SoC02 Ukitaka kufanikiwa kwenye maisha yako, basi zingatia haya

Stories of Change - 2022 Competition

Abou Twika

New Member
Jul 13, 2022
4
18
By Abou Twika
0784327893

Mafanikio ni safari yenye vingi vikwazo, vilima, maumivu, na mipito ya aina yake. Uwepo wa vikwazo katika safari zetu, ni moja ya sababu inayopelekea wengi wetu kukata tamaa, na hata kufikia tamati ya kuendelea kuamini mwagiko la jasho. Kuna njia kadha wa kadha ambazo wengi walizitumia na hata wewe unaweza kuzitumia kupata mafanikio, lakini tambua ya kwamba mafanikio faafu ni yale yaliyopitia kwenye mikono au ushiriki wako kikamilifu wakati wa kuyatafuta. Mara nyingi mtu ambaye alisota miaka kwa miaka kwenye matope, ni nadra sana kupuuza kalamu na daftari ule wakati wa kuyala matunda yake.

Mafanikio ya kweli, si mfano wa kulala na kuamka asubuhi. Yatakikana uvumilivu, subra, na imani ya kwamba ipo siku magumu unayoyapitia yatakuja kugeuka na kuwa historia, kwani wahenga walisema "subira yavuta kheri" na mwenye kuvumilia ndiye hula mbivu. Binafsi kama ningalipata nafasi ya kuongeza orodha ya makosa ya kijinai, basi hata mtu yeyote mwenye kukata tamaa, ilihali bado yuko na uhai wa roho, mtu kama huyo angestahili kuhukumiwa.

Nachokiamini mimi, kitu pekee kinachoweza kukutenganisha mtu na ndoto yako, ni pindi Mwenyezi Mungu atakapoamua kukunyofoa roho na kukupumzisha katika makazi ya milele. Uhai na afya njema kwa binadamu, ni nyenzo katika kupambania kiu ya kile unachokihitaji.

Changamoto na vikwazo, visiwe tiketi ya kuzika malengo yako. Jizatiti kwa namna yeyote, na usichoke kutafuta daraja la kukuvusha katika mstari wa changamoto, kuelekea kwenye kilele cha mafanikio yako.

Hivi unatambua ya kwamba, mlemavu si kilema, ila unaweza kubakia kuwa kilema daima kama na kama tu utayapuuza magongo katika nyakati ambazo unayahitaji kuchechemea, kama mbadala wa miguu yako. Kiukweli inanishangaza sana, pindi nionapo mbilikimo wakilazimisha ungongoti katika nyakati ambazo haziwataki kufanya hivyo, na twasahau kwamba muda ndiye hakimu wa kweli.

Andiko hili ni mwarobaini kwa yeyote mwenye kukata tamaa. Sasa nini unatakiwa ukifanye?

Zingatia haya.

Mosi
, weka uthubutu. Hii ni ile hali ya mtu kuacha kufanya mambo kinadharia. Mthubutu, ni mtu ambaye hujenga imani ya kile anachokifanya, hutenga muda wake na kuangalia ubunifu wa namna gani ya kipekee anaweza kufanya katika kitu kilekile ambacho hufanywa na wengine, pia mthubutu ni mtu mwenye kiu na njaa ya mafanikio. Uthubutu, ni nguzo muhimu sana kwa mtu yeyote mwenye kuhitaji mafanikio. Kamwe huwezi pata ufanisi wa unachokifanya kama hukuwahi kuthubutu, iwe katika jambo la kibiashara, kielimu, kisiasa n.k

Pili, nidhamu. Kutokuwa na nidhamu ni moja ya kitu kinachoweza kukurudisha nyuma kwenye kilele cha mafanikio. Nidhamu ni kitu muhimu na huchagiza maemdeleo chanya ya mtu binafsi, taasisi, na hata katika ngazi ya familia. Ili ufanikiwe kwenye maisha yako, basi hupaswi kutengana na nidhamu, kwani ni nguzo muhimu inayoweza kukufikisha kule utakako. Kuwa na akili darasani, si kitu pekee kinachoweza kukufanya uweze kufanikiwa kwenye ufaulu wa mitihani yako. Taasisi yeyote inaweza kushuka kiutendaji, na hata kimapato kama suala la nidhamu kwa watumishi halitotiliwa mkazo. Hata kwa mjasiriamali, usipokuwa na nidhamu ya kile kidogo unachokipata, pia ukakosa nidhamu kwa wateja wako, basi tegemea anguko la biashara yako. Itoshe kusema nidhamu ni mfano wa nambari kiraka, kwani inahitajika kila mahali.

Tatu, epuka kuweka lazima ya mafanikio kwa kitu unachokipenda. Nina imani ya kwamba, kila binadamu kuna kitu fulani ambacho ni chaguo faafu ndani ya moyo wake. Kuna baadhi ya watu tangu wakiwa wadogo walisikika na kuonekana kuwa na ndoto za ualimu, udaktari, unahodha n.k
Nachokikusudi kukueleza ni kwamba, weka ndoto ya kuwa daktar lakini usiweke akilini kuwa lazima kuwa daktari.

Kwanini?
Kufanya ndoto kuwa lazima inaweza kuwa ngumu kwako ile nyakati itakayokubidi kubadlika na kugeukia kwenye kitu kingine kinachoweza kukupa mkate wa kila siku.
Tambua ya kwamba, mafanikio hayako kwenye ndoto yako tu. Kuna nyakati ndoto unaweza shindwa kuifikia pamoja na jitihada zako zote. Hivyo hupaswi kuulisha ubongo wako kasumba ya ulazima wa ndoto, ila ipe ndoto yako kipaumbele ili isiwe ngumu wakati wa mabadiliko.

Nne, usiache kufanya ulichokuwa unafanya. Sina maana ya kwamba huwezi kubadilika na kuanza kuuza machungwa kama ulitajirika kupitia biashara ya kuuza karanga. Ninachokimaanisha, wengi wetu ni wepesi kuridhika punde tu tukishazipata shilingi kadhaa. Tusichokijua, kingi si kingi kwenye hesabu ya kutoa, ila kinaweza kuwa kingi na zaidi ya kingi kama kitaendelezwa daima katika hesabu za kujumlisha.
Tunatakiwa kuongeza na kutanua wigo wa vile tulivyokuwa tunavifanya, kama ulikuwa hulali kipindi uko mstari wa sufuri, basi unatakiwa hata kusinzia iwe ndoto kwako katika kipindi ambacho ushapata miliki kadhaa ya mali.

Tano, epuka kukata tamaa. Binafsi ninauhusudu msemo usemao "mtembea si mkaa". Sikuzote mwenye kutembea na kuambua tupu, kamwe hawezi fanana na yule aliyekaa pasi na kutembea tembea. Mwenye kutembea hata akarudi nyumbani na mikono mitupu lakini vingi ataviambua kama vile, kuongeza maarifa, kupata fursa mbalimbali, kujifunza n.k
Kukata tamaa ni kosa kubwa tunalolifanya. Tukumbuke hata Roma haikujengwa kwa siku moja, na "haraka haraka haina baraka" wahenga walisema.
Mafanikio yanahitaji jasho lako na damu, maumivu, uvumilivu, na pindi uonapo koswakoswa za mishale basi zidisha juhudi, hiyo ni dalili ya ushindi wa kile unachokipigania.

Sita, epuka mkato wa mafanikio. Mkato, ni ile njia isiyo halali/ njia ya kughushi katika kutafuta mafanikio. Mwenye kutumia njia ya mkato, moja kwa moja anajiandalia bomu ambalo muda wowote linaweza kuripuka.
Unaweza kufaulu mitihani, unaweza kupata mali kwa njia nyang'anyi, na hata kununua haki ya mtu fulani, lakini sikuzote ni nadra kudumu mafanikio yaliyopatikana kwa njia ya mkato. Kheri ya mwenye kutambaa au kuchechemea kuliko ya yule mwenye kuharakia kutembea akiwa anatambaa.
Mafanikio ya kweli, ni yale yaliyopewa muda wa kimchakato.

Saba, anza kufanya kidogo ulichonacho. Tambueni, kingi ni kidogo kilichoongezewa mwendo. Njia pekee na faafu ya kukipata kingi, ni kukidunduliza kidogo chako, kwani tajiri ni masikini ambaye aliunganisha vipunje kuwa kitu kizima.
Katu, usikibeze kidogo ulichonacho, unayo nafasi ya kupanda mche wa kidogo na ukavuna kingi zaidi, kwani tusichofahamu mbele ni nyuma iliyojongea hatua.

Mwisho, safari ya mafanikio, ni mfano wa tamthiliya. Kuna kipande kitakupa furaha, huzuni, mpwito na mengine mengi. Hivyo subira, ni nguzo ya kukufikisha kwenye kilele cha mafanikio.
 
Congrats mkuu kabla ya kulala nmepitia hii thread nmegundua iko na madin sana

Be blessed
 
Back
Top Bottom