Bunge la Wananchi
New Member
- Jan 30, 2023
- 4
- 5
Kifo cha Dk. Mkamilo aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TARI kimeacha simanzi na huzuni kubwa kwa wanataaluma wa masuala ya utafiti wa Kilimo ndani na nje ya Tanzania.
Kifo cha Dk. Mkamilo kimeacha maswali mengi sana kutokana na utata uliopo kwani Dk. Mkalimo hadi anastaafu alikuwa na afya njema na siku ya tarehe 20 Februari 2024 alikwenda kukabidhi Ofisi kwa Mkurugenzi mpya Dk. Thomas Bwana na baada ya tukio hilo akafariki dunia huku chanzo cha kifo chake hadi sasa kikiwa hakijulikani.
Sio Serikali, wala Wafanyakazi wa TARI wanaojua sababu ya Kifo cha Dk. Mkamilo, suala hili limeacha simanzi kubwa sana huku kukiwepo minong'ono mingi kuhusu kifo cha Dk. Mkamilo.
Wanaojua ukweli wa suala hili watuambie ili kuondoa sintofahamu kubwa iliyopo sasa.
"Tafiti za kilimo zilete mageuzi ya biashara kwenye kilimo"- Katibu Mkuu Mweli | Ministry of Agriculture
Watafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) wametakiwa kuhakikisha matokeo ya tafiti zao yanaifikia Jamii wakiwemo wawekezaji na kampuni za kibiashara ili matokeo hayo yatumike kibiashara na kutatua kero mbalimbali kwa jamii.Wito huo umetolewa leo Februali 20 na Katibu Mkuu wa Wizara...
www.kilimo.go.tz