Usijivune: Kassim Majaliwa, Prof Mark Mwandosya na marehemu Prof Idris Mtulia, Wakiwa ndani ya Mtumbwi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,493
54,900
maja.jpg

Picha hii ni ya mwaka 2010, Wa tatu kwa waliokaa kutoka nyuma ni Kassim Majaliwa ambaye wakati huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji. Majaliwa hakuwa hata mbunge wakati huo.

Nyuma ya Majaliwa ni Prof Mark Mwandosya ambaye wakati huo alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, asiye na Wizara Maalum. Na nyuma ya Mwandosya ni aliyekuwa Mbunge wa Rufiji, Prof Idris Mtulia (marehemu). Katika Uchaguzi Mkuu mwaka huo, Majaliwa alichaguliwa kuwa mbunge na baada ya hapo aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi, akishughulika zaidi na upande wa elimu.

=====

Picha hii ni ya mwaka 2010, Wa tatu kwa waliokaa kutoka nyuma ni Kassim Majaliwa ambaye wakati huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji. Majaliwa hakuwa hata mbunge wakati huo.

Nyuma ya Majaliwa ni Prof Mark Mwandosya ambaye wakati huo alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, asiye na Wizara Maalum. Na nyuma ya Mwandosya ni aliyekuwa Mbunge wa Rufiji, Prof Idris Mtulia (marehemu).

Katika Uchaguzi Mkuu mwaka huo, Majaliwa alichaguliwa kuwa mbunge na baada ya hapo aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi, akishughulika zaidi na upande wa elimu.

Miaka mitano iliyofuata Majaliwa akawa Waziri Mkuu. Ukiangalia picha hii unapata jawabu kuwa hakuna ambaye alikuwa anawaza kama Majaliwa ni Waziri Mkuu baada ya Mizengo Pinda.

Hapo Majaliwa alikuwa akionekana mwenye cheo kidogo tu, Mkuu wa Wilaya. Pichani anaonekana ni mtu mnyonge tu, mnyeneyekevu mbele ya wezake.

Majaliwa wa leo huwezi kumpandisha kwenye mtumbwi hivyo, maana ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika ofisi yake kuna kila aina ya usafiri bora ambao unaweza kumfikisha popote, tofauti na mtumbwi huo ambao unaona kuupanda ni kama vile kuhatarisha maisha.

Majaliwa ana ndege yake kama Waziri Mkuu, ana helikopta na magari. Majaliwa wa leo hawezi kuvuka Mto Rufiji kwa mtumbwi hivyo, helikopta itamvusha.

POKEA ELIMU HII

Mwenye kibali cha kuyafahamu maisha yanayofuata kwa kila binadamu ni Mungu tu. Mungu alijua Majaliwa ni Waziri Mkuu baada ya Pinda, ila watu wengine wote kwenye mtumbwi huo akiwemo nahodha na Majaliwa mwenyewe hakuna aliyeifahamu siri hiyo.

Picha hii inafundisha watu kuwa wanyenyekevu katika maisha yao. Unaweza kumdharau mmachinga anayekubembeleza kununua bidhaa zake lakini miaka inayofuata ndiyo akawa Rais.

Ukijiona umebarikiwa kwa maisha fulani usiongeze tambo, bali mshukuru Mungu na uwe mnyenyekevu. Unaweza kumdharau housegirl nyumbani kwako, baadaye akawa Rais mwanamke au mke wa Rais, na mkamwita First Lady kisha barabarani mkapanga foleni kwa kuzuiwa na traffic, maana First Lady anapita.

Si mnasema kupanga ni kuchagua? Basi mpangaji ni Mungu na yeye ndiye humchagua amtakaye. Anaweza kumchagua kumwinua mtu ambaye wewe unamchukia kupita kiasi, acha chuki. Anaweza kumchagua unayemdharau, hebu acha dharau. Anaweza kumchagua unayemwonea na kumnyanyasa kwa unyonge wake, tafadhali usionee wenzako.

Ishi maisha ambayo yatakufanya uwe huru leo na kesho. Tenda wema na kama huwezi basi usitende ubaya. Usipomtendea mtu ubaya utakuwa huru kila siku. Na utatabasamu kwa mafanikio ya kila mmoja. Ukiwa mwovu, kuna watu wakifanikiwa utaona wanaifanya dunia yako iwe chungu.,

===

Wakati Majaliwa akiwa DC Rufiji, alikua anaripoti kwa RC Pwani Magesa Mulongo na Waziri wa TAMISEMI Stephen Wassira. Leo wote wawili hawapo tena serikalini.

Majaliwa alipoteuliwa Naibu Waziri TAMISEMI alikua anaripoti kwa Kepteni George Mkuchika. Leo mzee Mkuchika ndiye anayeripoti kwa Majaliwa.

Maisha ni mzunguko. Ukifanikiwa usijae kiburi ukadhani ndio mwisho wa safari. Al-Bashir alikua na madaraka makubwa na pesa nyingi. Lakini leo ni mfungwa. Anakula, kulala na kuamka kwa amri. Hana tena hiyari ya maisha yake.

Na pia ukikosa leo usikate tamaa ukadhani Mungu amekuacha. Bado lipo tumaini. Anayekudharau kwa sababu ni 'Housegirl' kesho unaweza kuolewa na Rais ukawa First Lady na akakuheshimu.

Wana wa Israel walipowekwa mateka kule Babeli, Esta na mjomba wake Mordekai walikua watumwa. Esta akachukuliwa na Hegai kuwa kijakazi kwenye nyumba ya Mfalme.

Hegai alikua kama 'Afisa Utumishi' kwenye kasri la mfalme Ahasuero. Vijakazi wote wa mfalme waliripoti kwake akiwemo Esta. Lakini baadae Esta akawa Malkia, na Hegai akawa anaripoti kwa Esta. Life is circle.

Hakuna aliyejua kiongozi mwenye ulinzi mkubwa na fedha nyingi kama Gadafi siku moja angeweza kujificha kwenye mtaro wa maji taka kama mwizi wa kuku wa Gongo la Mboto.

Usijivune kwa kufanikiwa leo, na usivunjike moyo kwa kufeli leo. Winston Churchill aliwahi kusema "Success is not final, and failure is not fatal. It is the courage to continue that counts"
 
View attachment 694945
Picha hii ni ya mwaka 2010, Wa tatu kwa waliokaa kutoka nyuma ni Kassim Majaliwa ambaye wakati huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji. Majaliwa hakuwa hata mbunge wakati huo.

Nyuma ya Majaliwa ni Prof Mark Mwandosya ambaye wakati huo alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, asiye na Wizara Maalum. Na nyuma ya Mwandosya ni aliyekuwa Mbunge wa Rufiji, Prof Idris Mtulia (marehemu). Katika Uchaguzi Mkuu mwaka huo, Majaliwa alichaguliwa kuwa mbunge na baada ya hapo aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi, akishughulika zaidi na upande wa elimu.
Heri ya mwaka mpya.
 
Good to know!

All those are despots at the core!
 
Back
Top Bottom