Usitumie "Reviews" kama kigezo cha kununua Bidhaa mtandaoni utajuta

Ibanda1

JF-Expert Member
Jul 18, 2015
716
1,109
Habari za majukumu wadau, naomba nizame kwenye maada moja kwa moja

Wiki iliyopita nikiwa kwenye harakati za kusaka tonge mara nikasikia mlio wa message WhatsApp kwa kuwa simu ilikuwa kimya kwa muda mrefu chap nikaitoa mfukoni nikafungua message nikakutana na namba mpya code +27 nilijua tu hii ni kwa madiba basi nikasoma ujumbe, Jamaa anakajitambulisha kisa akasema namba yangu imechaguliwa na online promotion company inataka inipe ajira ya ya muda mfupi ambayo nitakuwa nafanya kwa wakati wangu wa muda wa ziada ili kujiongezea kipato, uso ukajawa na tabasamu ile kimoyomoyo nikisemea "naijua hiyo" nikiwa bado naangalia simu jamaa akashusha text nyingine ya kuniomba nifungue link nikamkatalia kwani huwa sina utaratibu wa kufungua link kutoka kwa mtu nisiye mfahamu, zaidi nikamtaka aeleze hiyo ni kazi gani na wanajihusiha na kitu gani?

Jamaa akaanza kufunguka kwamba wao ni kampuni ya kufanya promotion mtandaoni kwa wauza bidhaa na watoa huduma mbalimbali zaidi wamejikita kwenye kufanya promotion kwenye website za hotels na restaurants hivyo kazi yangu itakuwa kuingia kwenye website hizo kupitia link itakayokuwa inatumwa then nitakuwa naweka ratings ya 5 stars na kuandika positive feedback na kwa kila review watakuwa wananilipa 5k, akanitumia sample na akaniomba nigoogle jina ya hiyo lodge then nikitoa comment ni screenshot kisha nimtumie kwa haikudhuru chochote nikafanya hivyo jamaa akaniomba number yangu chap muhamala kwenye tigo pesa ukasoma 5k. Akaniambia ataniunganisha na HR atanipa code then watanialika kwenye group la telegram kisha wataanza kunipa kazi.

Basi nikaunganishwa na HR anakaniomba details kama vile number ya simu na umri wangu, taarifa sahihi nilizompa ni namba ya simu tu baada ya siku moja nikaona wamenijoin kwenye hiyo group ila nimepewa limitations sitaweza kupost chochote hadi nifanye kazi 68 (68 reviews), hapo mimi kazi yangu nitakuwa nasubiri Admin awake link ya website then naenda naweka 5 stars ratings then naweka comment nzuri na screenshot namtumia huyo HR zikifika tano wananiwekea mzigo wangu (25k) mimi nikaona poa tu coz haichukui muda wangu kabisa, sasa baada ya kazi tatu nikiwa nasubiri kazi ya nne nikaona imekuja bila link wanasema ni salary increase task yaani hapa unapewa option nne kwamba kuna mtu wanamuita merchant unamtumia pesa then anakurudishia baada ya dakika 30 baada ya hapo dau lako litakuwa limepanda kwa kila kazi utakuwa unapewa 10k, yaani option A utanuma 40k anakurudishia 52k, option B unatuma 80k unarudishiwa 104k option C unatuma 140k unarudishiwa 180k, option D unatuma 200k unarudishiwa 260k hapo ndani vijana wanachagua option D na wachache sana C na B nikajismea enheee ndo yaleyaleee!

HR akanifuata inbox akaniuliza nimeelewa task number task 4, nikamwambia hapana hasi ndio akaja na hizo blabla nilizoeleza hapo juu nikamuuliza nini kitatokea nisipotekeleza hiyo task? Aksema itakuwa vigumu kwa finance department kunilipa coz nitakuwa nimevuruga utaratibu, nikamwambia nashukuru ila siwezi kulipa ili niongezewe dau basi naomba huu mchezo tuishie hapa, akasema basi haina shida wewe endelea na task number 5 na 6 ili ukamilishe row ya kwanza tukulipe, aiseee muda huo wale jamaa kwenye group wamechafukwa wanatuma screenshot jinsi wamelipa na wamerudishiwa hela na dau limepanda yani ni kutamba tu huko, basi nikamaliza kazi tano nikamwambia nishamaliza naomba mzigo wangu kweli baada ya dakika 10 wakaweka 25k nikaendelea kupiga kazi aisee baada ya kupiga nyingine tano akanifuata akaniambia saa hz hawataweza kulipa hadi nitume pesa kwa merchant, nikamwambia sina hiyo pesa aisee nikashangaa ghafla nimekula kufuli nikasema sipendi ujinga nikatoa pesa yangu alafu nikampasua sana yule Dada, kumbe wanahangaika kurudisha muhamala baada ya kuona nimewawahi akashusha mvua ya povu ila tukawa tumemalizana hivyo kibabe. Kuna jambo limenishangaza coz nilikuwa sifahamu kama hizo reviews zinanunuliwa na mbaya zaidi wengi tunazitumia kama njia ya kupima ubora kumbe ni biashara za watu.

Nimeshare na nyie yawezekana kuna watu wakaingia huu mkenge ama kama kuna mtu amewahi kukutana na jambo kama hili pia anaweza kutuoa uzoefu wake.

Screenshot_20240504_234746_Maps.jpg
Screenshot_20240505_000621_Maps.jpg
 
Hizo revews ni za biashara/makampuni halali au ni page fake zilizotengenezwa na hao matapeli?
 
yaani option A utanuma 40k anakurudishia 52k, option B unatuma 80k unarudishiwa 104k option C unatuma 140k unarudishiwa 180k, option D unatuma 200k unarudishiwa 260k
Dah,
Nahisi ulikuwa smart kukwepa huu mtego. Ungetuma pesa wangekukomba chap.

Halafu kumbe reviews ni scam, itafika wakati hazitakuwa na tija
 
Aisee yani jamaa wanakutia tamaa vibaya mno muda wote wanatuma screenshot za mihamala,
Mkuu achana na mambo ya reviews kumbe ni biashara za watu eti
 
Si mchezo, mfano kule booking..com kuna marobot kibao... Jichanganye uende kwenye hotel ambayo utakuja jutia pesa yako

Point: ndio review zisikuchanganye kwenye ununuzi wa bidhaa ama huduma
Ni kweli huko booking.com nimewahi kuingizwa chaka na hizo reviews ile nafika nakuta hiyo room mbovu balaa
 
Back
Top Bottom