Utata mkubwa kifo cha Dkt. Mkamilo wa TARI

Bunge la Wananchi

New Member
Jan 30, 2023
4
5
TARI_3.jpg
Dk. Mkamilo akizungumza wakati wa kukabidhi Ofisi baada ya kumaliza muda wake kama Mkurugenzi wa TARI hii ilikuwa Februari 20, 2024 baada ya kutoka kwenye tukio hilo akafariki tarehe 2.3.2024

Kifo cha Dk. Mkamilo aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TARI kimeacha simanzi na huzuni kubwa kwa wanataaluma wa masuala ya utafiti wa Kilimo ndani na nje ya Tanzania.

Kifo cha Dk. Mkamilo kimeacha maswali mengi sana kutokana na utata uliopo kwani Dk. Mkalimo hadi anastaafu alikuwa na afya njema na siku ya tarehe 20 Februari 2024 alikwenda kukabidhi Ofisi kwa Mkurugenzi mpya Dk. Thomas Bwana na baada ya tukio hilo akafariki dunia huku chanzo cha kifo chake hadi sasa kikiwa hakijulikani.

Sio Serikali, wala Wafanyakazi wa TARI wanaojua sababu ya Kifo cha Dk. Mkamilo, suala hili limeacha simanzi kubwa sana huku kukiwepo minong'ono mingi kuhusu kifo cha Dk. Mkamilo.

Wanaojua ukweli wa suala hili watuambie ili kuondoa sintofahamu kubwa iliyopo sasa.

 
Alikuwa na afya njema kivipi?. Ni ngumu kuthibitisha hali ya afya yake kwa kumuangalia tu.
 
Kifo kipo na hakina sababu.
Tuamini tu ametutoka kwa kuwa muda wake umeisha.
 
Inakuwaje mtu anakuwa unprepared kustaafu kiasi cha kupata mshtuko?
Huwa unawapata wale waadilifu ktk kazi. Wanajisahau kabisa wanaendelea na kazi bila kuchoka wanashtukia barua ya kustaafu hiyo hapo. Ninashindwa kwa vipi utumishi hawawashtui maana wanajulikana. Sio wakurugenzi tu ni aina ya wafanyakazi wanaofia kazini. Yeye na kazi, kazi na yeye. Bahatj mbaya huku kwetu hakuna uangalizi wa watu wa aina hii. Sio wengi ila hawaangaliwi zaidi. Hawa habari ya wizi nk sio upande wao. Hawaplan baada ya kustaafu itakuwaje zaidi ya pensheni. Barua ikifika hajui lenshen atalipwa lini. Ingesaidia sana mstaafu apate hundi yake siku ya kustaafu.
 
Back
Top Bottom