Unaona nini kila unapoutizama mwezi (moon)?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
16,375
24,738
Salaam, Shalom!!

Nipo hapa Mahali tulivu, nimerudi kuspend muda kidogo kuangalia mwezi juu angani, hii imekuwa Moja ya starehe yangu Kwa muda sasa.

Hali ya hewa ni tulivu, hakuna wingu angani, mwezi wote mzima unaonekana vizuri kabisa,

Kuna kitu nimekuwa nakiona tangu utoto, maana TABIA na mazoea ya kutizama mwezi sijaanza Leo,

Kitu kile kile nilichokuwa nakiona tangu zamani ninapoutizama mwezi Ukiwa full bila kuzibwa na chochote ndicho nakiona hivi sasa.

Ninamwona mtu, na mtu huyo anaonekana sura yake, imeujaza mwezi wote, na mtu huyo anaangalia chini huku sisi tulipo,

Siongelei macho ya Rohoni, la, naongelea macho haya ya Damu na nyama,

Ninamwona mtu, ninaona sura ya mtu, mtu huyo ni Mwanaume, hajatabasamu Wala kukasirika, Yeye mara zote Huwa anaangalia huku tulipo WANADAMU na kuangalia kwake, kunaambatana na Nuru kuu inayoangazia Dunia nzima bila kuchoka,

Mtu huyo Si Mzee, pia Si mtoto, kwa kukadiria, ni umri wa miaka ipatayo 30-40 hivi, Kila mara nipatapo wasaa huu adimu, hutoka kumuangalia mtu huyo, ingawa Yeye hajawahi kuniangalia direct, Huwa Yuko busy kuangalia anachokiangalia duniani na Nuru kuu ikiangaza itokayo katika uso wake, natamani siku moja ageuke na kuniangalia pia Mimi ambaye, Kwa muda sasa nimekuwa nikipoteza muda mrefu kumuangalia.

SWALI: Huwa unaona nini unapoangalia full moon (mwezi)?

Karibu🙏
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom