Uliza chochote kuhusu kujiunga Chuo Kikuu Huria Tanzania

dindilichuma

JF-Expert Member
Dec 19, 2015
1,662
2,541
Udahili umeanza, Chuo Kikuu Huria Tanzania na vyuo vingine hapa nchini.

Tuna chuo kimoja hapa nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla kinachotoa elimu wazi na Masafa(Open and distance learning)

Serikali ilianzisha chuo hiki kwa sheria ya bunge namba 17 ya mwaka 1992. Hii ilikua kuwapa fursa wafanyakazi na watu wenye majukumu yanayowafanya washindwe kwenda conventional university, hivyo kujikuta mahitaji yao ya kujiendeleza kielimu yakishindwa kufikiwa.

Kwa mwaka huu wa masomo udahili utakua ni bure.
Ingia tovuti ya chuo www.out.ac.tz na ufanye online application. Unahitaji kuwa na soft copy ya vyeti na picha(passport size moja).

Kwa tuliosoma na kufanikiwa tujitahidi wenzetu pia ambao wanauhitaji, kuwatangazia waweze kuitumia fursa hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nna 2.8 diploma vipi nawaza kujiunga au altenative yakufika huko vp
GPA inayotakiwa kwa mujibu wa wasimamizi wa Vyuo vikuu (TCU)kwa mtu anaepaswa kudahiliwa Kutoka Diploma kujiunga na shahada ya kwanza (Bachelor degree) anapaswa kuwa na GPA ya kuanzia 3.0 zamani ilikua 2.7 lakini kuanzia mwaka wa masomo uliopita imewekwa GPA ya 3.0.

Alternative unaweza kufanya diploma nyingine upate GPA stahiki, au unaweza kufanya mtihani wa kidato cha sita na kupata sifa stahiki au unaweza kufanya mtihani wa RPL unaotolewa na TCU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heee mbona mnahangaika sana kutafuta wanafunzi
Kutoa elimu kwa umma ni muhimu sana ili mtu awe na taarifa sahihi. Kuna mtu anahitaji kusoma na anashindwa kwa kuyokua na taarifa sahihi.

Sidhani kama OUT wanahangaika sana kutafuta wanafunzi kwasababu ni chuo cha umma na kina mfumo wa tofauti kinapaswa kwaeleza wananchi wengi ambao hawaelewi mfumo unaotumiwa na chuo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwann kwny center zenu za mikoani mnakuwa wasumbufu sana kuwahudumia wanafunz wanaosoma cert na dip?nasema hvyo kwakuwa mm n muhanga ktk hlo uan mnaboa sana
 
Back
Top Bottom