Wanaokuacha kwenye Mahusiano, wengi wao walishapanga hivyo hata kabla ya kufanya kosa hilo…

Feb 4, 2024
81
237
Wanaokuacha kwenye mahusiano wengi walipanga hivyo hata kabla ya hilo kosa wamelotumia kama sababu

Mara nyingi anayeachwa anakuwa na msongo wa mawazo na kujiona asiye faa kwenye hii Dunia na wengine huenda mbali mpaka kujiona wasio na thamani yoyote, je nawe umewahi kuwa hivyo baada ya kuachwa?

Sababu kubwa inayofanya anayeachwa kujiona hivyo ni maneno anayotamkiwa wakati wa kuachwa ikiwemo mpaka vitisho na muachaji hutumia kosa moja la wazi kama fimbo ya kumuadhibu huyo mkosaji na kwa yote hayo muachwaji hujiona mwenye hatia kubwa sana, Je unajua ukweli ni upi?

Ukweli ni kuwa yawezekana kweli hilo kosa limekuwa kubwa kuliko nguvu ya upendo baina yenu na hatimaye kusababisha uhusiano kuvunjika kutoka upande mmoja

Lakini kwa walio wengi wanakuwa tayari na sababu zote za kukuacha ila ule ujasiri ndio hawana hivyo wanasubiria tu ukosee kisha watumie hilo kosa kama sehemu ya kuwasilisha nia zao za muda mrefu.

Unaweza kuomba sana msamaha ila wapi na sio kwamba kosa lako ni kubwa zaidi ya ambavyo kawahi kukukosea ila katu katu anasimamia msimamo wake kuwa muachane, ukiona mtu yupo hivyo usiendelee kumlilia bali kubali tu matokeo kwa sababu kuna uwezekano mkubwa alikuwa kishakuacha kitambo ila akawa hana sababu ya kupitia hivyo sasa kaipata basi anaisimamia vilivyo

Sio kila unapoachwa basi wewe ni mkosaji mkubwa la hasha wengine walikuwa tu wapitaji wenye sababu zao binafsi hivyo wakabaki tu wanakutafutia kosa ili wapate mlango wa kutokea .

Mwanasayansi Saul kalivubha
fikia ndoto zako.
 
Wa kukutafutia kosa huwa hajifichi, kama upo smart utaona tu kwenye namna mnavyowasiliana na matendo yake.
 
Back
Top Bottom