Wadogo zangu wa kike hata kama nyumbani kwenu maisha ni magumu usikubali ndoa ya sogea tukae

BabaMorgan

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
4,133
10,847
Mtu akitaka kuishi na wewe kanuni ni kutambulishana kwa wazazi wa pande zote mbili tena physically kama kwao ni mbali hakikisha mnaenda achana na biashara za kutambulishwa kwenye simu ama video call kama ni Kigoma pandeni Saratoga muende.

Flat TV, sofa set, bedsofa, friji na sabufa zisifanye uforce ndoa wewe ni mtu wa thamani sana kama mtu anakupenda basi ataenda kujitambulisha kwenu.

Miongoni mwa vitu navyojutia ni kuishi na mtoto wa mtu bila ya kwao kuwa na taarifa.
 
𝖭𝖣𝖮𝖠 𝖭𝖨 𝖠𝖨𝖭𝖠 𝖸𝖠 𝖬𝖠𝖴𝖠𝖩𝖨 𝖸𝖠 𝖪𝖨𝖬𝖶𝖨𝖫𝖨, 𝖪𝖨𝖱𝖮𝖧𝖮 𝖭𝖠 𝖪𝖨𝖴𝖢𝖧𝖴𝖬𝖨 𝖸𝖠𝖫𝖨𝖸𝖮𝖧𝖠𝖫𝖠𝖫𝖨𝖲𝖧𝖶𝖠 𝖭𝖠 𝖪𝖨𝖪𝖴𝖭𝖣𝖨 𝖥𝖴𝖫𝖠𝖭𝖨 𝖧𝖨𝖵𝖨 𝖢𝖧𝖠 𝖶𝖠𝖧𝖴𝖭𝖨.

𝖪𝖠𝖳𝖠𝖠 𝖭𝖣𝖮𝖠, 𝖪𝖠𝖳𝖠𝖠 𝖭𝖣𝖮𝖠, 𝖪𝖠𝖳𝖠𝖠 𝖭𝖣𝖮𝖠.
 
Hapana kimsingi maisha ya sogea tukae yanakuwa yametawaliwa na hisia na motivation kubwa ni ngono na sio upendo wa kweli na case nyingi za sogea tukae zinwakuta vijana wadogo walioanza kujitegemea ni mara chache ndoa za namna hiyo kutoboa

Unachosema ni sawa.

Lakini ukienda Mahakamani Majibu ni tofauti.

Ndoa nyingi zinavunjika kila siku na zimefungwa kanisani, na Watu wametambulishana.

Kutoboa kwa ndoa hakuna uhusiano wowote na kwenda kwa wazazi au kutokwenda.

Hoja yako kuu ambayo ni nzuri ambayo ninaikubali ni kuwapa wazazi heshima na kuonyesha kuwa mtoto huyo iwe kijana au binti hakujizaa wala kujikuza mwenyewe.

Thamani ya mwanamke sio mpaka apelekwe kwa wazazi sijui kutambulishwa.

Heshima ya mwanamke ni kumtunza na kumheshimu.

Wapo wanawake mamilioni kwa mamilioni wameolewa na kutambulishwa kwa wazazi na wanapitia unyanyasaji wa hali ya juu. Ukatili na kubagazwa.

Kitendo cha Mwanamke kuoelewa wake wengi ni kushusha heshima na utu wa mwanamke.
Kitendo cha kumtolea Mwanamke mahari ni kumshushia heshima mwanamke.

Kutambulishana na utaratibu mzuri na hasa unalenga kuwapa wazazi heshima na thamani.
 
Mtu akitaka kuishi na wewe kanuni ni kutambulishana kwa wazazi wa pande zote mbili tena physically kama kwao ni mbali hakikisha mnaenda achana na biashara za kutambulishwa kwenye simu ama video call kama ni Kigoma pandeni Saratoga muende.

Flat TV, sofa set, bedsofa, friji na sabufa zisifanye uforce ndoa wewe ni mtu wa thamani sana kama mtu anakupenda basi ataenda kujitambulisha kwenu.

Miongoni mwa vitu navyojutia ni kuishi na mtoto wa mtu bila ya kwao kuwa na taarifa.
Ubarikiwe ndugu
kama anakupenda lazma atafika kwenu , mahari ni maonezi tu zitalipwa baadae, from there piteni kanisan fungeni ndoa hata ya watu sita maisha yaendelee....hizi mambo za njoo tuishi zinawaponza sana wadogo zetu
 
Unachosema ni sawa.

Lakini ukienda Mahakamani Majibu ni tofauti.
Ndoa nyingi zinavunjika kila siku na zimefungwa kanisani, na Watu wametambulishana.

Kutoboa kwa ndoa hakuna uhusiano wowote na kwenda kwa wazazi au kutokwenda.

Hoja yako kuu ambayo ni nzuri ambayo ninaikubali ni kuwapa wazazi heshima na kuonyesha kuwa mtoto huyo iwe kijana au binti hakujizaa wala kujikuza mwenyewe.

Thamani ya mwanamke sio mpaka apelekwe kwa wazazi sijui kutambulishwa.
Heshima ya mwanamke ni kumtunza na kumheshimu.
Wapo wanawake mamilioni kwa mamilioni wameolewa na kutambulishwa kwa wazazi na wanapitia unyanyasaji wa hali ya juu. Ukatili na kubagazwa.

Kitendo cha Mwanamke kuoelewa wake wengi ni kushusha heshima na utu wa mwanamke.
Kitendo cha kumtolea Mwanamke mahari ni kumshushia heshima mwanamke.

Kutambulishana na utaratibu mzuri na hasa unalenga kuwapa wazazi heshima na thamani.
Kutambulishana ni sign ya wote kuwa mnajitambua na ndio namna kumuonyesha mwenza wako kuwa unampenda na kumthamini na upo proud kumtambulisha kwa watu wako wa muhimu kama wazazi.

Ndoa zinazofika mahakamani kwa ajili ya talaka ni chache sana kulinganisha na wale wanaokubali yaishe kutumia kigezo cha takwimu za mahakamani sio sawa kwanza kibongo ndoa nyingi sio rasmi maana watu wanaishi kama mke na mume na hawana cheti cha ndoa.

Ndoa za sogea tukae mostly umri wa wahusika huwa ni chini ya 30 vijana ambao wameanza kupata pesa za kujikimu lakini wengi wanakuwa hawapo tayari na ndoa furaha yao ni uhakika wa kupata sex masaa 24 sasa majukumu yanapoongezeka na uchumi unapokuwa tight wanakuwa sio wepesi wakuvumilia.
 
Back
Top Bottom