Karungikana
JF-Expert Member
- Jan 8, 2017
- 852
- 795
Kuna unyanyasaji nilioushuhudia ubalozi wa Marekani nilipoenda kushughulikia visa.
Kwanza pale getini, unaambiwa unaacha kila kitu huingii na chochote! Ila cha kushangaza, hawajaweka hata sehemu ya kuhifadhi mkoba au simu. Sasa sijui wanategemea ukienda huko usiende na pochi? Na je simu unamwachia nani?
Zamani wakati visa zinashughulikiwa ubalozi wa Uingereza, kulikuwa na lockers nje unaweka simu yako na kupewa kikaratasi. Sasa hawa binafsi sijawaelewa.
La pili; Ukishaingia ndani ya compund, nje ya ofisi zao, mnapanga foleni hapo nje mmesimama, hakuna hata benchi la kukaa! Iwe mvua liwe jua! Nikajiuliza je, na wenye ulemavu inakuwaje? Wanashindwa nini kuweka shed fulani na benchi angalau watu wakae?
Kutafuta visa ya Marekani ni kama kutafuta ruhusa ya kwenda mbinguni, wakati wao, wanaweza hata kupata visa airport! WHY?
Naamini wakiambiwa wanaweza kujirekebisha. Hakuna sababu ya kutunyanya kiasi hicho!