Ushauri wa Bure kwa Wadudu-Msitumike Bila Manufaa

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
2,044
3,931
Habari za wakti huu;
Kwanza niweke wazi kwamba Mimi Nimekulia Arusha.
Ninafahamu Fursa na Changamoto zilizoko Katika Mkoa wa Arusha na Ninatambua tabia na Hulka za Vijana wa Arusha.Kimsingi katika Mikoa Yote Tanzania Ukiondoa Wamasai Vijana wa Arusha ndio Jamii Pekee ambayo imeweza kutengeneza Utambulisho wa Kipekee wa kujiita Wadudu ambao sasa naona wanasiasa wanaanza kutaka kuwatumia.Arusha ndio mkoa Pekee ambao Vijana wake wanaitwa Majina ya aina tofauti kama vile NYOKA,CHALII na sasa Wadudu/Mdudu.

Mara ya kwanza kuwaona vijana hawa wa Arusha ambao kimsingi ni wapambanaji kama wapambanaji wengine niliwaona kama vijana ambao ama walikuwa wamepoteza uelekeo au walikuwa wanajitafuta.Hii ni kutokana na namna yao ya kuwakilisha ujumbe wao katika Jamii na PIA namna yao ya mavazi uzungumzaji na hata mitazamo yao mbalimbali.

Leo Nimewaona katika Maonesha ya Wafanyakazi yaani Mei Mosi,Wakiwa Pamoja na Madereva wa Boda Boda.Baada ya kutazama kwa makini wajihi wao Nikasema Hawa vijana inabidi sasa niwape ushauri wa Chap kabla hawajatumika na kutupwa.

Wanasiasa kwa SILKA huwa wanapenda Kutumia Watu wakati wakiwa na maslahi nao na kisha kuachana nao wakati wanapokuwa hawana Maslahi.Ni jambo la kawaida katika SIASA ila kwa ambaye SIO Mwanasiasa linaumiza sana.Na hilo ndilo limenifanya niwatake Wadudu sasa Waamue Kujipa IDENTITY na KUTAMBULIKA rasmi kama Kikundi cha Sana.

Rafiki zangu wadudu.Sasa Ni wakati wa Nyinyi Kwenda BASATA na Kujisajili kama Jumuia ya Wasanii na Mpeani Vitambulisho.Mjiite Kabisa Wadudu na Msajili kwa JINA hilo na muwe na Vitambulisho vya Uanachama.

Nawashauri hivi ili Msijegeuzwa kama Wamachinga ambao ukiakribia uchaguzi huwa Magari yanaondolewa Barabarani ili wafanye Biashara na Uchaguzi ukiisha Wanafukuzwa Barabarani na Rungu na Migambo na kufilisiwa.

Narudia TENA kusisitiza WADUDU wa CHUGA Kwa kuwa Tayri serikali imeonesha kutambua UWEPO wenu Basi ni wakti sasa wa ninyi kujiunda Kitaasisi.

Nawatakieni Kila la Heri
 
Hawa watumika tu kipindi hiki cha uchaguzi kama wanavyotumika WALIMU NA POLISI CCM
Exactly,Niemona Hilo Ndio maana nimetoa Ushauri kwao Kwamba SASA walazimishe Kutambulika kama Kikundi Maalum Cha kijamii chenye Maslahi Sahihi
 
Nilikuwa siwajui hao watu ila leo ndio nimewaona. Hongera RC Makonda kwa kuwatambulisha.

Na kingine acha wivu kijana...kama angewatumia Mbowe usingepiga kelele
 
Habari za wakti huu;
Kwanza niweke wazi kwamba Mimi Nimekulia Arusha.
Ninafahamu Fursa na Changamoto zilizoko Katika Mkoa wa Arusha na Ninatambua tabia na Hulka za Vijana wa Arusha.Kimsingi katika Mikoa Yote Tanzania Ukiondoa Wamasai Vijana wa Arusha ndio Jamii Pekee ambayo imeweza kutengeneza Utambulisho wa Kipekee wa kujiita Wadudu ambao sasa naona wanasiasa wanaanza kutaka kuwatumia.Arusha ndio mkoa Pekee ambao Vijana wake wanaitwa Majina ya aina tofauti kama vile NYOKA,CHALII na sasa Wadudu/Mdudu.

Mara ya kwanza kuwaona vijana hawa wa Arusha ambao kimsingi ni wapambanaji kama wapambanaji wengine niliwaona kama vijana ambao ama walikuwa wamepoteza uelekeo au walikuwa wanajitafuta.Hii ni kutokana na namna yao ya kuwakilisha ujumbe wao katika Jamii na PIA namna yao ya mavazi uzungumzaji na hata mitazamo yao mbalimbali.

Leo Nimewaona katika Maonesha ya Wafanyakazi yaani Mei Mosi,Wakiwa Pamoja na Madereva wa Boda Boda.Baada ya kutazama kwa makini wajihi wao Nikasema Hawa vijana inabidi sasa niwape ushauri wa Chap kabla hawajatumika na kutupwa.

Wanasiasa kwa SILKA huwa wanapenda Kutumia Watu wakati wakiwa na maslahi nao na kisha kuachana nao wakati wanapokuwa hawana Maslahi.Ni jambo la kawaida katika SIASA ila kwa ambaye SIO Mwanasiasa linaumiza sana.Na hilo ndilo limenifanya niwatake Wadudu sasa Waamue Kujipa IDENTITY na KUTAMBULIKA rasmi kama Kikundi cha Sana.

Rafiki zangu wadudu.Sasa Ni wakati wa Nyinyi Kwenda BASATA na Kujisajili kama Jumuia ya Wasanii na Mpeani Vitambulisho.Mjiite Kabisa Wadudu na Msajili kwa JINA hilo na muwe na Vitambulisho vya Uanachama.

Nawashauri hivi ili Msijegeuzwa kama Wamachinga ambao ukiakribia uchaguzi huwa Magari yanaondolewa Barabarani ili wafanye Biashara na Uchaguzi ukiisha Wanafukuzwa Barabarani na Rungu na Migambo na kufilisiwa.

Narudia TENA kusisitiza WADUDU wa CHUGA Kwa kuwa Tayri serikali imeonesha kutambua UWEPO wenu Basi ni wakti sasa wa ninyi kujiunda Kitaasisi.

Nawatakieni Kila la Heri
wazo la kipumbavu zaidi tangu mwaka uanze.

sasa unataka wakajisajili kuwa wao ni wasanii,then what? wakishajisajili ndio hawataweza kutumika kwa manufaa ya wanasiasa?

siku zote mlikuwa wapi mpaka Leo mdandie gari kwa mbele?

pumbavu
.
 
Mkuu,Nimekujiabu kwa sababu nina mudi nzuri ila ulivomalizia na neno Pumbavu Umenikosea sana.Kwanza kabisa Soma uelewe Msingi wa Hoja na Ushauri wangu kisha uchangie katika Msingi wa Hoja.Sidhani kama kuna ambacho nimekisema ambacho kinastahili wewe kusema Pumbavu.

All in All ni ushauri tu wanaweza wakauchukua au wakauacha.Kila la heri
 
Nilikuwa siwajui hao watu ila leo ndio nimewaona. Hongera RC Makonda kwa kuwatambulisha.

Na kingine acha wivu kijana...kama angewatumia Mbowe usingepiga kelele
Hivi unaelewa Msingi wa Hoja?Any way Ndivyo Watanzania Tulivyo.Ni vigumu Sana Kulitazama Suala Kwa Objectivity.Sio Kosa lako...
 
Ushauri wa kipumbavu mno. Vijana wa Arusha ni makini na hawana huo upuuzi wa kikundi cha wahuni wanaojiita wadudu. Vijana wa Arusha kama Seth Benjamin aliyefariki kwenye matembezi ya Azimio la Arusha ndo wanaohitajika na sio huo uchafu unaopromotiwa kwa jina la Wadudu. Ungewashauri hata wajiunge VETA kupata ujuzi kwasababu kama ni sanaa hakuna sanaa yoyote wanayofanya zaidi ya kujifanya wendawazimu.
 
Sasa hao wadudu wanakua wasanii wa kitu gani?au mamodel wakuvaa aina hiyo ya mavazi.
 
Back
Top Bottom