Tresor Mandala
JF-Expert Member
- Aug 20, 2010
- 38,081
- 79,964
Felix hajafeliWatu wengi wamesahau yale yalokuwa yakifanywa na Hybyarimana dhidi ya watutsi kabla ya mauaji ya Kimbari.
Sasa hivi Tshisekedi amefeli mambo makuu matatu ambayo yatoa ishara ya kurudi kwa mambo yale ya miaka ya 1990s:
1. Ameshindwa kuwarudisha wakimbizi wa Congo DRC wanoishi uhamishoni katika nchi jirani kwa miongo zaidi ya miwili.
2. Ameshindwa kuukubali ukweli na kuzidi kukataa kuwatambua watutsi walozaliwa ndani ya Congo DRC ambao wao shida yao ni kutambuliwa kama raia halali wa Congo DRC. Watutsi hawa ndio wengi wanounda kundi la M23.
3. Kuwalinda watutsi hao wa Congo DRC na kuwabatiza majina kuwa hao ni wahalifu wa kigeni walojipenyeza kuingia Congo DRC na hivyo kuhimiza kampeni dhidi yao ambayo ni kuwadhuru na kuwaua jambo linosababisha M23 waendelee kupata mafunzo na vifaa vya kujilinda (tuhuma kwa Rwanda) dhidi ya udhalimu huo.
Tshisekedi pia amefanya jambo jingine baya sana ambalo ni kuwaingiza waasi wa Congo waso watutsi na kuwachochea hasira dhidi ya waasi wa M23 ambao ni watutsi wenye asili ya Rwanda walozaliwa Congo.
Kagame anavyokuja na kutoa kauli zake yabidi kuketi na kumwelewa maana amelenga kuzungumzia nguvu inotokea nje.
Huu mkono usoonekana (invisible hand) ni wa kuuogopa na kuchukua tahadhari ya juu na Tanzania inapojihusisha na mgogoro huu ni lazima ifanye hivyo kwa tahadhari na uangalifu.
Jambo la msingi hapa ni kuelewa kuwa waasi wa M23 wakalia hazina kubwa ya utajiri wa madini katika jimbo waliloko ya Kivu.
Nimeeleza katika uchambuzi wa masuala makuu ya msingi ya kuyatambua katika kutatua mgogoro wa waasi wa kitutsi na serikali ya Congo DRC hapa: Uchambuzi: Mambo ya msingi kabisa ya kuyatambua kuhusu mgogoro wa wapiganaji wa M23 na Congo DRC na mapendekezo ya nini kifanyike
Kinoendelea hapa ni mtiririko wa matukio ambayo ipo siku hayataishia mahala pazuri.