Wakazi wa Dar es salaam kulazimika kutembea na oksijeni baada ya miaka mitano

CONSISTENCY

Senior Member
Feb 16, 2023
135
307
Profesa wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM), Julius Nyahongo amesema kuwa miaka mitano ijayo, wakazi waishio Dar es Salaam watalazimika kutembea na oksijeni kutokana na ongezeko la joto.

Profesa Nyahongo amesema kuwa ongozeko hilo la joto linachangiwa na ukataji wa miti kiholela hali inayohatarisha mazingira.

Aidha Profesa amemuomba Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango kuwasihi wakandarasi wote nchini wanapotaka kujenga wakumbuke kuhifadhi mazingira kwani miti imeota kwa shida.

Amesema hayo leo April 15, 2024 katika mdahalo wa kumbukizi wa miaka 102 ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa, Julius Nyerere uliofanyika Dar es salaam.
Chanzo: Azam TV
 
Kumbe wale wanaowekewa mitungi ya oxygen hospitali wanasikiaga AC Kwa mdomo na pua. Sikujua.

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
Huyo Professor alikua na hoja ila ameshindwa kuelezea.
Hoja ni kwamba baada ya miaka mitano kutakua na ongezeko kubwa la joto hasa mikoa ya pwani.
Ongezeko la joto limekua kubwa karibia dunia nzima hadi limefikia hatua ya kuua watu, hivyo tahadhari inayotakiwa kutolewa ni kwamba serikali ijifunze na kutoa elimu ya namna ya kukabiliana na joto lililozidi viwango vya kawaida.
 
Ni kweli analosena barabara alizojemga mchina za mitaa kakata sana miti na akuacha hata sehemu ya kupanda miti
Tofauti na barabara zilizojengwa na Mjapani KONOIKE
Mfano mnzuri angalia kawawa road ilikuwa ina miti mingi pembezoni mwa barabara ambayo iliacha space
Ukija barabara za mtaani mchina kaweka mitaro tu ambayo simu yako ikitumbukia sahau miti kakata yote na wala hakuwa na habari ya kuacha space za kupanda miti

Lakini pia utakuta mpuuzi anakata muarobaini wenye zaidi ya miaka 20 au muembe wa zaidi ya miaka 50 ili biashara yake ionekane then baada mwaka kivuri hana kisha anapanda miti furani hivi ya KINGESE iliyotapakaa Dar nzima inachanua tu lakini kiviuri kizuri haina kazi yake matawi kusambaa kama paa la uyoga
 
Profesa wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM), Julius Nyahongo amesema kuwa miaka mitano ijayo, wakazi waishio Dar es Salaam watalazimika kutembea na oksijeni kutokana na ongezeko la joto.

Profesa Nyahongo amesema kuwa ongozeko hilo la joto linachangiwa na ukataji wa miti kiholela hali inayohatarisha mazingira.

Aidha Profesa amemuomba Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango kuwasihi wakandarasi wote nchini wanapotaka kujenga wakumbuke kuhifadhi mazingira kwani miti imeota kwa shida.

Amesema hayo leo April 15, 2024 katika mdahalo wa kumbukizi wa miaka 102 ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa, Julius Nyerere uliofanyika Dar es salaam.
Chanzo: Azam TV
Kweli nimeamini maprofesa....afya ya akili....inawahusu....
 
Tukishindwa kuheshimu ELIMU yake basi tuheshimu UMRI wake maana UZEE una changamoto nyingi, kuna mwenzake naye alisemaga kaokotwa jalalani 😂😂....
 
Back
Top Bottom