Ushauri wa bure kwa abiria wa Bodaboda; Usipande bodaboda kama...

Kama unatumia Bodaboda hasa maeneo ya MJINI pitia hapa!

1. Usipande bodaboda isiyokuwa na vioo vya pembeni (saiti mira) – side mirror
Pikipiki ambayo haina vioo vya pembeni, dereva haoni gari linalokuja nyuma au hata akitaka kupinda, haoni nyuma hivyo uwezekano wa kugongwa ni mkubwa sana; ni suala la muda tu wala haijalishi uzoefu. Kama unajali uhai wako na familia yako, zingatia sana hii

2. Usipande pikipiki ambayo dereva hajavaa Kofia/helmet
Ile kofia inakioo kinachozuia wadudu wanaoingia machoni na hata vumbi anapopishana na magari makubwa; Fikiria boda anakimbia KMS 70, halafu wadudu wamuingie machoni; ushukuru sana Mungu kama hutaishia kwenye mtaro au hata kugongwa...

Ushauri: Vile vioo vya pembeni vyote viwili havizidi shs 10,000 hivyo kama una bodaboda wako, unaweza kumnunulia/kumkopesha. Kofia ngumu ya kawaida ni kwenye shs 20,000=

Mwisho: Ukiona pikipiki ipo ovyo ovyo (haina sifa), ujue na muendeshaji yuko hivyo hivyo, uamuzi ni wako!

-
Usipande bodaboda main road( highway).
Bodaboda ni usafiri convenient kwenye barabara za kuingia ndani,mitaani,hizi za vumbi zisizokuwa na magari mengi

Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app
 
15. usipande bodaboda ya dereva aliyenyoa kiduku
Katika vitu ambavyo nakiwa makini navyo ni pamoja na.muonekano wa Bodaboda. Naangalia kama amevaaje, ana viatu au yebo? Umri wake upoje then ndio nakuja ubora au muonekano wa pikipiki yake ila.Mara nyingi huwa napanda Pikipiki za watu wazima/wazee.
 
Katika vitu ambavyo nakiwa makini navyo ni pamoja na.muonekano wa Bodaboda. Naangalia kama amevaaje, ana viatu au yebo? Umri wake upoje then ndio nakuja ubora au muonekano wa pikipiki yake ila.Mara nyingi huwa napanda Pikipiki za watu wazima/wazee.
ni kweli, bodaboda za watu wazima/wazee au za kijana ambae unamfahamu ana mke na watoto ambao wanamtegemea ndo za kupanda.
 
Back
Top Bottom