Ugomvi kati ya Nyerere na Malechela Chanzo...

NGULI

JF-Expert Member
Mar 31, 2008
4,803
638
Wana JF,

Katika kipindi cha uongozi wa Nyerere nilikuwa sijazaliwa kwa hio nimesikia kupita watu mbalimbali kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa hampenid kabisa Malechela na ilifika kipindi cha uchaguzi ndani ya CCM kwa ajili ya uchaguzi wa atakayegombea urais kupitia tiketi ya ccm Nyerere alisikika akisema ''Endapo Malechela angepewa ridhaa ya kugombea kwa tiketi ya CCM basi angerudisha kadi yake ya chama na kujiunga na upnzania'' Je ugomvi wake mkubwa na Malechela ulisababishwa na nini?
 
Nyerere aliwashutum, Malecela na H. Kolimba kwamba wanamshauri vibaya raisi (Mwinyi), Kolimba alijibu mapigo akapotea, Malecela alikaa kimya, bado yupo.
 
Wewe ulidanganywa, na ni afadhali umesema kuwa ulikuwa hujazaliwa kwa vile unamfahamu Maelecela leo kwa sababu ya Nyerere; wangekuwa na ugomvi basi hata jina la Malecela ungekuwa hulijui kabisa katika siasa za leo kwa kuwa Nyerere alikuwa na uwezo wa kufuta wanasiasa kabisa, wapo wengi sana waliofutwa na Nyerere. Malecela aliendela kutumika kwenye serikali ya Nyerere kwenye ngazi za juu sana serikalini mapungufu yake kwa muda mrefu sana hadi Nyerere alipostaafu. Hata hivyo Nyerere alikuwa anajua mapungufu yake ndiyo maana akasema kuwa mtu huyu hana uwezo wa kuwa rais. Kusema kuwa hana uwezo wa kuwa rais siyo kuwa walikuwa na ugonvi, ingawa Malecela na wafuasi wake walilichukulia hilo kama ugomvi, na inawezekana ndio wanaokupa taarifa hizo kuwa Nyerere alikuwa na ugomvi na \Malecela.
 
ni katika kupitisha serikali tatu mwaka 1992,nyerere aliwaona ni wahaini maana hawawaonei huruma wa znz,maana serikali tatu wanazolilia hawaziwezi hivyo ni watu wa kuonewa huruma na kubebwa tu katika muundo wa serikali mbili
 
Wewe ulidanganywa, na ni afadhali umesema kuwa ulikuwa hujazaliwa kwa vile unamfahamu Maelecela leo kwa sababu ya Nyerere; wangekuwa na ugomvi basi hata jina la Malecela ungekuwa hulijui kabisa katika siasa za leo kwa kuwa Nyerere alikuwa na uwezo wa kufuta wanasiasa kabisa, wapo wengi sana waliofutwa na Nyerere. Malecela aliendela kutumika kwenye serikali ya Nyerere kwenye ngazi za juu sana serikalini mapungufu yake kwa muda mrefu sana hadi Nyerere alipostaafu. Hata hivyo Nyerere alikuwa anajua mapungufu yake ndiyo maana akasema kuwa mtu huyu hana uwezo wa kuwa rais. Kusema kuwa hana uwezo wa kuwa rais siyo kuwa walikuwa na ugonvi, ingawa Malecela na wafuasi wake walilichukulia hilo kama ugomvi, na inawezekana ndio wanaokupa taarifa hizo kuwa Nyerere alikuwa na ugomvi na \Malecela.

Nakushukuru nimeelimika hapa kaka
 
Tatizo ni malecela kuridhia hoja ya serikali tatu ya akina jen ulimwengu na issue ya zanzibar kujiunga na oic. Ni hapo tu kabla ya hapo walikuwa maswahiba wazuri.
 
Back
Top Bottom