Wachambuzi wameisahau Kengold kuwa imepanda ligi kuu, wanaisifu Pamba muda wote kwa kua wamepewa supu ya Ng'ombe na mboga ya kupeleka nyumbani

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,383
12,946
Hili ndiyo taifa lenye wachambuzi wa ajabu kabisa katika tasnia ya mpira wa miguu, wachambuzi wengi walijifungia Mwanza toka waliposikia kuwa timu itachinja ng'ombe 25, wamesahau kabisa kuwa kengold kutoka Mbeya nayo imepanda ligi kuu na ndiyo timu iliyoongoza kwa point 70 na kufuatiwa na pamba iliyopata point 67

lakini ukisikiliza redio na wachambuzi wa michongo wanaisifu Pamba muda wote utadhani imepanda peke yake ligi kuu

oya wachambuzi wa clouds media na wachambuzi wengine chambueni timu zote na siyo kuchambua timu moja kwa kua mmekula ng'ombe
 
Labda story ni story sababu Pamba timu ambayo hapo kabla ilikuwa kwenye ligi bila kushuka sasa imerudi kwenye ligi - Pamba ina historia hawa Kengold sijui....
HIYO SABABU YENYE MASHIKO KABISA KATIKA UCHAMBUZI WA MPIRA
 
Binafsi nilifurahi sana kusikia pamba imepanda daraja na kuingia ligi kuu,,, juzi nimefanya suprize party kwa watoto wangu na hubby wangu maana hiyo timu ina historia kubwa sana katika maisha yangu..... Pia naiombea ilete ushindani mkubwa.
 
Beya Simba, Mao Mkami 'ball dancer' ni Baadhi tu Ya Majina Ya Wana T.P Lindanda yanayochagiza Watu Waisahau Ken Gold..!

Hata wao Ken Gold Wakija kufanya maajabu, hawatasahaulika huko mbeleni
 
We jamaa sometimes unafeli. Yaani kwa historia ya Pamba unataka iongelewe sawa na KenGold? Level za KenGold ni kuongelewa na wachambuzi aina yako inatosha. Hata hapo hapo Chunya pamoja na nationalism kubwa miongoni mwa Wanyaki watakuwa wanaiongelea zaidi Pamba kuliko KenGold
 
Hili ndiyo taifa lenye wachambuzi wa ajabu kabisa katika tasnia ya mpira wa miguu, wachambuzi wengi walijifungia Mwanza toka waliposikia kuwa timu itachinja ng'ombe 25, wamesahau kabisa kuwa kengold kutoka Mbeya nayo imepanda ligi kuu na ndiyo timu iliyoongoza kwa point 70 na kufuatiwa na pamba iliyopata point 67

lakini ukisikiliza redio na wachambuzi wa michongo wanaisifu Pamba muda wote utadhani imepanda peke yake ligi kuu

oya wachambuzi wa clouds media na wachambuzi wengine chambueni timu zote na siyo kuchambua timu moja kwa kua mmekula ng'ombe
Kwani Kengold ni timu ya kutoka mkoa wa Mbeya au Songwe?
 
We jamaa sometimes unafeli. Yaani kwa historia ya Pamba unataka iongelewe sawa na KenGold? Level za KenGold ni kuongelewa na wachambuzi aina yako inatosha. Hata hapo hapo Chunya pamoja na nationalism kubwa miongoni mwa Wanyaki watakuwa wanaiongelea zaidi Pamba kuliko KenGold
Anafeli vipi wakati ameelezea vizuri tu. Pamoja na hiyo historia ya Pamba bado wachambuzi hawakuvutwa nayo kuiongelea, wameanza kuiongelea baada ya kupewa Mwaliko wa nyama za ng’ombe na hapo ndiyo hoja yake ilipo.
Maana kabla ya huo mwaliko timu zote ziliongelewa, ila baada ya mwaliko hali ikabadilika.
 
Back
Top Bottom