Uhasama wa Everton na Liverpool ulianzia hapa

DIDAS TUMAINI

JF-Expert Member
Nov 11, 2014
234
657
Kulikuwa na timu iliyoitwa Everton kutoka kitongoji cha Merseyside cha jiji la Liverpool nchini England.

Timu hii ilikuwa ikitumia uwanja wa Anfield, uliokuwa ukimilikiwa na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo, John Houlding, mfanyabiashara mkubwa wa Freemason kutoka jiji la Liverpool.

Ukatokea mzozo mkubwa baina yake na bodi ya klabu, wajumbe wakipinga masharti yake mapya kwa Everton kuukodi uwanja wa Anfield.

Mzozo huo ukapelekea wajumbe kuamua kuihamisha timu kutoka uwanja wa Anfield na kujenga uwanja wao karibu yake na kuuita Goodson Park.

Freemason Houlding akabaki na uwanja bila timu, hivyo akaamua kuanzisha timu yake ili itumie ule uwanja.

Watu wa kitongoji cha Merseyside na jiji zima la Liverpool hawakulipenda wazo la Houlding la kuanzisha timu katika mji wao lao kwani hawakutaka timu nyingine katika mji wao zaidi ya Everton.

Freemason ni Freemason tu, akakomaa na wazo lake la kuanzisha timu, hadi likafanikiwa…timu hiyo ndiyo Liverpool FC.

Ule mgogoro wa uwanja na upinzani wa kuanzisha timu mpya ukasabisha uhasama mkubwa kati ya timu mpya, Liverpool FC, na ile kongwe, Everton FC.

Uhasama huu ndiyo ukazaa dabi kubwa katika kitongoji chao cha Merseyside inayoitwa Merseyside Derby.

Dabi ni dabi tu, hakuna raha kama kumuona mpinzani wako akiteseka kwa maumivu hasa uliyomsababishia wewe.

Ndiyo raha wanayoipata Everton muda huu. Kuwakatisha Liverpool matumaini ya ubingwa ni jambo kubwa kwao zaidi ya alama tatu walizozipata.
 
Attachments

  • zakazakazi-20240425-0001.jpg
    zakazakazi-20240425-0001.jpg
    402.9 KB · Views: 6
Hiyo Ina Maana Manchester city Ni Champion Wa EPL 2023/2024.

Arsenal Hawezi Tena Hizi Mbio Kwa Manchester City Ikifika Mwishoni Wa Msimu.

Manchester City Kupoteza Mechi Mwishoni Mwa Msiku Kwa Kipindi Cha Misimu Ya Minne Hatujashuhudia Hilo
 
Nguvu za pesa, bila hela Mwacity ni mweupe kuliko hata Mashujaa FC

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.
 
Hiyo Ina Maana Manchester city Ni Champion Wa EPL 2023/2024.

Arsenal Hawezi Tena Hizi Mbio Kwa Manchester City Ikifika Mwishoni Wa Msimu.

Manchester City Kupoteza Mechi Mwishoni Mwa Msiku Kwa Kipindi Cha Misimu Ya Minne Hatujashuhudia Hilo
Usimalize maneno rorote laweza kutokea. Man city ana game 6 arsenal ana game 4 sioni arsenal akipoteza mechi tena city akitoa sare tu arsenal bigwa
 
Mimi namaliza maneno Man city bingwa
Na muhasibu alimaliza maneno kama wewe, leo yanamtokea puani.

Anyway, as a Chelsea fan lolote litokeage hata kama ni Luton kuchukua ndoo ila Arsenal aendelee kuikosa kila msimu. Ngoja nikaze maombi wapoteze na kutoa sare. Kwanza kipigo cha mbwa mwizi walichotupa mahasimu wao juzi kinawatosha sana kwa sherehe msimu huu.
 
Biashara ya Freemason ndio ipi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom