Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,077
- 22,790
Wabunge walipe kodi. Katika nchi nyingi ulipaji wa kodi ni majawapo katika sifa kuu kwa wagombeaji wa ubunge kuwa nayo ili wakidhi kuchaguliwa.
Ni wazi kuwa kwa Wabunge wetu hawa kwa kutolipa kutolipa kodi wanakosa uhalali wa kuikosoa serikali pamoja na jukumu la kuhimiza ulipaji wa kodi.
Sasa hivi tunawaona wabunge wanavyoisifia Serikali kwa kuwatoza kodi kibao wananchi wanaowawakilisha kama chanzo kikuu cha mapato.
Swali linalonisumbua kama mwananchi ni sababu zipi zilipelekea hawa wawakilishi wetu wenye kipato na marupurupu maradufu kutolipa kodi.
Kila mbunge anayesimama bungeni cha kwanza kinachotoka kinywani kwake ni shukhrani kwa serikali na sifa pekee kwa kingozi Mkuu wa serikali.
Je bunge letu ni rubber stamp ya serikali na Rais wa nchi? Je kutolipa kodi ni mojawapo katika utekelezaji wa state sponsored corruption?
Hata wakitumia lugha gani katika utetezi ukweli utabaki pale pale; kwa kutolipa kodi wabunge wetu wanakula rushwa inayotolewa na serikali.