milioni 19 tu.

Kuna tatizo la msingi hapo, Watanzania wanahitaji kupata majibu toka kwa Viongozi wao tuliowapa dhamama ya kuongoza.
 
This is pure cooking of data. Hiyo nyongeza ya zaidi ya watu milioni 10 waliojiandikisha kwa siku 3 ilitokea wapi? Mbona hatukuona hiyo misururu?
Maajabu ya awamu ya tano.
 
Mimi nilijiandikisha Jana Tarehe 17 October 2019 Mvua ilikuwa ikinyesha... bado sijaelewa dar ina idadi ya watu wengi hivyo? last time i checked kura za Raisi ilikuwa 5m sasa hili ongezeko la watu wa Dar wametoka wapi? 26M
Usishangae sana. Hata upigaji kura utavuka asilimia za waliojiandikisha.
 
Back
Top Bottom