Ulishawahi kujikuta mjuaji kwenye maakuli ukaongeza kiungo fulani kwenye chakula ukaishia kuharibu?

Black Opal

JF-Expert Member
Jan 22, 2023
201
262
Habari wazee wa masotojo,

Moja kwa moja kwenye mada. Hii sikufanya mimi, alifanya dogo nyumbani. Alikuwa anataka kutengeza juice amazing ili aoneshe ujuzi wake.

Mango-Juice-8.jpg

Basi akachukua maembe na pensheni freshi, akatia ka hiliki vizuri na sukari safi, sasa kwenye kuongeza madikodiko si akaweka na vitunguu swaumu 😂 😂 😂 😂 eti ili juice inukie vizuri.

Yaani kila aliyekuwa anakunywa lazima aulize kuna nini humu, akisikia vimewekwa vitunguu swaumu ili kuongeza harufu nzuri anakufa mbavu. Juice ilibidi inywewe kibishi maana ilikua nyingi😂😂😂😂.

Vipi wewe, ulishawahi kujikuta mjuaji au ukataka ku impress watu ukaishia kutoa kituko?
 
Nliwahi kuzidisha mint na lemon zest kwenye juice matokeo yake juice ikawa chungu though ilikuwa na harufu nzuri.

Nilishawahi kuzidisha bakig soda kwenye biscuits ,zikawa chungu na harufu kama sabuni ya unga hivi.

Nilishazidisha paprika powder kwenye mchuzi ukawa mchungu.

Niliwahi kuzidisha red chilli powder nikidhani ni kashmir red chilli powder ambayo huwa ni mild kiasi, matokeo yake mchuzi ulikuwa ukiwasha mnooo!!
 
Habari wazee wa masotojo,

Moja kwa moja kwenye mada. Hii sikufanya mimi, alifanya dogo nyumbani. Alikuwa anataka kutengeza juice amazing ili aoneshe ujuzi wake.

View attachment 2599244

Basi akachukua maembe na pensheni freshi, akatia ka hiliki vizuri na sukari safi, sasa kwenye kuongeza madikodiko si akaweka na vitunguu swaumu 😂 😂 😂 😂 eti ili juice inukie vizuri.

Yaani kila aliyekuwa anakunywa lazima aulize kuna nini humu, akisikia vimewekwa vitunguu swaumu ili kuongeza harufu nzuri anakufa mbavu. Juice ilibidi inywewe kibishi maana ilikua nyingi😂😂😂😂.

Vipi wewe, ulishawahi kujikuta mjuaji au ukataka ku impress watu ukaishia kutoa kituko?
Niliweka tangawizi kweny maharage
 
Mwaka 2012, nikiwa mkoani Tabora maeneo ya chemchem nipo geto na mzee, kulikuwa na kama. nusu kilo hivi ya mchele, basi me nikaona ni ndogo haitotosha kula watu wawili hadi night, basi likaja wazo la kufanya wali uwe mwingi,

Nikapanda shop chap nikachukua hamila ya buku yaani vijiko 20 vya sh 50, nikaiweka yote kwenye nusu ya mchele,

Tulilala njaaa , havikulikaa
 
Hiyo buku ungeongeza robo kilo ya mchele
 
Nliweka maziwa kwenye njegere.
Ladha nzuri ila hiyo harufu kila ukisogeza Karibu na pua unatamani utapike.
Nkaja kutia mchuzi mix nyingiii ili kutoa harufu lakini haikusaidia
 
Tangawizi ktk magarage ni nzuri ila ikaange na kitunguu then na maharage yaliochemka yakaange pamoja then weka mchuzi acha uchemke ongeza na nazi oya pilipil kidgo maharage yananoga kikquma
 
Back
Top Bottom