Ulianza lini kupenda na kufuatilia SIASA?

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
9,686
13,052
katika mazingira tofauti tofauti, mathalani mitandaoni, vyuoni na majukwaani kuna aina tofauti tofauti za wanasiasa na siasa. wapo vijana katika siasa, wazee, wanawake kwa wanaume.

wapo wanataaluma wa siasa za kitaifa na kimataifa. Lakini pia wapo wasio na taaluma bali vipaji na utashi wao tu kupenda na kuingia kufanya siasa..

Na katika makundi yote ya wanasiasa, wapo wanao weza kudhibiti hisia zao za kisiasa vema sana, na wengine bado ni dhaifu katika kujizuia na kuwastahimili wale wenye maoni na mitazamo tofauti na yao kisiasa...

na kwahivyo,
utashi, hekima na busara katika kujenga na kutetea hoja dhidi ya upande wenye utofauti wa maoni na wengine, imekua ni miongoni mwa vipimo muhimu sana kubainisha ukomavu wa kisiasa wa mwanasiasa husika, achilia mbali msimamo 🐒

nini kilikuchochea,
nini kilikuvutia na kukusababisha kuamua kufuatilia siasa katika kiwango hicho ulichonacho sasa?

uliwezaje kua katika hali hiyo ya ukomavu uliojaa ustahimilivu, hekima, busara na subra licha ya maoni na mitazamo ya wengine kua tofauti na wako vikiambatana na kejeli, mizaha, ghadabu na pengine matusi ya nguoni dhidi yako?🐒

tafadhali shirikisha uzoefu wako JF fraternity inufaike na maarifa hayo muhimu kuepuka lugha na mambo yasio faa katika siasa na tuwe wastahimilivu na wenye subra kama wewe na hatimae sote kwa pamoja tufanye siasa za kistaarabu 🐒
 
Siasa ni mwenendo na mtiririko wa maisha ya kila siku ya mwanadamu.Hapo kuna swali moja tu.
-Ulianza kuishi lini?Utakuwa umeijibu siasa.
inawezekana uko kwenye kundi la wenye taaluma hiyo 🐒

anaesema hataki kuskia kabisa habari za siasa unamzungumziaje?

anakataa maisha au kuishi?
 
Huyo aitwe "ANAJIDANGANYA"!Hana tofauti na anayekataa kupiga kura kipindi cha uchaguzi kwa kujiaminisha CCM wataiba kura yake.
sure,
coz politics is life...
thus why nataman kujua why wengine wana hekima na busara sana kwenye siasa licha ya utofauti wa kiitikadi na maoni wengine hawana 🐒
 
zingatia signal, mathalani....

ukiniporomoshea la nguoni ati kwasabb tu maoni yangu ni left dhidi ya right ambayo ni yako,

najua hapo busara hakuna ni zero square 🐒
Kwani matusi huwa unayatambuaje?Je,ni kwa kuyasoma,kuyaona,kuyanusa au inakuwaje?Unayapimaje?
 
Wengi tunahusisha siasa na mambo ya vyama na serikali kutokujua siasa ipo kila sehemu katima maisha yetu ya kila siku toka tunazaliwa kama alivyo comment Moisemusajiografii

Maisha yako ya nyumbani na mkeo ni siasa tosha.

Ila ukiongelea siasa ya kivyama/serikali/nchi, binafsi nahisi nilianza kufuatilia rasmi kipindi cha campaigns za 2015 mpaka awamu ya Magufuli yote. Pale siasa ya nchi ndio ilikuwa na hamasa.

Kwa sasa awamu hii, ni bora yaende tu maana hakuna la kufuatilia zaidi ya kusikia mijtu mizima na akili zao timamu ikimshukuru mama kwa mvua kunyesha au jua kutoka, hivyo naweza sema sifuatilii tena siasa za nchi.
 
Siasa ni upumbavu kama ilivyo mpira, kemea siasa na mpira kwa nguvu zote.

Siasa ni kwa ajili ya kumfaidisha tajiri na kumkandamiza maskini. Eti mtu anasema asiejihusisha na siasa anajidanganya coz siasa ni maisha??? How?
 
Kwani matusi huwa unayatambuaje?Je,ni kwa kuyasoma,kuyaona,kuyanusa au inakuwaje?Unayapimaje?
Ikiwa maoni yako ni left na yangu ni right tumejadiliana weeee...

moja akikwama, na akipandisha mori anatoka kwenye reli....

akianza kuleta hoja za center, ambayo haikuepo, tayari ataanza kuyaporomosha ya kutosha na hapatakua na hoja tena, japo yawezekana ni haki yake pia lakini isiyo na maana 🐒

hekima na busara ielekeze tu kutafuta lugha au namna nyingine ya kumuifluence left awe upande wako ambao ni right bila kumlazimisha wa kuyaporomosha akikataa 🐒
 
Bado haujaeleza matusi ni nini hasa.Matusi/tusi ni tafsiri hasi imuijiayo mtu/watu kwa kutokubaliana na neno husika.Siyo lazima unalodhani tusi nami nikalazimika kulitafsiri hivyo na kinyume chake.Huku uswahilini ukikuta watu wanaongea maneno yao na kucheka wewe unaweza ukadhani wanatukanana au kugombana.
 
Siasa ni upumbavu kama ilivyo mpira, kemea siasa na mpira kwa nguvu zote.

Siasa ni kwa ajili ya kumfaidisha tajiri na kumkandamiza maskini. Eti mtu anasema asiejihusisha na siasa anajidanganya coz siasa ni maisha??? How?
Maisha ukiyakemea huwa yana kawaida ya kutoa adhabu.Je,unapenda kufa huku unacheka au unalia?
1-Ufe kwa kutekenywa unyayo (unacheka hadi unakufa)AU
2-Ufe kwa kukatwa shingo kwa kisu?
 
Siasa ni upumbavu kama ilivyo mpira, kemea siasa na mpira kwa nguvu zote.

Siasa ni kwa ajili ya kumfaidisha tajiri na kumkandamiza maskini. Eti mtu anasema asiejihusisha na siasa anajidanganya coz siasa ni maisha??? How?
wew una kipaji tu, na actually unafundishika kirahisi 🐒

ungekua mwanataaluma wa siasa uelewa na ufahamu wako katika siasa ungekua ni zaidi ya kujua kwamba mpira ni siasa .....

ungejua kwamba kule kwenye nyumba za ibada ni siasa inafanyika, inaitwa religious politics, kule kwenye family yako ni siasa inafanyika, inaitwa family politics, kule kazini kwako ni siasa inafanyika, ukiwa shuleni ni siasa inafanyika, huko kwenye mpira n.k

ndio maana tunasema siasa ni maisha....

ndio maana Aristotle alisema human being are political animals...

kwamba huwezi epuka siasa maishani mwako upende usipende 🐒

mipango yako yote maishani na maamuzi yako ni pure politics, ndio maana unaweza mwanmbia mwenzio ntakupigia cm baadae na usipige wala kutuma meseji ...🐒
 
Wengi tunahusisha siasa na mambo ya vyama na serikali kutokujua siasa ipo kila sehemu katima maisha yetu ya kila siku toka tunazaliwa kama alivyo comment Moisemusajiografii

Maisha yako ya nyumbani na mkeo ni siasa tosha.

Ila ukiongelea siasa ya kivyama/serikali/nchi, binafsi nahisi nilianza kufuatilia rasmi kipindi cha campaigns za 2015 mpaka awamu ya Magufuli yote. Pale siasa ya nchi ndio ilikuwa na hamasa.

Kwa sasa awamu hii, ni bora yaende tu maana hakuna la kufuatilia zaidi ya kusikia mijtu mizima na akili zao timamu ikimshukuru mama kwa mvua kunyesha au jua kutoka, hivyo naweza sema sifuatilii tena siasa za nchi.
umeeleza vizur sana mwanzo,

ila conclusions yako nadhani inahitaji michango ya wadau kwamba tunawzaje kua na siasa safi tukazifanya kwa lugha ya kiungwana, hekima na busara ktka kueleza hisia zetu za kutokuridhishwa au kuridhishwa na jambo fulani kiungwana bila kukejeli🐒
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom