Uganda: Aliyeshindwa ubunge awanyang'anya Wananchi ambulance alivyokuwa amewapa

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
44,776
51,614
Mwanasiasa mmoja wa kike wa Uganda ameibua hisia tofauti mtandaonibaada ya kukiri kwa ujasiri kuwa ameamua kujirejeshea gari la wagonjwa alilotoakama msaada kwa wapiga kura wake kwa matumaini kwamba wangempigia kura.

Anite Evelyn, Waziri wa sasa wa Fedha wa Uwekezaji naUbinafsishaji nchini Uganda, aliwashangaza wengi baada ya kukiri kuwa kweli amejirudishiagari la kubebea wagonjwa alilolitoa kabla ya uchaguzi, akisisitiza kuwa wananchialiokuwa amewapatia msaada huo ni watu wasio na shukrani.

Ufichuzi wote ulianza baada ya akaunti ya X (zamani kiitwaTwitter) kwa jina @AfricaFactsZone kuchapisha habari za maoni yake baada yauchaguzi.

"Mwanasiasa wa Uganda, Evelyn Anite alichukua tena gari lawagonjwa alilotoa kwa wilaya yake, baada ya kushindwa katika uchaguzi wa2021," waliandika kwenye Twitter.

Anite Evelyn hakuwa na aibu yoyote wa kujutia kitendo hicho, ambacho baadhiwanakiona kama cha aibu.

Akijibu kuhusu uamuzi wake huo Bi Anite alisema: "@AfricaFactsZone, asante kwa kuleta hili. Kwanza, ni kweli nilirudisha gari langu la wagonjwa na sina pole kwa hilo. Kwa nini nilifanya hivyo? Ni kwa sababu hawakunipigia kura. Kwa hivyo ulitarajia niende zangu bila kitu? Wagalatia 6:7 Mtu huvuna alichopanda! aliandika kwenye ujumbe wake wa X.

My Take
Naunga mkono Uamzi wa mbunge,Kila mtu akale alikopeleka mboga 🤣🤣🤣🤣

Kuna yule wa Zimbambwe aling'oa miundombinu ya maji aloyowawekea baada ya kupigwa chini.

Hata Jiwe aliwaambia waliochagua chadomo wakadai maendelea huko 😂😂

Tukutane Oktoba 2025.
 
Kula kulana, mbona wananchi hawataki kuliwa na mbunge!!
Hata mimi ningesepa na chuma yangu nikapak home, litanisaidia mwenyewe kuendea hospital, bar na sokoni😆😆😆
 
Siasa ni biashara, sijui kwanini inatuchukua muda kulijua hilo, msipompa naye achukue mtaji wake....
 
Hiyo ambulance ilikuwa rushwa ili apewe kura. Wananchi hawakutimiza wajibu wao katika mkataba huo wa rushwa. Huyo bibie hajakosea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom