Black Opal
JF-Expert Member
- Jan 22, 2023
- 201
- 262
Wazee wa maakuli kwema?
Naomba tutumie uzi huu kuweka recipes mbalimbali za juice tupate vinywaji amazing kipindi hiki cha sikukuu.
Ili kufanya juice yangu iwe bomba huwa nafanya haya katika mchanganyiko ninaotengeza;
- Ikiwa matunda ni matamu sana labda umetumia maembe yameiva sana pamoja na parachichi, ama embe na tikiti, huwa naongeza ka ndimu/limao pamoja na tangawizi kiasi, hii inaongeza ladha na kufanya juice ichangamke
Ikiwe juice ina matunda yenye asili ya uchangu, kama vile pensheni, ukwaju, machungwa hapa naweka maganda ya limao (unakwangua tu limao yako baada ya kuiosha vizuri na kuweka maganda yake) ambayo yanaongeza harufu nzuri pamoja na iriki, hii pia inasaidia kuweka harufu nzuri
Kwenye michangayiko yote huo unaweza ukaweka ladha za juice kama vanila (inategemea hasa wewe unapendelea nini, ila mi sio mpenzi sana wa hizi).
Pia kwenye matunda ambayo unalazimisha kuchemsha maji ndio utengeneze mchanganyiko wako wa juice mfano kwenye juice ya mabungo, ukwaju au rozela, kunakuwa na tofauti sana kama utachemsha tunda alo pamoja na sukari, kuna ka ladha fulani hivi kanachomoza ambako huwezi kukakapata kama utaweka sukari baadae maji yakiwa yamepoa.
Kwa wapenzi wa mchaichai pia unaweza kuchemshia kwenye juice zinazokuhitaji kuchemsha matunda/kutumia maji ya moto. Hii huongeza harufu nzuri kwenye juice yako na kuongeza hamu zaidi ya kuinywa.
Kwenu wazee wa misosi, unafanyaje kuongeza utamu na kufanya juice yako iwe ya kipekee?