Ushauri: Mwanamke niliezaa naye watoto 2, kanikata, nikaomba msamaha, kakataa, sasa ananitaka tena

Ndakilawe

JF-Expert Member
Jul 6, 2011
4,815
2,814
Habarini wana MMU

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu! Naomba ushauri wadau, hili jambo linanitatiza sana.

Mimi ni baba wa watoto 3. Watoto wawili nilizaa na mama mmoja, na huyo mwingine mama mmoja.

Ishu ipo hivi, wakati nilipomaliza chuo, nilienda home likizo ndogo kabla ya kurejea DSM kuja kusaka ajira, pale home wadogo zangu wa kike walikuwa wamemaliza kidato cha nne, kuna rafiki yao alikuwa pale home kabla kabla ya kurejea kwao. Yule binti nikamweka sawa (nikamtongoza). Akakubali, but hakunipa tunda. Niliporudi DSM, baada ya kama miezi 8 akaja dsm tukatengeneza mtoto, binti mzuri tu, nipo naye (mtoto) mpaka sasa. Mama yake hana tatizo, na alishaolewa, but akitaka kumuona mtoto, namruhusu.

Huyu niliyezaa naye watoto wawili:

Niombe msamaha kwanza kwa rafiki yangu. Alikuwa girlfriend wa rafiki yangu wakati huo tukiwa Advance secondary, tulikuwa tumepanga huko Tegeta. Baada ya kumaliza, mimi nikarudi Ubungo kwa Brother (Mola amrehemu).
Huyu binti wakati huo anasoma chuo cha uhazili (hapa jijini). Nikiwa ubungo, huyu binti (mama watoto wangu 2) akawa anakuja ubungo kuwasiliana na yule jamaa yake (rafiki yangu) pale napokaa, pia nawaachia chumba wanatumia. Pia yule mshikaji wangu hakuwa na simu, ivo mawasiliano yalikuwa yanapitia kwangu ndio namfikishia huyo MSHIKAJI.

Wakagombana, na binti akawa ananitumia msg kumuambia mshikaji kuwa hamtaki, na akanileta picha zake nimrudishie coz mapenzi yameisha.

Baada ya kitambo kidogo kupita, yule binti (mama watoto wangu wawili) akaanza kunitumia msg za kunitaka kimapenzi. Wakati huo sikua na mtu, girlfriend wangu alirudi kwao huko Mwanza, kwavile nlikuwa na ukame, nikapiga (2005) kama mara 2 nakumbuka. Baada ya hapo hatukuonana tena mpaka nimemaliza chuo 2008.

Kuna siku nilikuwa Landmark hotel, nikiwa chuo mwaka wa mwisho wakati wa sikukuu ya Mtakatifu Valentino, nilikuwa na msukuma wangu, na yeye alikuwa na jamaa yake( Huyu jamaa yake ni mwingine, sio yule, ila hata huyu naye pia ni rafiki yangu ila sio sana kama yule mshikaji wa awali).

Msukuma wangu akarudi Mwanza, baada ya kumaliza chuo,pia akapata kazi huko huko kanda ya ziwa. Siku moja nikakutana na huyu binti (mama watoto wangu wawili) maeneo ya riverside, nikamuuliza vp, upo na falani, akanimabia hapana. Ila nilishasikia kuwa wameachana.Tukapeana namba za simu pale. Of-course, nikiwa na kiu namtafuta nakula,

Mungu ni shahidi kama nasingizia (Hata watoto wangu awadhuru) ktk hili;

Nililala naye mare 4 kwa kutumia kinga (condom), siku moja alikuja anataka mambo, nikiwa nimeshavaa kingi ipo ndani ya papuchi* akaniambia namuuza na mpira, nivue, kweli nikavua (uongo mbaya siku hiyo pia nlikuwa nimekunywa kasichana/nyagi ndogo) nikampe heavy duty exercise , baada ya hapo kila mtu akaenda kwake.

Baada ya siku 3/5 kupita akaniambia ana mimba yangu, nikamuambia mimi sipo tayari kuwa na mtoto, tufanye dhambi tu (Mungu anisamehe), binti akakaata kuwa hajawahi kutoa mimba hivyo hawezi kufanya hivyo( na pia hana haja ya mimi kulea mtoto, wakati huo yeye ni mwajiriwa serikalini pia ni aged kuliko mm kwa miaka 3, na mm ndio nimemaliza chuo bado sina kazi), nikaenda kwa wale X wake kuwauliaza, yule wa mwisho akaniambia yeye mwenyewe alishamtoa si chini ya 3, nikajua tu alipanga kuzaa na mimi. Kweli wakuu, baada ya miezi 9, mtoto akazaliwa.

Nikamuona, nikafurahi kweli! (Kumbuka yule binti aliyekuwa anasoma na mdogo wangu na yeye alijifungua mwaka uliofuata, na nilitaka kumuoa huyo, coz tulipishana kama miaka 6).

Hapo vikaanza vitimbi kwa ndugu zake, wakaanza kulazimisha nimuoa, kaka yake akaniambia nisiwe na shaka juu ya maisha, atanipa hela za kuanzia maisha kama nitakubali kumuoa mdogo wake na ahadi nyingine kibao. Wakaanza kuforce wazazi wajuane( kwa kifupi nlikuwa naozeshwa kwangu). Mimi nikawaambia tu, haina haraka, nikiwa tayari nitawajulisha, pia mm sina ugomvi na binti yao, maana mtoto namhudumia kama kawaida. Baada ya mtoto kuzali mwezi uliofuata nikapa kibarua hapo UDSM.

Ukweli ni kuwa nilikuwa na matarajio ya kumuoa yule binti mwingine na sio huyu, na ni kwasababu tu (nilimtoa bikra), pia niliharibu mahusiano yake na wazazi wake ( Ila nilimsomesha certificate ya childhood Education).

Miaka ikaenda, kazi ikaisha UDSM, hapa nikawa naishi na huyu binti ( mama mtoto mmoja). Kile kidogo nilichotoaka nacho pale UDSM, nikafungua Ki-grocery, pia kujilipia ada ya Masters (MPA). Nikapata tukazi twa muda taasisi moja, tukawa tunaenda mikoani, tunakaa siku 60/21/72 inategemea. Kumbe mama mtoto mmoja akashindwa kuvumilia, akawa anamegwa kisela na watu wa Bongo Movie( na movie akacheza pia, sizitaji hapa), nikaambia! Sikuweza kuvumilia baada ya ushahidi kukamilika, tukaachana.

Nikiwa katika kujipanga upya (hapa sina kazi kwenye ile taasisi yaliingia majungu, kazi ikafa)

Mama watoto wawili (WAKATI HUO ANA MTOTO MMOJA) aliposikia hivyo, akaniambia basi nimuoa, au niishi naye atanipa kila kitu, mpaka nipate kazi, nikakaata, but nikawa nammega. Wakati huo nika naishi kwa misaada ya washikaji wenye kazi.

Baadaya ya muda, nikawa nimenogewa na mama wawili, niaanza kumpeleka nguo anifulie, nakula full time. Kidogo kidogo nikawa nalala huko hata mwezi. Nikawa baba kamili sasa, Mungu si Athuman, nikapata kazi ya kufundisha chuo fulani hapa mjini part time,, hale ya mboga ikawa hainipigi chenga.

Riwaya (simulizi ya kweli) inaanzia hapa:
Pale nyumbani kulikuwa na mabinti wawili, mmoja msaidizi wa kazi za nyumbani, mwingine ndugu yake mama watoto wawili.

Nilikuwa na mazoea sana na binti wa pili, ila sikuwahi kumtongoza wala kumtaka, japo yeye alipenda sana kupiga story za kikubwa nikiwa nyumbani (WAKATI HUO MAMA WATOTO WAWILI YUPO KAZINI). Nadhani yeye alitaka nimgegede, coz aliwahi kunishika (ikulu kuu) tukiwa kwenye corrido akakimbilia chumbani kwao, mimi nikaenda zangu bafuni kuoga.

Huyu binti wa pili (msaidizi wa kazi za ndani), ndiye nlikuwa namtaka, nikaanza kumsarandia. Tunatumiana msg kwa siri kubwa sana. Pia nikimhimiza afute msg mara baada ya kusoma ujumbe wangu (lakini cjawahi kumla). Siku moja kaacha msg chumbani,kumbe yule binti wa pili alikuwa chumbani, akasoma msg nilizomtumia na zile alizonitumia. Nikawa natumiwa msg, kumbe ni yule binti wa kwanza.

Akaja kumwambia mama watoto wawili (wakati huo ndio ana mimba ya mtoto wa pili (very handsome kid), nadhani utanielewa kwann nilitaka kula msaidizi wa kazi za ndani). Wakapiga simu wakiwa wote wakaweka loud speaker, wakamlizimisha binti aongee. Baada ya kustukia mchezo, nikageuza maneno pale, but haikusaidia kitu chochote. Mama akawa mkali sana, ila nikamueleza ukweli kuwa sijatembea naye, nilikuwa kwenye process, anisamehe. Mungu mkubwa, nilikuwa badi nyumba yangu nailipia kodi, nilipoona mambo yanakuwa magumu, nirudi kwangu.

Nikamwomba msamaha, nirudi tuendelee na maisha (wakati huu nilikuwa na furaha kwa sababu alinizalia mtoto wa kiume). Nikampa muda wa mwezi mmoja, wale mabinti wote waondoke, maana sio ndugu zangu wala ndugu zake. Ili maisha yaanze upya, na nikwamwambia nitatafuta house maid mwingine. Akanijibu, ni bora kuishi na wale mabinti kuliko kuishi na mm. Nikamtuma mama yangu mzazi akaongee naye, akakataa katukatu.

Maisha yameenda, Mungu si athumani , nikapata kazi nzuri tu (Meneja), nikanunua kagari, na kasehemu ka kujenga. Hapo movie ikaanza upya.

Akaanza kunisumbua, baba watoto wangu rudi tuwalee watoto. Mwaka na nusu ulishapita, tayari ni msichana nipo naye. Ishu ikaenda tena kwa wazazi, mimi nikawahadithia mkanda mzima ulivyo. Wakaduwaa, na sikuficha kitu.

Upande wake wakesema gharama za watoto nani atatoa, nikamuuliza anataka sh ngapi kwa mwezi, akasema LAKI MOJA. Nikaanza kutoa kuanzia ile siku mtoto alipozaliwa mpaka leo. Na ada ya mtoto wa kwanza na house girl namlipa. Ni kwasabu nawapenda wanangu.

Kila siku usumbufu, mara leo ameota tuna do, mara tumehamia kwetu. Mara ataniambia naomba mifuko 50 ya cement.. Kero chungu nzima. Mimi msimamo wangu ni kuwalea watoto na kuwapa elimu kwa kadiri ya uwezo wangu, ila mama yao sina mpango naye. Ni kwasabu alinidharau nilipokuwa sina kitu, akanifukuza home, hata baada ya kuomba msamaha akanikatilia.

Wadua msaada wenu, nifanyeje , maana nataka mwaka kesho nimuoe huyu binti niliyenae, pia kero za mama wawili sizitaki, na pia hataki kunipa watoto.

Riwaya ni ndefu, nimefupisha, kuna vitimbi vingi nimafanyiwa na mama wawili (Sijasema hapo)
 
daah nmeishia kati kat maana hata sielewi kwa kwel? labda nikushaur from heading tu
 
Sijamaliza kuisoma ila Jamaa wewe mwaribifu huna hata hofu ya maradhi.


Nitashauri nikirudi baada ya kumalizia kuisoma
 
  • Thanks
Reactions: amu
Umevuna ulichokipanda na maji yameshamwagika hayazoleki la msingi kua na msimamo thabiti
 
dihitajimeni lai kachomeni


Anuk intibak ahc oznawm ahsilazmema ufalah aukuhcmaka ototm ajaka anet ahsilazmaka enignewm ototaw iliwaw amam iliwaw atelaka odoyn akak atapaka enignewm won amam iliwaw atelijana
 
Sijamaliza kuisoma ila Jamaa wewe mwaribifu huna hata hofu ya maradhi.


Nitashauri nikirudi baada ya kumalizia kuisoma


Huyo dogo ni mjasiriamali wa kutisha. Nina hakika hata huyu anayetaka kumuoa hatamweza.

Bora angerudi kwa mama watoto ili waendelee kucheza movies kwani na huyo mama ni mtata!
 
Huyo dogo ni mjasiriamali wa kutisha. Nina hakika hata huyu anayetaka kumuoa hatamweza.

Bora angerudi kwa mama watoto ili waendelee kucheza movies kwani na huyo mama ni mtata!


Nimejikuta nacheka kwa nguvu na majibu haya
 
Anuk intibak ahc oznawm ahsilazmema ufalah aukuhcmaka ototm ajaka anet ahsilazmaka enignewm ototaw iliwaw amam iliwaw atelaka odoyn akak atapaka enignewm won amam iliwaw atelijana

eilabukma ehsilazma nate ut...!!
 
Nimejikuta nacheka kwa nguvu na majibu haya

Unadhani utani? Kuna mambo ukiyasikia kama mwanamume unaanza kutetemeka. Siwezi kupata picha bibi aniweke kwenye kikaango kwa sababu ya kukimbizana na beki tatu...


Nahisi nausea!
 
Back
Top Bottom