Ujenzi wa daraja la Kivule wageuka shubiri kwa wakazi

Aquatic

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
715
268
da2-jpg.703251

Mkandarasi Singh and Sons anaitia aibu taaluma ya uhandisi majenzi na mihimili, ujenzi wa daraja aliouanza hivi karibuni mwanzoni ulikuwa ni tumaini jipya kwa wakazi wa kivule na vitongoji vyake ila sasa umegeuka shubiri kwa wakazi hao. Mkandarasi huyo anatia mashaka uwezo wake katika taaluma hiyo kuanzia vifaa na wataalam alikuwa nao ( equipments & Skilled Labour ), kazi aliyokuwa nayo dhahiri shahiri sasa inaonekana kumshinda .

Mfano siku za hivi karibuni alianza uwekaji wa mawe kwa ajili ya kitako cha daraja hilo baada ya ubomoaji wa daraja la zamani kukamilika kazi hiyo mpaka sasa hajakamilika takribani wiki ya pili sasa, zipo sababu yingi za kitaalam na uzembe zinazopelekea kutilia mashaka uwezo wake.

Mosi: Man power anayoitumia kwenye kazi hiyo
Pili: Equipments
Tatu: Time consumed

Kazi ya upangaji mawe kwa ajili ya kitako kwa Mkandarasi mwenye experience ni kazi ya siku mbili pamoja na umwagaji zege ni kazi ya siku moja tu, chakushangaza na kusikitisha Singh & Sons sasa ana wiki ya pili kazi hiyo haijakamilika, man power anayoitumia kwa kazi hiyo hawazidi watu watatu. Hapa ndio unatambua mkandarasi huyo hana wataalam wanaojua ukubwa wa kazi aliyonayo na idadi ya skilled labour na unskilled labour wanao hitaji kwa kazi hiyo.

Ushauri wangu kwa Mkandarasi Singh & Sons kama hukuwai kushiriki katika mradi kama huo wapo wataalam wengi sana ambao unaweza kuwatumia kwa ushauri na kazi hiyo ikaenda kama inavyotakiwa iende bila kuitia doa taaluma ya Uhandisi, kwasasa hata mtoto wa shule asie na ufahamu wa taaluma ya ujenzi wanaanza kuulizana kulikoni tena au nini unachokifanya hapo?.

Mwisho
Mkandarasi umeshindwa kujenga diversion ya kueleweka hali inayopelekea wakazi wa kivule kupata kadhia ya usafiri kuanzia wazee, wanafunzi, watoto wadogo, mama wajawazito, wagonjwa na wake kwa waume hali inayoplekea kutembea umbali mrefu kufuata usafiri wakuwafikisha sehemu zao za kazi na makazi na pia kutumia nauli mara mbili kuliko waliyokuwa wanatumia hapo awali kwa magari ya abiria kushindwa kupita sehemu uliyoshindwa kujenga diversion ambayo hukatika pindi mvua isiyozidi mm 10 tu inaponyesha. Ujenzi wa diversion sio feva kama unavyoufanya katika mradi huo, kama uwezo wa kujenga daraja hilo huna usingebomoa daraja lililokuwa likitumika na wakazi hao kwa zaidi ya miaka 5 licha ya kwamba lilikuwa halipo katika hali nzuri. Mkandarasi Singh & Sons wajengee diversion ya kueleweka wakazi wa kivule ili waondokane na kadhia wanazopata hivi sasa , ili uendelee kusubiri mvua za masika zinyeshe na kuficha mapungufu yako na ujipange upya tena kwa kazi hiyo inayoonekana kukushinda.
 
Back
Top Bottom