Vyombo vya Plastic husababisha ugumba

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,977
15,525
Uchambuzi wa kitabu cha Lisa EATING TO CONCEIVE, (Kula Upate Mimba)

Kanuni ya 16 na ya Mwisho:Usitumie Vyombo vya Plastiki, Husabisha Ugumba

1. Mwandishi Lisa anasema *usitumie vyombo vya plastiki kuwekea vyakula vya moto kama chai, maziwa, supu, maji, ugali, wali nk kama una mpango wa kupata mimba.
2. Plastiki inapopata moto huzalisha kemikali iitwayo BPA (Bisphenol A) ambayo ikiingia mwilini huvuruga homoni na kusabaisha ugumba.
3. Na ikitokea umepata mimba basi inaweza kuharibifu.
4. Lakini pia Lisa anasema kemikali hii ni hatari kwa mwanaume maana inaua nguvu za kiume na hivyo kushindwa kuzalisha.
5. Ikitokea umempa mimba mama yoyo basi mtoto atakuwa dhaifu sana; hospitali kila siku.
6. Unaona hii ishu ilivyo hatari?
7. Sasa kuna waapishi hufunikia mifuko ya plastiki wakati wa kupika kwamba inasaidia kuivisha chakula haraka.
8. Kwamba plastiki husaidia mvuke wote hubaki ndani na chakula kuiva vizuri.
9. Mada hii ilinivutia nikaendelea kuitafiti zaidi. Niliyokutana nayo sisi, mwe! Kidogo nikimbie!
10. Kwamba matumizi ya vyombo vya plastiki huongeza unene kwa sbb kemikali zinazopatikana kwenye plastiki hubadili seli shina kuwa seli za mafuta.
11. Ndiyo maana unafanya mazoezi kila siku lakini hupungui. Kitambi kimekung'ang'ania hadi kero😄. Kumbe shida vyombo!
12. Sa itakuaje? Maana wengi tunachemsha maji ya kunywa, tunaweka kwenye ndoo yapoe kisha tunahamishia kwenye firiji. Ahoo! Kumbe tunajimaliza ati!🫢🫢
13. Kwamba vyombo vya plastiki husababisha aina 52 za kansa, wanasema wataalam wa kansa kutoka Hospitali ya kansa Johns Hopkins Marekani.
14. Au ndiyo maana kesi za kansa zinashamiri kwa kasi? Siku hizi kuna kansa mpaka ya kongosho!
15. Kwamba kifaa cha plastiki kinapo pata joto au baridi kali hutoa kemikali ya Dioxin inayo sababisha kansa.
16. Halafu haya mambo kama hayajakupata utaona hizi stori ni sound tupu!
17. Sasa tunaogonga maji ya chupa baridiiiii kutoka kwenye friji tuacheni. Kinga ni bora kuliko tiba!
18. Hata watoto wetu wanaonyonya barafu baridiii kwenye mifuko ya plastiki tuwafundishe waache! Madhara ya hii kitu huchukua mpaka miaka 10 ndo yanaanza kuonekana wanasema wataalamu.
19. Kwamba ukikutana na mtu ana kansa basi alianza kuipata zamani, siyo leo. Miaka 10 iliyopita!
20. Kwamba matumizi ya vyombo vya plastiki husababisha mtu kupoteza kumbukumbu.
21. Au ndiyo maana tunasahau sana? Maana ukiweka kitu sehemu kukumbuka ulipoweka ni ntihani😄😄. Hasa funguo. Zinatesa sana!
22. Au tiketi ya basi🫢😌. Konda akianza kukagua unaikosa. Unatafuta weee, akipita ndo unaiona! Nyie!!
23. Sasa sipati picha hii kitu itakuwa imejeruhi kumbukumbu za watoto wetu kwa kiasi gani.
24. Maana watoto wetu marufuku kutimia vyombo vya udongo na glasi.
25. Wao ni maplastiki. Kwamba wasiungue, kwamba watavunja vyombo vya wageni🫢🫢.
26. Matokeo yake tunavunja kumbukumbu zao. Unakuta katoto kanafanya kosa, unakachapa, baada ya muda, kanarudia kosa lile, unakachapa tena.
27. Unaweza kudhani kanafanya makusudi. Kumbe kanasahau maskini ya Mungu. Tuwanusuru watoto wetu!
28. Wataalamu wanasema kemikali hizo za plastiki kwa watoto zinaharibu kinga yao hali inayosababisha homoni kubadilika na kusababisha matatizo katika tabia. Watoto wa kiume kama mabinti tu. Hatari.
29. Sasa kuna wengine wanawasha jiko la mkaa kwa kutumia mifuko ya plastiki. Moshi unasambaa nyumba nzima. Hatari juu ya hatari.
30. Sikiliza kelele za mama sasa akiwa jikoni. Happyiii, niletee kisu na wakati alikuwa nacho mwenyewe. Hakumbuki alikiweka wapi😄😄
31. Jamani. Tuacheni vyombo vya plastiki. Tuanze kutumia vyombo vya wageni😄.Maana kila nyumba vipo!
32. Tunafanyaje hapa wazee?
33. Wataalamu wanashauri kutumia vyombo vya udongo,chuma na hata miti kama vile ungo na vyungu na mitungi na vibuyu.
34. Nunua limtungi lako, weka hapo mambo safi. Maji mnanywe kata. Chakula kama vipi funikia majani ya migomba kama wahaya!
35. Ndiyo sasa kama huwezi vyombo vya maglasi siujirudie kwenye miti, vibuyu na vyungu.
36. Ni kweli maisha bila plastiki hayawezekani. Lakini tufanyaje sasa. Tukubali kuugua kansa, kuwa gumba, kupoteza kumbukumbu?
37. Hapana. Tubadilike. Kuishi kwa kula dawa nako ni mtihani mgumu maana ukisahau umekufa!

Narudia

1. Usiweke chakula kwenye kontena la plastiki na kisha kupasha moto kwa kutumia microwave.

2. Usitumie chupa ya plastiki kwa kugandisha maji ya kunywa! Acha kula na barafu pia.

3. Ufungaji wa chipsi za moto na kunywea chai ya moto kwenye vikombe vya plastiki vikomee!

Cheers
Mwl. Denis Mpagaze
Muhenga wa Karne ya 21!
 
Hii ni kweli. Hizo biphenols zina chemical structure kama za baadhi ya hormone za uzazi. Ukizitumia zinaenda kuvuruga mpangilio wa hormones. Kunywa chai kwenye vikombe vya plastiki ni hatari.
 
Nikikutana na Rais Mojawapo ya mambo nitamshauri ni pamoja na hili jambo.
Ni uda mrefu nimekuwa nikiwiwa nalo.

Kwamba Serikali ipige marufuku matumizi ya vyombo vya plastic sababu ni hatari kwa afya.

Kama vile ambavyo ilipiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastic halikadhalika na matumizi ya vyombo vya plastic yafanyike haraka sana kuokoa maisha ya watanzania wengi.

Watu wote wa hali ya chini ambao ndio wengi zaidi nchini wanatumia vyombo vya plastic sababu ndio nafuu kupatikana, bei ni magii sana.
Lakini ni hatari kiafya.
Hata vikioshwa havitakati. Ukiweka Chakula au kinywaji cha moto unakula na uchafu unayeyuka 🙆‍♂️

Mamalishe karibia wote wa mjini na vijijini wanatumia vyombo vya plastic.

Wanadumbukiza kwenye Maji na kutoa 😭
Ni huzuni kwa kweli.

Kwako Rais na Waziri wa afya chukueni hatua haraka ya kupiga matufuku matumizi na uingizwaji na uzalishaji wa vyombo vya plastikowy
 
Uchambuzi wa kitabu cha Lisa EATING TO CONCEIVE, (Kula Upate Mimba)

Kanuni ya 16 na ya Mwisho:Usitumie Vyombo vya Plastiki, Husabisha Ugumba

1. Mwandishi Lisa anasema *usitumie vyombo vya plastiki kuwekea vyakula vya moto kama chai, maziwa, supu, maji, ugali, wali nk kama una mpango wa kupata mimba.
2. Plastiki inapopata moto huzalisha kemikali iitwayo BPA (Bisphenol A) ambayo ikiingia mwilini huvuruga homoni na kusabaisha ugumba.
3. Na ikitokea umepata mimba basi inaweza kuharibifu.
4. Lakini pia Lisa anasema kemikali hii ni hatari kwa mwanaume maana inaua nguvu za kiume na hivyo kushindwa kuzalisha.
5. Ikitokea umempa mimba mama yoyo basi mtoto atakuwa dhaifu sana; hospitali kila siku.
6. Unaona hii ishu ilivyo hatari?
7. Sasa kuna waapishi hufunikia mifuko ya plastiki wakati wa kupika kwamba inasaidia kuivisha chakula haraka.
8. Kwamba plastiki husaidia mvuke wote hubaki ndani na chakula kuiva vizuri.
9. Mada hii ilinivutia nikaendelea kuitafiti zaidi. Niliyokutana nayo sisi, mwe! Kidogo nikimbie!
10. Kwamba matumizi ya vyombo vya plastiki huongeza unene kwa sbb kemikali zinazopatikana kwenye plastiki hubadili seli shina kuwa seli za mafuta.
11. Ndiyo maana unafanya mazoezi kila siku lakini hupungui. Kitambi kimekung'ang'ania hadi kero😄. Kumbe shida vyombo!
12. Sa itakuaje? Maana wengi tunachemsha maji ya kunywa, tunaweka kwenye ndoo yapoe kisha tunahamishia kwenye firiji. Ahoo! Kumbe tunajimaliza ati!🫢🫢
13. Kwamba vyombo vya plastiki husababisha aina 52 za kansa, wanasema wataalam wa kansa kutoka Hospitali ya kansa Johns Hopkins Marekani.
14. Au ndiyo maana kesi za kansa zinashamiri kwa kasi? Siku hizi kuna kansa mpaka ya kongosho!
15. Kwamba kifaa cha plastiki kinapo pata joto au baridi kali hutoa kemikali ya Dioxin inayo sababisha kansa.
16. Halafu haya mambo kama hayajakupata utaona hizi stori ni sound tupu!
17. Sasa tunaogonga maji ya chupa baridiiiii kutoka kwenye friji tuacheni. Kinga ni bora kuliko tiba!
18. Hata watoto wetu wanaonyonya barafu baridiii kwenye mifuko ya plastiki tuwafundishe waache! Madhara ya hii kitu huchukua mpaka miaka 10 ndo yanaanza kuonekana wanasema wataalamu.
19. Kwamba ukikutana na mtu ana kansa basi alianza kuipata zamani, siyo leo. Miaka 10 iliyopita!
20. Kwamba matumizi ya vyombo vya plastiki husababisha mtu kupoteza kumbukumbu.
21. Au ndiyo maana tunasahau sana? Maana ukiweka kitu sehemu kukumbuka ulipoweka ni ntihani😄😄. Hasa funguo. Zinatesa sana!
22. Au tiketi ya basi🫢😌. Konda akianza kukagua unaikosa. Unatafuta weee, akipita ndo unaiona! Nyie!!
23. Sasa sipati picha hii kitu itakuwa imejeruhi kumbukumbu za watoto wetu kwa kiasi gani.
24. Maana watoto wetu marufuku kutimia vyombo vya udongo na glasi.
25. Wao ni maplastiki. Kwamba wasiungue, kwamba watavunja vyombo vya wageni🫢🫢.
26. Matokeo yake tunavunja kumbukumbu zao. Unakuta katoto kanafanya kosa, unakachapa, baada ya muda, kanarudia kosa lile, unakachapa tena.
27. Unaweza kudhani kanafanya makusudi. Kumbe kanasahau maskini ya Mungu. Tuwanusuru watoto wetu!
28. Wataalamu wanasema kemikali hizo za plastiki kwa watoto zinaharibu kinga yao hali inayosababisha homoni kubadilika na kusababisha matatizo katika tabia. Watoto wa kiume kama mabinti tu. Hatari.
29. Sasa kuna wengine wanawasha jiko la mkaa kwa kutumia mifuko ya plastiki. Moshi unasambaa nyumba nzima. Hatari juu ya hatari.
30. Sikiliza kelele za mama sasa akiwa jikoni. Happyiii, niletee kisu na wakati alikuwa nacho mwenyewe. Hakumbuki alikiweka wapi😄😄
31. Jamani. Tuacheni vyombo vya plastiki. Tuanze kutumia vyombo vya wageni😄.Maana kila nyumba vipo!
32. Tunafanyaje hapa wazee?
33. Wataalamu wanashauri kutumia vyombo vya udongo,chuma na hata miti kama vile ungo na vyungu na mitungi na vibuyu.
34. Nunua limtungi lako, weka hapo mambo safi. Maji mnanywe kata. Chakula kama vipi funikia majani ya migomba kama wahaya!
35. Ndiyo sasa kama huwezi vyombo vya maglasi siujirudie kwenye miti, vibuyu na vyungu.
36. Ni kweli maisha bila plastiki hayawezekani. Lakini tufanyaje sasa. Tukubali kuugua kansa, kuwa gumba, kupoteza kumbukumbu?
37. Hapana. Tubadilike. Kuishi kwa kula dawa nako ni mtihani mgumu maana ukisahau umekufa!

Narudia

1. Usiweke chakula kwenye kontena la plastiki na kisha kupasha moto kwa kutumia microwave.

2. Usitumie chupa ya plastiki kwa kugandisha maji ya kunywa! Acha kula na barafu pia.

3. Ufungaji wa chipsi za moto na kunywea chai ya moto kwenye vikombe vya plastiki vikomee!

Cheers
Mwl. Denis Mpagaze
Muhenga wa Karne ya 21!

serikali hamasisheni matumizi vya vyombo vya bati , walau hivi vina afadhali.

Though vya udongo ni vizuri zaidi.
 
Back
Top Bottom