Pablo Blanco
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 7,328
- 6,591
Sasa kumpata mwanamke mwenye tabia nzuri halafu akakuvutia pia hapo ndipo pana patashika nguo kuchanika,wapo wachache sana wa style hiyoTukubali kwamba wanaume tunaongozwa na tamaa halafu ndo tunapenda, zaidi ya hapo, kuna mambo mengi yanachngia hili; yawezekana ni tabia ya mtu mwenyewe anapenda kuonja onja, au wanawake na nyinyi ubunifu umepungua mpaka hamvutii tena, wanawake wengine jeuri mpaka wanapoteza mvuto (mwanamke hata kama anaumbo zuri kiasi gani kama ni mjeuri mvuto wake kwa mwanaume hupungua sana), wanaume na sisi wakati mwingine tusijidanganye kuoa wanawake wenye tabia njema tu ndo maisha yatakuwa mazuri, tuchanganye kidogo, mke wako lazima akuvutie na machoni pia, unapomtizama unakubali uchaguzi wako (ndivyo nilivyofundishwa na nimeanmini ni kweli kwa asilimia zaidi ya 90%), hisia za mapenzi huanza kwa kutazama sio kusikiliza busara za kihenga.