Unadhani ni jambo gani ambalo Watu wengi hawalifahamu kuhusu kupata Mtoto/Watoto?

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,513
9,309
Waswahili wanasema Mtu akipata Mtoto kuna namna hujikuta akibadilika na kugundua baadhi ya Mambo ambayo hapo awali hakuwahi kuyajua wala kuambiwa na waliomtangulia kwenye Malezi

Mtu mmoja aliniambia ukipata Mtoto/Watoto Maisha yako yanakuwa na Hofu mara kwa mara ukiwaza kama Ukifa mapema Maisha ya Wanao yatakuaje

Namna yako ya kufikiri mambo pia hubadilika na unajikuta Maamuzi mengi unayoyafanya lazima uwafikirie Watoto wako kwanza

Kwako ni jambo gani umeligundua baada ya Kupata Mtoto??
 
Tangu niwe mama, nimekuwa na hisia sana juu ya huzuni za watoto(ata kama sio mtoto wangu) nikiona mtoto anafanyiwa vitendo vibaya nalia mno, mpka tumbo linabana. Uchungu nilio nao kwa watoto umevuka mipaka.
Hongera kuwa sirias na uchungu wa watoto kuliko kuwa bize kusaka chapaa 24/7 na kuwaachia malezi ya Watoto housemaids wasio na uchungu hata chembe ya Mtoto/Watoto.
 
Kumpa mtoto/wototo muda wako na attention yako. Sio kwamba sikuwa nafanya,ila tu sikuwahi kufanya kwa kubwa huu wa sasa. Yaani kuna namna unatengeneza muunganiko Kati yenu kiasi kwamba asipokuona siku moja ni mitihani kwa mama yake.
Tujitahidi kuwapa watoto wetu muda wetu,tuwasikilize shida zao,tunazoweza kuzitatua tuzitatue,zilizo ndani ya uwezo wao tuwafundishe namna ya kuzikabili. Dunia inaangamia kwasababu wazazi tumepoteza nafasi zetu kwa kuzigawa kwenye majukumu na marafiki,madada wa kazi,muda wa kulea familia unakuwa mdogo sana kiasi cha watoto wengi kutopea kwenye tabia na mienendo hatalishi.

Tusiuachie ulimwengu utulelee watoto(uchafu mwingi unachangiwa na malezi mabovu,pesa isitusahaulishe jukumu muhimu la uwepo wetu kwao)
 
Waswahili wanasema Mtu akipata Mtoto kuna namna hujikuta akibadilika na kugundua baadhi ya Mambo ambayo hapo awali hakuwahi kuyajua wala kuambiwa na waliomtangulia kwenye Malezi

Mtu mmoja aliniambia ukipata Mtoto/Watoto Maisha yako yanakuwa na Hofu mara kwa mara ukiwaza kama Ukifa mapema Maisha ya Wanao yatakuaje

Namna yako ya kufikiri mambo pia hubadilika na unajikuta Maamuzi mengi unayoyafanya lazima uwafikirie Watoto wako kwanza

Kwako ni jambo gani umeligundua baada ya Kupata Mtoto??
Mada yako nzuri sana dada
 
Hongera kuwa sirias na uchungu wa watoto kuliko kuwa bize kusaka chapaa 24/7 na kuwaachia malezi ya Watoto housemaids wasio na uchungu hata chembe ya Mtoto/Watoto.
Serious?? Kwamba sisi tunaopambana kutafuta chapaa hatuko serious na watoto? Try to think twice, unavyomuachia housemaid mtoto doesn't mean humtaki ila your just out chasing what will make your child proud
 
Watu wengi wanapenda kuzaa watoto lakini wanasahau malezi kwa watoto walio wazaa.
Hii kitu hua inanisikitisha sana.
 
Back
Top Bottom