Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro uboreshwe

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,900
KIA Airport mimepita karibuni nikitokea Doha, walishuka watalii zaidi 200.

Bahati ilikuwa asubuhi nimeweza kuona vizuri mandhari na mazingira yake, ni Airport iliyo eneo zuri na panaweza kuwezeshwa kuwa Airport ya kipekee hapa nchini kwani pana nafasi kubwa sana ya kuwezesha kujenga runways kwa namna yo yote kuwezesha ndege kutua kwa usalama zaidi.

Jambo la kushangaza Airport hii ni ya miaka mingi tangu zama za Nyerere na ikiwa ni gate way ya watalii, lakini anayefika kwa mara ya kwanza anaweza kupata wasiwadi maana panaonekana ni porini kana kwamba ndege imetua Loliondo au Seronela.

Abiria hushuka kwenye ndege na kutembea kwa miguu kwenda nyumba ya checkout for security checkpoint, hiyo ni international Airport. Sikuona movement ya huduma kwa disable passengers.

Pako kimya sana, na hakuna hata jengo la hotel lililo karibu na Airport hata lodge hakuna. International Airports nilizoona nchi mbalimbali bara la Ulaya, Asia na America pale pale Airport huwa kuna hoteli za kitali. Mjini Arusha na Moshi yes zipo lakini baadhi hupendelea karibu na airport.

Kawaida mazingira ya Airport husaidia watalii kupata picha ya hali ya nchi ilivyo kwa maendeleo na uchumi, kwa hali ilivyo ukiongozana na wageni wakati ulikotokea nao ulijidai na ukifika utaanza kujisikia vibaya.

Nashauri serikali iwe na mipango ya kuboresha KIA Airport kwa kujenga hotel za kitalii kwa kuwa KIA ni gate way ya watalii nchini.

Pafunguliwe shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kiuchumi ili kuwezesha kuondoa hali iliyopo inayoonekana ndege imetua porini.

Serikal8 pia ifungue milango kwa wawekezaji ili wapapendezeshe KIA yetu.

Pale KIA Airport pajengwe jengo lenye hadhi ya shughuli za Airport kwa mazingira ya kuvutia watalii na wawekezaji.

Jamani KIA serikali ifungue macho zaidi, utalii huliingizia taifa pesa za kutosha kila mwaka. Itapendeza KIA kwa sasa iende na wakati.

TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE!
 
Attachments

  • InCollage_20240425_081301995.jpg
    10 MB · Views: 2

Kwanaza kabisa unatakiwa utambue huo uwanja ulijengwa kwenye eneo ambalo lilikuwa ni nia ya wanyama kuhama toka Arusha kwenda Kilimanjaro. Uwanja huo ulijengwa na Waisraeli enzi ya Hayati Mwalimu Nyerere baada ya kuona watalii wanashukia Nairobi kwa ajili ya kuja kupanda mlima Kilimanjaro. Turudi kwenye mada yako ni kweli kwa sasa uwanja unahitaji baadhi ya vitu siyo tu kwa watalii wanaotembelea hata wananchi wanaokwenda kupokea wageni. Inasikitisha hakuna sehemu nzuri ya kukaa kama Dar Es Salaam ambapo utapata huduma ya chakula na kinywaji na hata screen kwa kuangalia news na mambo mengine. Yes hata jengo lingeangaliwa upya liendane na mahitaji ya sasa kama eneo la kuondoka wageni ni dogo na hata wanaowasili. Lakini pia magetini kumekuwa na njia moja ya kuingia na moja ya kutoka kitu ambacho kinaleta foleni kubwa sana kwa wanaoingia na kuondoka uwanjani. Kwenye hoteli hapo kidogo ntatofautiana na wewe kwani ukishaweka hoteli maeneo hayo kunaweza changia mahoteli ya Arusha na Moshi kukosa boashara lakini pia kwa wenzetu wanaofanya biashara ya usafirishaji. Uzuri uliopo wa asili ndiyo kivutio kikubwa mandhari ya ukiwa unatoka KIA kuelekea Arusha-Moshi Road unaweza uona mlima Kilimanjaro kwa ukaribu na unavyopendeza.Kumbuka lengo la watalii ni kuja kuona vivutio vilivyopo hasa Mlima na Mbuga. Sasa tukijenga mahoteli ile madhari yote ya kivutio kuwa uwanja wa ndege upo kwenye mazingira ya kitalii itapoteza maana.
 
Upo sahihi na ukitazama hiyo zone ni ya kitalii wageni ni wengi, ila hata hizo ndege kama pre*** ni kama boti ndege zenyewe zinatia huruma, wizara husika waboreshe usafiri wa anga na miundombinu yake
 
Kulikuwa na fununu za uwanja huu umebinafsishwa labda ndio maana hawauendelezi wanangoja mwekezaji aweke yeye pesa.
 
Tunaotumia huu uwanja mara kwa mara tunaona ipo nafuu kubwa tofauti na mwanzoni. Japo haizuii hoja yako ya kupaendeleza ila Natalia na volume ya abiria wanaopita hapo
 
Waondoe vyombo visivyofanya kazi pale uwanjani.

Kuna gari la zimamoto bovu limetelekezwa pale na bahati mbaya ni karibu na parking ya ndege za abiria.

Ile ndege mbovu ya jeshi la waarabu pia iondolewe maana pale sio mahali pa maonyesho ya junky.
 
Ndege mbovu ya jeshi la waarabu iliyotelekezwa KIA Airport kwa kipindi kirefu sasa
 
Attachments

  • 20240222_090020.jpg
    20240222_090020.jpg
    2.9 MB · Views: 2
Ule Uwanja uko vizuri pale ulipo.
Ni mshamba tu Kama wewe ndio atapenda kulala kwenye hoteli iliyo karibu na airport ili aone midege na kuamshwa na kelele kila Mara ndege zikitua na kupaa.
Umeenda Doha Mara moja unataka kutufundisha Nini wewe?
Kama Kuna barabara za kwenda Arusha kwenye hoteli fasta, what is the problem?
 
Point Mkuu. Pata k-vant. Katika viwanja unique basi KIA ni kimojawapo. Kipo mbali na mji kama Ilivyo Cairo. Mgeni anapata wasaa wa kuona mandhari ya nchi kabla ya kuingia mjini
 
Kwanaza kabisa unatakiwa utambue huo uwanja ulijengwa kwenye eneo ambalo lilikuwa ni nia ya wanyama kuhama toka Arusha kwenda Kilimanjaro. Uwanja huo ulijengwa na Waisraeli enzi ya Hayati Mwalimu Nyerere baada ya kuona watalii wanashukia Nairobi kwa ajili ya kuja kupanda mlima Kilimanjaro. Turudi kwenye mada yako ni kweli kwa sasa uwanja unahitaji baadhi ya vitu siyo tu kwa watalii wanaotembelea hata wananchi wanaokwenda kupokea wageni. Inasikitisha hakuna sehemu nzuri ya kukaa kama Dar Es Salaam ambapo utapata huduma ya chakula na kinywaji na hata screen kwa kuangalia news na mambo mengine. Yes hata jengo lingeangaliwa upya liendane na mahitaji ya sasa kama eneo la kuondoka wageni ni dogo na hata wanaowasili. Lakini pia magetini kumekuwa na njia moja ya kuingia na moja ya kutoka kitu ambacho kinaleta foleni kubwa sana kwa wanaoingia na kuondoka uwanjani. Kwenye hoteli hapo kidogo ntatofautiana na wewe kwani ukishaweka hoteli maeneo hayo kunaweza changia mahoteli ya Arusha na Moshi kukosa boashara lakini pia kwa wenzetu wanaofanya biashara ya usafirishaji. Uzuri uliopo wa asili ndiyo kivutio kikubwa mandhari ya ukiwa unatoka KIA kuelekea Arusha-Moshi Road unaweza uona mlima Kilimanjaro kwa ukaribu na unavyopendeza.Kumbuka lengo la watalii ni kuja kuona vivutio vilivyopo hasa Mlima na Mbuga. Sasa tukijenga mahoteli ile madhari yote ya kivutio kuwa uwanja wa ndege upo kwenye mazingira ya kitalii itapoteza m

Ule Uwanja uko vizuri pale ulipo.
Ni mshamba tu Kama wewe ndio atapenda kulala kwenye hoteli iliyo karibu na airport ili aone midege na kuamshwa na kelele kila Mara ndege zikitua na kupaa.
Umeenda Doha Mara moja unataka kutufundisha Nini wewe?
Kama Kuna barabara za kwenda Arusha kwenye hoteli fasta, what is the problem?
Jadili hoja iliyoletwa, usimjadili metal hoja. Tujifunze kufanya debate kwa ustaarabu
 
Ule Uwanja uko vizuri pale ulipo.
Ni mshamba tu Kama wewe ndio atapenda kulala kwenye hoteli iliyo karibu na airport ili aone midege na kuamshwa na kelele kila Mara ndege zikitua na kupaa.
Umeenda Doha Mara moja unataka kutufundisha Nini wewe?
Kama Kuna barabara za kwenda Arusha kwenye hoteli fasta, what is the problem?
Mkuu doha ni transit tu. Usikute katokea newzealand, Australia, Canada ama marekani huko.
 
Kati ya Airports nilizoziona kwenye mabara kadhaa, KIA ni moja ya airport chache zenye eneo zuri lisilo na miinuko karibu wala utitiri wa majengo.

Mfano Airport ya Zurich huko Switzland barani Ulaya iko bondeni karibu na ziwa Zurich, full mountain ranges na ukichungulua nje mwenye moyo mchache unsogopa.

Tatizo la KIA ni iboreshaji, hata jengo la huduma za wasafiri liko poor kidogo.
 
Back
Top Bottom