Wakazi wa Gongo la Mboto kuelekea Chanika tunasubiri kwa hamu awamu mpya ya ujenzi wa mwendokasi

passion_amo1

JF-Expert Member
Dec 3, 2023
1,611
3,285
Watanzania wenzangu ni matumani yangu mu buheri wa afya, mliopo na Matatizo mbali mbali muwe na subira na kutokata tamaa hata mnapohisi kushindwa.

Leo katika pita pita zangu nikakutana na uzi wa dada Janeth Thomson Mwambije akiwa amekutana na mkuu wa wilaya ya ILALA mheshimiwa Edward Jonas. Katika kusoma uzi huu nikapata kufahamu kwamba kuna awamu mpya ya mpango wa barabara za mwendokasi zitakazoanzia G/mboto- Chanika kueleka Msongola.

Binafsi Nina furaha sana kusikia habari hii, wakazi wengi wa G/mboto mtakubaliana na mimi kwamba awamu ya kwanza ya barabara ya mwendokasi sasa imefikia hatua nzuri. Pamoja Na changamoto nyingi tunazokumbana nazo kama vumbi na matope wakati wa kipindi hichi cha matengenezo ila tunategemea yatakapokamilika mambo yatakuwa mazuri.

Hivi sasa barabara inakwenda mpaka mbele ya maliasili kidogo ikitazamana na upande wa jeshini. Ninapenda kusema machache.

Mosi, upande huu wa Jeshini kuna fremu ambazo zinajengwa mpya nyingi na zinaenda karibia na mwisho wa lami. Kwa wafanyabiashara wenzangu kama mimi hii nafasi adhimu sana sababu patakuwa ni sehemu yenye mzunguko mkubwa wa kibiashara.

Kwanza ni sehemu ya awamu ya kwanza magari ya mwendokasi yatakapokuwa yanaishia, pili mradi wa reli ya umeme, tatu ni sehemu ya jeshini, nne kuna chuo cha Kampala nyuma. Na imani wafanyabiashara wenzangu tumeshaona fursa kubwa iliyopo hapa.

Katika awamu hii mpya ya mwendokasi itakayoanzia G/mboto kueleka mpaka Msongola Tunaomba Serikali iweke juhudi kubwa katika kulifanikisha hili.

Wafanyabiashara, wajasiriamali Wa wilaya ya Ilala natumai wana shauku kubwa sana kuona mambo haya yakikamilika. Sababu itafungua fursa nyingi sana.

Niwatakie Jioni njema 16:08
 
Watanzania wenzangu ni matumai yangu m buheri wa afya, mliopo na Matatizo mbali mbali muwe na saburi na kutokata tamaa hata mnapohisi kushindwa.

Leo katika pita pita zangu nikakutana na uzi wa dada Janeth Thomson Mwambije akiwa amekutana na mkuu wa wilaya ya ILALA mheshimiwa Edward Jonas.katika kusoma uzi huu nikapata kufahamu kwamba kuna awamu mpya ya mpango wa barabara za mwendokasi zitakazoanzia G/mboto- chanika kueleka msongola.

Binafsi Nina furaha sana kusikia habari hii, wakazi wengi wa G/mboto mtakubaliana na mimi kwamba awamu ya kwanza ya barabara ya mwendokasi sasa imefikia hatua nzuri. Pamoja Na changamoto nyingi tunazokumbana nazo kama vumbi na matope wakati wa kipindi hichi cha matengenezo ila tunategemea yatakapokamilika mambo yatakuwa mazuri.

Hivi sasa barabara inakwenda mpaka mbele ya maliasili kidogo ikitazamana na upande wa jeshini. Ninapenda kusema machache,

Mosi, upande huu wa jeshini kuna fremu ambazo zinajengwa mpya nyingi na zinaenda karibia na mwisho wa lami. Kwa wafanyabiashara wenzangu kama mimi hii nafasi adhimu sana sababu patakuwa ni sehemu yenye mzunguko mkubwa wa kibiashara. Kwanza ni sehemu ya awamu ya kwanza magari ya mwendokasi yatakapokuwa yanaishia, pili mradi wa reli ya umeme, tatu ni sehemu ya jeshini, nne kuna chuo cha Kampala nyuma. Na imani wafanyabiashara wenzangu tumeshaona fursa kubwa iliyopo hapa.

Katika awamu hii mpya ya mwendokasi itakayoanzia G/mboto kueleka mpaka msongola Tunaomba serikali iweke juhudi kubwa katika kulifanikisha hili.

Wafanyabiashara, wajasiriamali Wa wilaya ya ilala natumai wana shauku kubwa sana kuona mambo haya yakikamilika. sababu itafungua fursa nyingi sana.

Niwatakie Jioni njema 16:08
Usafiri wa mwendokasi siyo suluhisho kwa janga la usafiri lililopo Dsm, na wala haitaweza kupunguza makali ya janga Hilo bali litaongeza tatizo zaidi. Suala la Mipango miji tayari lilishakosewa tangu hatua za awali kabisa za uanzishwaji wa mji huu wa Dar.
 
Back
Top Bottom