Utekelezaji wa ukusanyaji wa kodi ya majengo kupitia mita za luku

TRA Tanzania

Member
Jul 16, 2022
82
230
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA )kwa Kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) tunapenda toa ufafanuzi kuhusiana na Utekelezaji wa ukusanyaji wa kodi ya majengo kwa kutumia njia ya ununuzi wa umeme kwa wamiliki wa majengo ya Ghorofa kama kiambatanisho hapa
PRESS lUKU.jpeg
 
Kwa iyo baada ya sensa ndio mmejua ghorofa ziko ngapi na mmeshabikia pesa ngapi mtashirikiana serikali kuiba ili CAG apate kazi eeh?
 
Kama ghorofa lina Floor kumi ni 60,000x10=600,000
Kama floor 1 ni 60,000x2=120,000
 
Huu ni wizi aisee. Yaani hakuna mizani kabisa kwamba nyumba isiyo ya ghorofa ilipe elfu 12 halafu ghorofa kila sakafu ilipe elfu 60. Walau wangesema ghorofa ichajiwe kama nyumba mbili, yaani elfu 24 nk
Au waseme floor ya chini inachajiwa kama nyumba ya kawaida elfu 12 na zinazofuata ni elfu 24, kidogo ingekuwa sawa. Tofauti ya bei imekuwa kubwa sana.
 
Kwny Bandiko lenu,
Mnasema mnatoza kuanzia julai 2021,

Ila mimi juzi nmekuta deni la 13,000 wkt kila mwezi wanakata bukubuku ya jengo.

Maelezo ya tanesco ni kwamba mnatoza kodi kuanzia mita yangu ilipoanza kutumika january 2021, na sio sheria ilivopitishwa julai 2021.

Imekaaje hii

Sent using JamiiForums mobile app
Jana usiku umeme uliisha kwenye mita yangu. Nikanunua shilingi elfu 9 kwa tigopesa, nashangaa muamala unasitishwa kila naponunua. (Ninatumia tarrif ya chini ile) umeme wa elfu 9 unanitosha kwa mwezi mzima.

Ikabidi nipige simu tigo, wakaniambia kuwa mita inadaiwa shilingi laki 1 deni ya kodi ya majengo kwa mwaka 2022/23, kwa hiyo ninunue umeme wa kuanzia Tshs. 100,000/= ndio itakubali.

Kwa kweli nimeshangaa na kusikitika sana. Nyumba ni andagraundi, imehesabika kuwa ni ghorofa, na muda wote nilikuwa nalipa elfu 1 kila naponunua umeme.

Sasa hii ya kufungia mita ili ninunue umeme wa laki kwa kweli ni uonevu, hapa ndio nimeelewa kwa nini wafanyabiashara wa Kariakoo waliandamana. Halafu mwaka 2022/23 unaisha mwezi huu, Juni 30, maana yake nitalipa laki na mwezi wa 7 watanifungia tena ili nilipe laki ya mwaka 2023/24..kisa vyumba viwili vya andagraundi.. TRA hapa mnazingua, mnachofanya ni wizi.
 
Sadly!!!

Hii 1K mbona mimi nakatwa mwaka wa pili huu?ina maana hata mimi kuna siku nitafungiwa madai sijalipa kodi ya jengo wakati kila mwezi wanakata?
 
Hawashindwi kufanya hivyo mkuu. Yaani kodi zao wanarudisha nyuma, hazianzii pale ulipoingia kwenye nyumba au pale wao walipopata taarifa sahihi kuhusu jengo lako, wanakutoza na za siku za nyuma kana kwamba wewe ndio ulikuwa hutaki kulipa.
 
Mtihani sana hii nchi.
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA )kwa Kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) tunapenda toa ufafanuzi kuhusiana na Utekelezaji wa ukusanyaji wa kodi ya majengo kwa kutumia njia ya ununuzi wa umeme kwa wamiliki wa majengo ya Ghorofa kama kiambatanisho hapa
View attachment 2610047
TRA mmetoa tangazo, lakini pia mgetangaza interpretation ya maneno " ghorofa sakafu na nyumba ya kawaida".

Mimi naona kama ni utendaji wa kukurupuka bila maandalizi.
TRA mgetangaza na interpretations za neno " ghorofa, sakafu na nyumba ya kawaida.

Hapo awali kodi ya majengo ilikuwa inalipwa kutokana professional valuations iliyokuwa inafanyiwa na halmashauri za miji husika.

Sasa ni flat rate, mimi nina manshion kubwa tu hapo Masaki sasa nitalipa sawa na nyumba iliyopo Chanika

TRA hapo awali kodi ilikuwa inakadiriwa kutokana na valuations inayofanwa na halmashauri za jiji.
Kwa hili tangazo ni utata mtupu. Nini interpretaions za " ghorofa,sakafu au nyumba ya kawaida".

Mimi nina manshion kubwa Masaki na babu yangu ana kibanda Chanika.Jee hizo zote ni nyumba ya kawaida?

Sakafu ikiwa na nyumba moja au nyumba 10 wanalipa vipi kama rate ni ya sakafu.

Kwa ghorofa yenye sakafu 2 na nyingine 14 zote ni sawa.
Tafadhalini naomba mtolee ufafanuzi kwa manufaa ya Tax Compliance
 
Mkuu, ni kweli kabisa zamani kodi ya jengo ilikuwa ikilipwa baada ya valuation kufanyika. JPM akaona huo ni wizi na kutengeneza mianyabya rushwa maana kulikua na uwezo wa kubageini kati ya valuer na mwenye nyumba, au valuer akiwa na bifu nawe anakukadiria parefu. Ikawa ni flat rate, elfu 12 kwa wote sasa hawajaridhika, wameleta hizi habari za Sakafu.

Halafu ajabu, Rais anayelipwa mshahara mkubwa kuliko watu wote wa serikali, amepewa msamaha wa kodi, Ikulu hailipi kodi ya jengo. Wasio na kazi na wenye vipato vya misheni town ndio tunapewa mzigo wa kuendesha nchi, sio kwa faida yetu bali ya kwao.

Karne hii kuwa na kodi za majengo ni kuwa na fikra za kizamani mno, kodi hii inatakiwa kufutwa. Dah, hapa nawaza hii laki naipataje niklie walau brenda iwake mwanangu ale mchanganyo.
 
Back
Top Bottom