UWT Taifa Wawafikia Waathirika wa Mafuriko Wilaya ya Kilombero (Ifakara) Kuwapa Msaada wa Kibinadamu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,994
961
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda ameongozana na Wajumbe wa Kamati ya Maafa ya UWT Taifa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Norah Waziri Mzeru wamefika Wilaya ya Kilombero kutoa Msaada kwa waathirika wa Mafuriko

Miongoni mwa viongozi walioambatana na Mwenyekiti UWT Taifa, Chatanda ni pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Norah Waziri Mzeru ambaye naye amekabidhi kiasi cha fedha kwa wafiwa walipokwenda kuwapa faraja ya misaada ya Kibinadamu.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Norah Waziri Mzeru amemshukuru sana Mwenyekiti Chatanda kwa kufika mpaka nyumbani kwa waathirika wa Mafuriko huku wanawake wa Morogoro wakimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuma wasaidizi wake ili kuwapa faraja na misaada ya Kibinadamu.

Aidha, Shuhuda wa ajali Mafuriko iliyopelekea kifo amesema Mabinti wawili waliokuwa kwenye Mtumbwi, Mvua na upepo ulivyozidi Mtumbwi ulipinduka na binti mmoja alikuwa amebeba mtoto, alivyokufa mwili wake ukawa unaelea pamoja na mtoto wa miezi mitano ambaye mtoto aliokolewa akiwa hai.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-04-24 at 14.29.22.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-24 at 14.29.22.jpeg
    403.1 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-04-24 at 14.29.21.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-24 at 14.29.21.jpeg
    375.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-04-24 at 12.45.28.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-24 at 12.45.28.jpeg
    150.4 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-04-24 at 12.45.27.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-24 at 12.45.27.jpeg
    177.1 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-04-24 at 10.46.00.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-24 at 10.46.00.jpeg
    111.9 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-04-24 at 10.45.58(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-24 at 10.45.58(1).jpeg
    127.5 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-04-24 at 10.45.58.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-24 at 10.45.58.jpeg
    130.8 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-04-24 at 10.45.57.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-24 at 10.45.57.jpeg
    132.5 KB · Views: 1
Back
Top Bottom