Wachina washerehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China baada ya wimbi la maambukizi ya COVID-19 kumalizika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,023
1,047
1675232614663.png

Mkesha wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China ulifanyika tarehe 21 Januari mwaka huu, ambapo wanafamilia kutoka sehemu mbalimbali walikusanyika pamoja na kukaribisha Mwaka Mpya wa Sungura.

Sikukuu hiyo kwa mwaka huu ilikuwa ni ya kwanza kufanyika baada ya China kutangaza mapema Januari kuwa, inapunguza usimamizi wa COVID-19 kutoka magonjwa ya kuambukiza ya ngazi A hadi ngazi B.

Tangu mwaka jana, China imekuwa inafuatilia sana hali ya maambukizi na mabadiliko ya virusi, kuongeza kiwango cha chanjo kwa wananchi, na kufanya maandalizi ya kukabiliana na maambukizi makubwa kwa umakini. Kiwango cha chanjo kwa wananchi nchini China kimezidi asilimia 90, na kiwango hicho kwa watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60 kimezidi asilimia 85.

Baada ya tathmini ya kina kuhusu virusi hivyo, China imerekebisha sera na hatua zake, kwa kufuata mwelekeo wa hatua za kuzuia na kudhibiti janga la COVID-19 duniani, na matumaini ya watu kurejesha maisha ya kawaida. Wakati huo huo, hali hii haimaanishi kwamba China imeacha kabisa juhudi za kukabiliana na janga hilo, bali China kwa sasa imeweka kipaumbele katika kulinda wazee haswa wale wenye magonjwa sugu.

Katika Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, watu walipata fursa kwa mara ya kwanza katika miaka mitatu kujumuika na familia zao kusherehekea Sikukuu hii muhimu zaidi kwa Wachina.

Jambo la kuvutia ni kwamba, vijiji vingi nchini China vilipita kilele cha maambukizi ya virusi vya Corona wiki mbili ama tatu kabla ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, na hivyo kufanya hali kuwa ya utulivu wakati wa Sikukuu hiyo.

Lakini swali ambalo wengi wamejiuliza ni kwamba, je, kuna hatua zozote zilizochukuliwa kuhakikisha kuwa watu wa vijijini wanakabiliana na janga hili? Katika kujibu swali hili, wanahabari nchini China walirejea kwenye maskani zao kwa mara ya kwanza katika miaka mitatu, na waliweza kujionea wenyewe jinsi taasisi za afya katika maeneo ya vijijini zilivyojiandaa kukabiliana na janga hilo.

Kitu kikubwa ambacho wanahabari hao wamejionea ni jinsi Tiba ya Jadi ya Kichina (TCM) inavyotumika katika kukabiliana na COVID-19. Madaktari katika hospitali za vijijini wanasema, TCM inatumika katika kutibu watu walio na dalili za COVID-19 na wanapata ahueni mapema, na kwa familia ambazo zilikuwa nahoma na kikohozi, zilipata tiba ya jadi ya Kichina na kupona mapema na hivyo kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina wakiwa na afya tele.

Dokta Shan Changping ni maarufu sana katika kaunti ndogo ya Juye, mkoa wa Shandong, mashariki mwa China. Dokta Shan anatumia Tiba ya Jadi ya Kichina (TCM) katika matibabu yake, na watu wanaosumbuliwa na maumivu ya mgongo, kupooza, na magonjwa mengine wameweza kupona kutokana na tiba hiyo. wakati wimbi la COVID-19 lilipotokea katika kautni hiyo mwezi Disemba mwaka jana, kliniki yake ndogo ilijaa wagonjwa ambao walikuwa na dalili ndogo za COVID-19, ikiwemo kikohozi, maumivu ya kichwa na homa. Kwa kutumia TCM, aliweza kusaidia wagonjwa wake kupata nafuu mapema na kupona kabisa. Anasema kuwa, ili kukabiliana na ugonjwa huo, muhimu zaidi ni kula vizuri, kunywa maji mengi na kupumzika zaidi, na pia kuwa na mtazamo chanya, mambo ambayo ni muhimu katika kuimarisha afya ya mwili na kuongeza kingamwili.

Tiba ya Jadi ya China inatumika katika mapambano dhidi ya COVID-19 duniani kote, na imethibitisha kuwa na ufanisi mkubwa. Shirika la Afya Duniani (WHO) limethibitisha katika ripoti yake kuwa, TCM ina faida kubwa katika tiba ya COVID-19, hususan kwa watu wenye dalili ndogo na za kati.

Kwa kutumia TCM, wakazi wa maeneo ya vijijini nchini China wameweza kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa furaha na afya tele, na hivyo kudhihirisha tena kuwa, serikali kuu ya China, chini ya Chama cha Kikomunisti cha China, kinatanguliza maslahi ya wananchi wake katika kila eneo.
 
Back
Top Bottom