A
Anonymous
Guest
Sisi Wanafunzi wa St. John's University of Tanzania cha Dodoma tunakidai chuo hela ambazo tulilipa kabla hatujalipiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), tumeandika barua nyingi sana kuomba waturudishie fedha zetu (refund).
Wazazi wengine walikuwa wanakopa ili watulipie ada na michango mingine wakiamini zitarejeshwa na kuingizwa kwenye matumizi ama ya mhusika au ya Mwanafunzi lakini chuo kinatuzungusha na kugoma kuturudishia fedha zetu na kutuwekea masharti magumu sana.
Wanafunzi wengi tunaodai ni wa ngazi tofauti, mfano sisi ni Wanafunzi wa Mwaka wa Tatu, madai tunayodai ni yale ambayo tulilipa wakati tunaanza Mwaka wa Kwanza Mwaka wa mazomo 2021/22.
Tulilipa zaidi ya Shilingi Milioni 1 (malipo yanategemea na aina ya kozi), hadi sasa ni mwaka wa Tatu hatujalipwa, tunazungushwa tu.
Kuna wachache ambao wamelipwa lakini kwa kucheza michezo na watu wa Idara ya fedha, wanaambiwa kwa kuwa hujarejeshewa fedha zako, mtafute mtu ambaye hajalipa ada, unampeleka kwake, wanachofanya ile amount ambayo mtu unadai kwa kuwa inaonekana kwenye mfumo wanaihamishia kwa mhusika mwingine kisha yule anayelipa anatoa fedha cash kwa makubaliano kwamba mtu wa Idara ya Fedha naye anapata chochote.
Sisi ambao hatutaki michezo ya aina hiyo wanatukazia na tunaendelea kulallamika mpaka sasa.
Kinachouma zaidi ni kuwa wapo ambao wanamaliza chuo mwaka huu na hawajalipwa, hiyo inamaanisha watahitimu bila kurejeshewa fedha zao.