USHAURI: Jiajiri kutokana na taaluma yako badala ya kulalamika ajira hamna

Wadiz

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
5,535
11,398
Tutafute pesa Kwa maarifa yetu.
👇👇👇

Badala ya kujificha na kulalamika kuhusu ajira fungueni centers/madarasa/ ofisi Mikoani, Wilayani na hasa mikoa yenye taasisi za elimu ya juu ama vyuo vikuu, kuna fursa kubwa sana sana.

Tuokoe taifa.

Ni hayo tu.
 
Unajipinda na maliterature weeeeeee hadi unakoma halafu malipo ni ya kibaba...
Wa tz huwa hawaheshimu utaalamu wa watu kabisa. Mtu unamuongoza kuanzia proposal nzima, data collection , analysis hadi reporting anataka akupatie laki kazi yote...
Kwakweli hapana
 
Unajipinda na maliterature weeeeeee hadi unakoma halafu malipo ni ya kibaba...
Wa tz huwa hawaheshimu utaalamu wa kabisa. Mtu unamuongoza kuanzia proposal nzima, data collection analysis hadi reporting anataka akupatie laki kazi yote...
Kwakweli hapana
Una bargain nae mwanzo tu, proposal inapesa yake na Report writing Ina pesa yake, data screening na processing ina pesa yake. You need to know the value of ur work, usikata tamaa inategemea ulipo, inalipa I tell you, watu wengi ni weupe sana kichwani kwenye anga hizo.
 
Me proposal tu ni milion moja hutaki bora niache
 
Unajipinda na maliterature weeeeeee hadi unakoma halafu malipo ni ya kibaba...
Wa tz huwa hawaheshimu utaalamu wa watu kabisa. Mtu unamuongoza kuanzia proposal nzima, data collection , analysis hadi reporting anataka akupatie laki kazi yote...
Kwakweli hapana
Hiyo proposal, analysis na reporting, inaleta matunda gani mwishowe? Degree na cheti? Ai kuna kingine?

Miki isingekuwa kutafuta title na kaheshima flani kwemye jamii, nisingehangaika na degree..., ningefanya biashara na kujenga majumba ya kupangisha from tje beginning, nimepoteza miaka mingi sana shule.., ila mwisho wa siku, uchawi wote kumbe upo kwenye ‘Business’ na ‘Real estate’. Zunguka kote, ila uchawi wote upo hapo.
 
Siasa ina kataa reports zenye ukweli ndugu yangu. Utatengeneza pesa wapi sasa.

Ila kiukweli sisi tunaweza kuo-organize vitu na kuviweka pamoja kwa ustadi mkubwa. Ni bora tukajikita kwenye fursa mbalimbali ambazo zinasumbua jamii.
 
Ushauri mzuri sana huu. Watu tumesoma lakini elimu yetu hautupi pesa kabisa. Tatizo wabongo wahatoi pesa.
 
Mimi nimesoma Statistics lakini ninapopatia hela ni kwenye masuala ya tax. Nimeshaacha hayo masuala kabisa. Lakini nilichogundua wabongo wengi hawathamini utaalamu wa mtu kabisa.
Usikate tamaa mwamba ila sio mbaya Kwa huo mchepuko unalipa sana
 
Unabei unaifanya yote hadi report na manuscripts au just proposal ipite tu? Wewe ni mnoma sana
Proposal tu ila ni hadi ipite ...hata kwenye reporting lazima nirudi kwenye kuongeza literature kulingana na kile nitakachopata filed ili connection iwepo kwenye process nzima ya research....
Na kila stage ina bei yake
 
Back
Top Bottom