Vijana tunaomba umri wa kustaafu uwe miaka 45 hiari na 55 lazima

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,275
7,840
Kuelekea siku ya wafanyakazi nchini Mei mosi, vijana ambao wanahitimu elimu ya vyuo vikuu tunaomba Serikali yetu chini ya Rais wetu mpendwa Mama Samia na timu yake yote tunamuomba jambo moja nalo ni;

1. Umri wa kustaafu upunguzwe uwe miaka 45 hiari na 55 iwe lazima, badala ilivyo sasa kuwa 50 hiari na 55 hadi 65 lazima.

Suala hili la umri wa kustaafu limekuwa kikwazo kikubwa kwa upatikanaji wa nafasi kwa kundi kubwa la vijana wanao hitimu vyuo vikuu.

Utafiti unaonyesha kwenye idara mbalimbali za serikali kuna wazee wengi ambao tayari wamechoka, hawana tija, hivyo ni vyema umri wa kustaafu ukapunguzwa ili kupisha vijana nao walitumikie taifa lao.

1.Umri wa kustaafu uangaliwe upya.
2. Kuwepo na ajira za mkataba maalum, ajira za masharti ya kudumu ziondolewe.

Tunaomba mapendekezo hili lizingatiwe.
 
Kuelekea siku ya wafanyakazi nchini Mei mosi, vijana ambao wanahitimu elimu ya vyuo vikuu tunaomba Serikali yetu chini ya Rais wetu mpendwa Mama Samia na timu yake yote tunamuomba jambo moja nalo ni;

1. Umri wa kustaafu upunguzwe uwe miaka 45 hiari na 55 iwe lazima, badala ilivyo sasa kuwa 50 hiari na 55 hadi 65 lazima.

Suala hili la umri wa kustaafu limekuwa kikwazo kikubwa kwa upatikanaji wa nafasi kwa kundi kubwa la vijana wanao hitimu vyuo vikuu.

Utafiti unaonyesha kwenye idara mbalimbali za serikali kuna wazee wengi ambao tayari wamechoka, hawana tija, hivyo ni vyema umri wa kustaafu ukapunguzwa ili kupisha vijana nao walitumikie taifa lao.

Tunaomba pendwkezo hili lizingatiwe.
Vijana qenyewe ndio mnaokalia uzushi tu?
 
Huko kwenye chama mtu ana umri 70 bado anapewa kazi ccm hii sio sawa kabisa
Mfano cheo cha urais
 
Endapo umri wa kustaafu utapu guzwa na kuwa miaka 45 kwakiasi kikubwa itapunguza tatizo la ajira.

Shida wazee wameziba nafasi za vijana.
 
Sikia ujumbe wenu huu hapa vijana mnaolilia Ajira! Serikali siyo mjinga ikaajiri watu wasio na uwezo!
 
Attachments

  • IMG-20240428-WA0007.jpg
    IMG-20240428-WA0007.jpg
    76.8 KB · Views: 3
Wazee vipi mbona hamtaki kustaafu????achieni vijana nafasi. Unataka kuifia ofisini?!!!
Uliona wapi watu wanakufa wakiwa na miaka 55? UN inasema umri wa kustaafu ni miaka 65 huyo ndiye mzee, sisi wenye below 60 bado tuna tija kwa Taifa! Zamu yako itafika ila kumbuka serikali haiajiri wenye zaidi ya miaka 45 kwa ajira ya kwanza!
 
Vijana na nyie akili zenu sijui mnazitumiaje
Sasa kama mnategemea kutustaafisha kwa lazima kwanini nyie na akili zenu msiwe wabunifu?
Siku hizi mchina anatengeneza mashine za kila aina tena ndogo unaweka hata kuweka chumbani ila unaweza kusambaza bidhaa zako

Kwanza je wewe unaweza kustaafu na 45? Utafanya nini na nguvu bado unazo?

Hakuna mahali duniani wanastaafishwa na 45 labda jeshini tu
 
Uliona wapi watu wanakufa wakiwa na miaka 55? UN inasema umri wa kustaafu ni miaka 65 huyo ndiye mzee, sisi wenye below 60 bado tuna tija kwa Taifa! Zamu yako itafika ila kumbuka serikali haiajiri wenye zaidi ya miaka 45 kwa ajira ya kwanza!
Je, unafahamu kwa sasa umri wa kuishi (life span)kwa mtanzania ni miaka 45 hadi 50??
Sasa wewe una miaka 55, 60 unatafuta nn kama sio kifo.
 
Back
Top Bottom