Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 3,894
- 7,426
Sasa kwanini hukumuaga chief 😂😂Wapo wengi sana, mimi mwaka juzi kuna classmate alikuwa anaolewa. Sikuwahi kuwa na ukaribu nae sana japo nilishawahi kuambiwa mbona kama ananielewa, nikapotezea. Siku moja tukiwa kwenye maandalizi ya shughuli yake akaniambia kuna jambo ataniambia nimpigie atakaponitext, muda ukafika nikafanya hivyo. Akaniambia ya moyoni anataka aniage, nikahisi ni mtego nikapotezea. Kwa bahati mbaya shughuli yake sikuweza kushiriki nilikuwa safarini. Akaja kuniambia ule ule ujinga tena akiwa ni mke wa mtu nikampotezea adi leo hii kaninunia hata tukikutana kwenye matukio hataki hata salamu yangu.
Nmejiuliza hivi mtu kama huyu kaolewa kwa kuridhia kwa upendo au ndio nayeye kaolewa kama hadhi tu.