Kwanza nianze kwa kuwapa maua yenu Jamiicheck, binafsi nawakubali sana kazi yenu. Big up sana sana.
Twende kwenye mada.
Naona kuna Picha za wachezaji wa kike wakiwa wanaweka mpira ndani ya jezi tumboni, baadhi ya watu wanasema hiyo ni kampeni ya kuvitaka vilabu wasiachane na wachezaji wao wakipata mimba.
Je, jambo hili ni kweli? Na je kama ni kweli ni sheria za mpira au wanawaonea tu?
=====
Jamiiforums imezungumza na Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo ili kujua ukweli wa jambo hili naye alikuwa na haya ya kusema:-
Suala la mkataba wa mchezaji na klabu siyo la TFF japokuwa tunafahamu kwa kuwa lazima Shirikisho liwe na taarifa za makubaliano ya pande hizo mbili, suala hilo linahusu pande mbili.
Ikitokea mkataba umevunjwa kwa kuzingatia vipengele vilivyopo katika mkataba huo, ikiwa umevunjwa kwa mazingira tofauti na vipengele husika hapo ndipo TFF tunaweza kuingilia, iwe ni mchezaji kavunja au klabu ndio imevunja.
Kuhusu Wachezaji kuweka mpira tumboni kama ni kampeni, anasema:
Hiyo ni aina ya ushangiliaji, kuhusu kama ni kampeni sisi kama TFF hatufahamu hilo, tunajua ni sehemu ya ushangiliaji kama ilivyo staili za aina hiyo.
Kuhusu kupata kesi au malalamiko ya kuvunjwa kwa mkataba kutokana na ujauzito hilo siwezi kujibu moja kwa moja kwa kuwa sijafuatilia, inawezekana halipo au lipo lakini halijafika mezani kwangu.
Ushauri
Tunatoa wito kwa Klabu kuendelea kutoa elimu kama TFF inavyofanya kuhusu haki za wachezaji na soka la Wanawake kwa jumla.