UZUSHI Wananchi wa Zimbabwe huuza vidole ili wajipatie kipato

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Hivi karibuni kulizuka uvumi wa watu kulipa hela nyingi kununua vidole vya miguu nchini Zimbabwe. Je, Ukweli ukoje?


images (62).jpg
 
Tunachokijua
Kumekuwa na uvumi kwenye mitandao mbalimbai ya kijamii ukidai kuwa imeibuka biashara ya vidole gumba vya miguu nchini Zimbabwe. Mathalani, Jarida la My News lilifafanua namna uvumi huo ulioenea katika mitandao mbalimbali ya kijamii katika nchi mbalimbali za Kiafrika. Sehemu ya Jarida hili iliandika:

"Kuna ujumbe kwenye mitandao ya kijamii unadai vidole vinaweza kuuzwa kwa hadi dola za Kimarekani 40,000 kulingana na ukubwa, 'Katika video moja kwenye mitandao ya kijamii, inaonesha mwanaume aliyekatwa kidole akidai gari kama malipo baada ya kuahidiwa.

Uvumi huo ulifika pia katika chombo cha habari cha BBC ambacho kinaeleza namna Utani wa kuuza vidole vya mguu zimbabwe waeleweka vibaya Nigeria. Wakifafanua uvumi huo BBC wanaandika:

Utani unaoendelea katika mtandao wa kijamii nchini Zimbabwe kuhusu watu kuuza vidole vyao vya miguu kwa fedha nyingi , kunachukuliwa na umuhimu mkubwa kwengineko barani Afrika.
Taarifa hiyo kwamba raia wa Zimbabwe wanauza vidole vyao vya miguuni ili kukabiliana na umasikini imesambaa sana nchini Nigeria. Mwanablogu mmoja wa Zimbabwe amedai kwamba biashara hiyo inafanyika katika kituo kimoja cha maduka katika mji mkuu Harare.
Inanukuua ujumbe wa WhatsApp ukiwa na takwimu za hadi $40,000 (£31,800) zinazotolewa na watatbibu wa kitamaduni. Wakijulikana kama waganga bandia wanaoshirikishwa na uchawi - hushtumiwa na waganga wa kienyeji wanaoheshimika kwa jina 'sangoma' kusini mwa bara Afrika.

Je, kuna ukweli wowote kuhusu jambo hili?
Baada ya taarifa hizi kuenea kwenye mitandao ya kijamii kiongozi wa Zimbabwe Bwana Kindness Paradza, Naibu Waziri wa Habari amejitokeza na kukanusha kuwapo kwa biashara hiyo. Anaeleza:

Kama serikali, tulifanya utafiti juu ya suala hilo na tukagundua kuwa sio kweli," Paradza alisema, kulingana na nakala iliyochapishwa 2 Juni 2022.

Paradza alichunguza duka moja katika mji mkuu wa Zimbabwe Harare ambapo ilisemekana vidole vya miguu vinauzwa, na inasemekana alisema baadaye:

"Hizi ni ripoti za mitandao ya kijamii zinazolenga kuchafua jina la nchi."Hatukupata ushahidi kwa mtu yeyote anayeuza- au kununua vidole vya miguu nchini Zimbabwe.

Pia mpaka sasa hamna mnunuaji au mnunuzi wa vidole japo ambapo Mahakama nchini Zimbabwe imemfungulia mashtaka mwanaume mmoja kwa kufanya mzaha kuwa alikuwa sehemu ya kundi la watu wanaonunua vidole vya miguu vya binadamu kwa hadi dola za kimarekani $78,000.
Madai kwamba Wazimbabwe waliokuwa na shinikizo kubwa wameamua kuuza vidole vyao vya miguu ili waokoke yalienea kwenye mitandao ya kijamii wiki mbili zilizopita na afisa wa ngazi ya juu wa serikali alikashifu utani huo kama jaribio la kuharibu taswira ya nchi.

Hivyo, kutokana na ufafanuzi huo wa Waziri wa Habari wa Zimbabwe JamiiForums inaona taarifa zinazosambaa kuhusu kuwapo kwa biashara ya vidole hazina ukweli
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom