Ushawahi kuingiwa na hofu na huzuni usiyojua inatokana na nini?

Mashaurijr

JF-Expert Member
Oct 8, 2016
716
1,151
Hali kama hii ya hofu inanitokea mara chache kabla hata sijapokea taarifa mbaya . Au jambo baya kutokea na sijui kwa nini sometimes inatokea alafu nisielewe kabisa shida nini na inapotokea naanza kuwaza ni tatizo gani linakuja namwomba Mungu Aniepushie.

Sasa leo nilitaka kutoka mida ya saa moja ila ghafla nikaingiwa na hofu hii ya ajabu yaani ni ajabu sana . Mwili unatetemeka najiskia kibaridi hivi na kukosa kabisa amani. Nimegairi kutoka nipo tu maskani mpaka mida hii hali bado inaendelea japo imepungua.

Pia naitumia kutabiri matokeo ya taarifa mbaya ninazopokea naweza kupokea taarifa za mgonjwa alafu niwe kawaida kabisa bila hofu wala nini ila nikiwa tu na hofu mgonjwa huyo kuna asilimia kubwa za kumpoteza kwa hiyo hata nafanyaga masihara kabisa mpaka watu wananishangaa wao wanapresha mimi nipo kawaida na nikiwahakikishia na inakuwa.
Yaani tatizo kubwa au sio tatizo nalipima kulingana na hofu ya ajabu

Kinachonitesa ni hii ya kabla ya tukio inatesa sana sijui naiondoaje maana inachosha na inawazisha sana. Naanza kuwaza sana ni baya gani linaenda kutokea . Hapo ndio shida ilipo hofu hii inanipa wakati mgumu sana

Wakuu huu ni ugonjwa au nini niisije nikawa nachukulia poa
 
Mara nyingi sana hutokea, na chasjabu mimi hutekea mara baada ya kua na furaha ambayo pia sijui imetokea wapi
 
Haikupita siku nilipewa kesi mbaya sana na walimwengu, ilinidhalilisha kiasi flani japo sio kivile kwa sababu Tanzania hii ni ngumu mtu kunijua kwa undani zaidi
 
Back
Top Bottom