Wakuu wa Wilaya Kilimanjaro Wapewa Magari Mapya

Wild Flower

Member
Jul 20, 2023
88
105
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, amekabidhi magari matatu mapya kwa ajili ya Wakuu wa Wilaya za Rombo, Mwanga na Same, yenye thamani ya zaidi ya Tsh. milioni 600 ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na kuleta maendeleo ya Mkoa huo.

Akiongea katika hafla fupi ya makabidhiano hayo nje ya viwanja wa ofisi za RC wa Kilimanjaro, Babu amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ameanza kutekeleza maombi mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro ya kuwapatia Wakuu wa Wilaya vitendea kazi.

RC Babu amesema Wabunge wamekuwa wakilalamika Bungeni kuhusiana na Wakuu wa Mikoa kukosa magari ambapo Mkoa ulipanga kuhakikisha bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 mpaka ifikapo mwezi Juni mwaka huu wawe wameshanunua magari matatu ya Wakuu wa Wilaya.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema magari hayo yatatumika kwa ajili ya shughuli za Kiserikali na kuwataka kwenda kuyatunza magari hayo kwani yamenunuliwa kwa gharama kubwa

SOURCE: MILLARD AYO
 
Tupate total cost hapa wanandugu.

M600 + M600 +M600=M 1800 ambayo ni sawa na B 1.8

NAMSHUKURU SANA MAMA KWA KUWEZESHA HILI 🙌🏽🙌🏽🙌🏽
 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, amekabidhi magari matatu mapya kwa ajili ya Wakuu wa Wilaya za Rombo, Mwanga na Same, yenye thamani ya zaidi ya Tsh. milioni 600 ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na kuleta maendeleo ya Mkoa huo.

Akiongea katika hafla fupi ya makabidhiano hayo nje ya viwanja wa ofisi za RC wa Kilimanjaro, Babu amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ameanza kutekeleza maombi mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro ya kuwapatia Wakuu wa Wilaya vitendea kazi.

RC Babu amesema Wabunge wamekuwa wakilalamika Bungeni kuhusiana na Wakuu wa Mikoa kukosa magari ambapo Mkoa ulipanga kuhakikisha bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 mpaka ifikapo mwezi Juni mwaka huu wawe wameshanunua magari matatu ya Wakuu wa Wilaya.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema magari hayo yatatumika kwa ajili ya shughuli za Kiserikali na kuwataka kwenda kuyatunza magari hayo kwani yamenunuliwa kwa gharama kubwa

SOURCE: MILLARD AYO
Yaani ukifuatilia sana Mambo ya watawala was Afrika unaweza kuwa ..,............
 
Back
Top Bottom