Ulishawahi kunusurika kifo? Ulijisikiaje vile unaona kabisa unaondoka

kaka hio sio chai ni kweli mimi , hio kitu ilishawahi nikuta wakat niko darasa la nne nilikuwa nimelala mchana, sasa kamlango kaka funguka na upepo, aisee mwili ukawa mzito, nakosa kupumua, mdomo mzito kuongea, kupiga kelele nashindwa alafu nilikuwa ndan peke angu, ila nilfanikiwa kujitoa kwenye situation ile aisee nilitoka nduki ndani kwenda nje, mpka leo sijui ile MERCHANISIM gan.
Hawezi kuelewa hiyo hali na haijui mpaka wamsimulie kijiweni kwake ndio ataamini.
 
Sikujua namna nilivyohama seat iliyoondoka na watu karibia wote baada ya ajali, Mungu yupo , Tena ana uwezo kuliko akili zetu

Mungu awalaze mahari pema peponi wale ndugu, they were the best compared to me, sijajua kwa Nini nilibaki, ila Mungu huyu anajua sababu,

Kama anasoma comment hii huyu Mungu ajue it sounds like prayers,awafunulie Hawa wasioamini mambo aliyonifanyia Mimi ili wamwamini kama Mimi,japo Bado Huwa natenda dhambi ilaa asinichoke,.

Guys Mungu anatupenda sana, nilijifunza kitu kufa au kuishi ni kwa neema tu, anapokufa mtu usihoji sababu ya kufa kwake,Kuna watu kibao wanatakiwa kufa ila wanaishi, alafu wanaokufa unaona kabisa kama wangeishi hiviii ila ndio wamekufa, MIMI NI NANI MPAKA NIWEPO HADI LEO!!???
Ni randomness au mipango ya Mungu?
 
Nilitoka mbali huko,
mshenzi mmoja tumetoka wote home,mama yangu anapika kuku wa kienyeji.
Hatukurudi.
Hawa sijui polisi waliandikisha pale fire tumekufa.
Yaani mochwari hii hapa.
Dah malaika wapo tu,doctor mmoja muhindi ndio akasema wazima hawa piga drip.
Siku3 tunazinduka ni km mazingaombwe.
Toka icu pelekwa kibasila.
Dah jamaa wakataka kunikata mguu.
Kumbe ni deal madoctor na kulikua na bwege mmoja nje pale anachonga magongo
Kwahiyo kuwa kilema ni sekunde tu.
Nilipiga kelele mpaka Mungu alisikia ndio nikapona
 
MIMI nina matukio kama mawili ivi.
1. Nakumbuka wakati niko mwaka wa tatu chuoni, mwezi kama wa 12 iv, ndio tunaelekea mwezi wa 1, nakumbuka ilikuwa mkesha nimekaa na pisi yangu ya kimeru night baridi inapiga hatari tuko kwenye vimbweta bana ile tuna enjoy that moment mpaka saa saba , nikaondoka kurudi hostel kulala, kumbe bana baridi ilipiga sana kifuani, na wakati huo mimi huwa nina (ASTHMA), kesho yake usiku nilikuwa bar naangalia mpira na jamaa yangu, ila ni kama hali siielewi ya kifua maana huwa nabanwa na kukosa kupumua, ila sio kwa siku ile, jamaa yangu akaniaga katangulia nikabak mwenyewe mida ya saa 1 usiku, nikaona mbna kama sielewi elewi, nikaanza kuondoka taratibu iv kirudi hostel, nikafika, nikatulia nikameza dawa, ila we kimbembe kikaja usiku wa manane pumzi zinakata kbsaa, nikamwamsha jamaa + mama anayemiliki hostel wakaniitia boda wakanibeba mpka hospital iv town kule nikapigwa sindano za kutuliza nikarudishwa hostel kulala , aisee hali ika serious saa 11 alfajir nikachukuliwa tena mpaka zahanat ya jeshi nikapigwa tena sindano sikupata nafuu, walipoona wameshindwa nikapigwa rufaa kwenda hospital kubwa ya kijeshi as mtoto wa askari nikapelekw bwana kufika kule, siwez tembea nakosa kupumua, nikawekwa kwenye wilchair kupelekw wodini, aisee nilipigwa sindano zaidi ya 21 within 2 weeks , marafiki wa class na hostel , pisi yangu, mama na mdog wangu walijua natembea kbsaa, nilikuwa nalia najua kbsaa sitoboi, ikafika time nikaletewa mpaka mitungi ya gesi kwaajil ya kupumulia, nikajua basi nikasema wacha niitiwe padre niungame dhambi ili nikalala niwe na aman.
Ila nashukuru MUNGU nilikuja kupata nafuu, nikarudi chuo ila napo sikuingia class nilikaa zaid ya wiki na siku kadhaa maana nilikuwa mtu wa kulala ndio napumua vzuri ila nikisimama na kutembea basi sipumui vizuri , hata nilivyorudi darasani na ilikuwa karbu na mitihani, maticha wengi walikuwa wananiandikia max za bure na kuwekewa coirsework nzuri , mkeka ukiletwa nakuwa nimewazidi wengen class, SITAKUJA KUSAHAU.
Umepata dawa ya pumu
Mimi nimeipata ukubwani inani attack kipindi cha baridi kama hiki jana saa nane usiku nimechoma sindano na leo saa sita mchana sasa hivi ndo nimerudo hali ya kawaida nilikaa kwenye gari lenye ac kali plus barid linaloendelea
Nahisi yako ni kama yangu baridi kali inalrta shida
 
Bora yako wewe mimi baridi, pafume kali, vumbi la aina yoyote, kukimbia sana aisee lazima viniletee matatizo. Jeshini nimeshindwa kwenda sababu ya hii kitu wanaogopa nisije kuvuta mazima maana kule ni mziki niliumia sanaa kwa kukosa nafasi huko, DAWA YA KUKITIBU SIJAWAHI KUIPATA KABISAA.
 
Mimi kifua kilikua kinanisumbua mda tu na kilianza utotoni
Alafu nimedevelop mwili flan wa kusikia baridi wakati wote
Ila pia pafyum situmii na jasho kali linaniamshia mafua then kifua
Ila miaka kama minne nyuma ndo hii hali inanitokea sana
Ya kubana kifua
So sinywi maji baridi
Sishiki maji baridi
Na vinywaji barid sinywi
Ila pia nalala nimejifunika vizuri

Niliona shuhuda sehem juu ya karafuu wanasema unaziloweka then unakunywa asubuh na jion mfululizo inaponyesha kabisa pumu
Alikua ni kwenye group flan mtu anatoa ushuhuda embu jaribu hii
Binafsi sijajaribu ila kwa jana kilichonikuta ni hatari itabidi niingie chimbo
 
K
Mgodini huko lwamgasa geita,nilikuwa shimoni nachoronga mwamba,kumbe huko juu kuna sehemu ilikuwa na ufa wa muda mrefu tu,kutokana na milipuko ya mara kwa mara hiyo sehemu ufa ukawa unazidi kutokea. siku hiyo nikapiga kaz mimi na jamaa yangu(rip mangu aka ntuzu man)ghafla udongo ukaanza kudondoka kidogo kidogo kiasi cha kutokuhofia chochote.

Machale yakanicheza nikamwambia mshkaji wangu tupande,mi nikatangulia yeye akawa ananifata kwa juu,nikaivuka ile sehemu yenye ufa kwa umbali kama wa mita 4 hivi,ile nimevuka tu nikasikia muungurumo mkubwa sana kumbe ni ile aridhi inaporomoka,ikawa imeshuka na mshkaji wangu mpaka chini kama mita 35 kutokea pale,nilipanda juu kwa kasi ya 5g huku nikiwa nimerukwa na akili kwa kile nilichokiona.
Wa hiyo jamaa alipona??
 
Mimi kifua kilikua kinanisumbua mda tu na kilianza utotoni
Alafu nimedevelop mwili flan wa kusikia baridi wakati wote
Ila pia pafyum situmii na jasho kali linaniamshia mafua then kifua
Ila miaka kama minne nyuma ndo hii hali inanitokea sana
Ya kubana kifua
So sinywi maji baridi
Sishiki maji baridi
Na vinywaji barid sinywi
Ila pia nalala nimejifunika vizuri

Niliona shuhuda sehem juu ya karafuu wanasema unaziloweka then unakunywa asubuh na jion mfululizo inaponyesha kabisa pumu
Alikua ni kwenye group flan mtu anatoa ushuhuda embu jaribu hii
Binafsi sijajaribu ila kwa jana kilichonikuta ni hatari itabidi niingie chimbo
sawa nitajaribu ila changu nimerithi kutoka kwa baba, na baba alirithi kutoka kwa marehemu babu yangu.
 
Bora yako wewe mimi baridi, pafume kali, vumbi la aina yoyote, kukimbia sana aisee lazima viniletee matatizo. Jeshini nimeshindwa kwenda sababu ya hii kitu wanaogopa nisije kuvuta mazima maana kule ni mziki niliumia sanaa kwa kukosa nafasi huko, DAWA YA KUKITIBU SIJAWAHI KUIPATA KABISAA.
Choma 'Triamcinolone' wakati ambapo upo mzima yaani huna attack. Utanishukuru!
 
Nimesoma visa vyote, vingine nimecheka na vingine kusikitika , poleni kwa nyote ambao bado mnapitia wakati mgumu kiakili na kiafya iliotokana na na hivyo visa.

By the way ile feeling ya kuzima iko so weird, kuna the most peacifullness mwili unapitia.

Kule kuzima huwa ni God's protection kumwambia mja wake tulia mja wangu hili huliwezi, nitegemee mimi, this fear is far beyond for you to witness it all.. pumzika utaamka baadae..

Imagine wale ambao huwa wanapata ajali kuna wengine huwa wamevunjika na bado unakuta hawajajua wanaanza kutembea au kucheka. Akioneshwa tu ndo maumivu yanaanza.
 
A
Nilitoka mbali huko,
mshenzi mmoja tumetoka wote home,mama yangu anapika kuku wa kienyeji.
Hatukurudi.
Hawa sijui polisi waliandikisha pale fire tumekufa.
Yaani mochwari hii hapa.
Dah malaika wapo tu,doctor mmoja muhindi ndio akasema wazima hawa piga drip.
Siku3 tunazinduka ni km mazingaombwe.
Toka icu pelekwa kibasila.
Dah jamaa wakataka kunikata mguu.
Kumbe ni deal madoctor na kulikua na bwege mmoja nje pale anachonga magongo
Kwahiyo kuwa kilema ni sekunde tu.
Nilipiga kelele mpaka Mungu alisikia ndio nikapona
Hàa baby Acha fix
 
Back
Top Bottom