Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Mkuu tazama hizo picha hapo chini; nilikuwa mmikoa ya kusini just three weeks ago, tutatembelea banda la mkulima mmoja na kuona jinsi alivyojikwamua kwa ufugaji kuku wa kienyeji. Alianza kufugia kwenye banda la kupikia, then sasa amejenga banda jipya, anafuga kwa kutumia njia bora zaidi kuku wale wale wa kienyeji. Kwa hivyo haihitaji kuanza na maelfu ya kuku, bali kidogo kadri unavyoweza, kikubwa ni kuhakikisha unawapatia huduma bora zikiwamo chakula na madawa.

Cheers..!

Mkuu, Hebu ungemwaga kidogo utaalam au masharti ya kuzingatia unapoamua kufuga kuku wa kienyeji mzee!
 
Mkuu tunashukuru kwa hizo picha.
Sipendelei sana faida za chap-chap. Kuku wa kienyeji naona ni bara-bara kabisa. Mambo ya taratibu lakini yenye uhakika. Demand and supply iko poa.


Mkuu tazama hizo picha hapo chini;

cheers..!
nilikuwa mmikoa ya kusini just three weeks ago, tutatembelea banda la mkulima mmoja na kuona jinsi alivyojikwamua kwa ufugaji kuku wa kienyeji. Alianza kufugia kwenye banda la kupikia, then sasa amejenga banda jipya, anafuga kwa kutumia njia bora zaidi kuku wale wale wa kienyeji. Kwa hivyo haihitaji kuanza na maelfu ya kuku, bali kidogo kadri unavyoweza, kikubwa ni kuhakikisha unawapatia huduma bora zikiwamo chakula na madawa....
6697d1258456578-biashara-ya-kufuga-kuku-dsc04282.jpg




6698d1258456578-biashara-ya-kufuga-kuku-dsc04286.jpg
 
UFUGAJI BORA WA KUKU WA NYAMA NA MAYAI:

WIKI YA KWANZA:SIKU YA 1 - 6 WAPE:GLUCOSEBROILER BOOST AU AMINOVIT AU SUPERVITVIGOSTART KWENYE CHAKULA (KILO 1 KWA MFUKO 1 WA KG 50) KUANZIA WIKI YA KWANZA HADI YA 4
SIKU YA 7CHANJO YA NEWCASTLE - MASAA 2 TU, WEKA MAJI NA VITAMIN MARA BAADA YA KUTOA MAJI YA CHANJO
WIKI YA PILICHANJO YA GUMBORO - MASAA 2 TU, HALAFU ENDELEA NA MAJI YA VITAMIN
WIKI YA TATUDOXICOL AU CTC20% NA AMPROLIUM, VITAMIN NA MOLASSES KWA SIKU 5 - 7
WIKI YA NNEHAKIKISHA KUKU WA NYAMA WANAKUWA KATIKA DOSE KUBWA YA VITAMIN
WIKI YA SITAWAPE KUKU WA NYAMA MAJI YA VITAMIN ASUBUHI NA MATUPU JIONI
WIKI YA NANEWAPE KUKU WA MAYAI CHANJO YA NDUIDAWA ZA MINYOO (PIPERAZINE AU LEKIWORM)VITAMIN AU SUPERVIT LAYERSWALISHE GROWERS MASH AU FARMERS CONCENTRATE HADI MIEZI 3 NA 1/2 TUMIA LAYERS MASH WAKIFIKA MIEZI 4 KAMILI AU WAPE MAJANI
WIKI YA KUMI NA MBILIWAPE CHANJO YA NEWCASTLE ( RUDIA KILA BAADA YA MIEZI 3) MASAA 2 KISHA WAPE MAJI YA VITAMIN
WIKI YA KUMI NA SITAKATA MIDOMO KISHA WAPE NEOXYVITAL KWA SIKU 3-5 ANDAA VIOTA
WIKI YA 54WAPE VIRUTUBISHO VYENYE KUONGEZA WINGI WA MAYAI MFANO GLP ( KILO 1 KWA KILA KILO 50 ZA CHAKULA, WIKI YA KWANZA NA NUSU KWA WIKI ZINAZOFUATA NA VITAMIN
WIKI YA 72TUMIA V RID KUSAFISHA MABANDA ILI KUUA VIJIDUDU PIA WEKA MAJI YA DAWA HII KWENYE DISH YA KUSAFISHIA MIGUU (FOOTBATH) ILI KUHAKIKISHA UDHIBITI WA VIJIDUDU (BIOSECURITY) NA KWAMBA VIFARANGA WANAOWEKWA HAWAATHIRIWI NA VIJIDUDU HIVYO.
WIKI YA 96ONDOA KUKU WOTE WALIOZEEKA

All the Best
 
Mkuu naona shule hapo imetulia.

Lakini mbona mnazungumzia haya makuku ya kisasa tu? Je, ufuguja wa kitaalam wa kuku wa KIENYEJI unakuwaje? Kumbuka hawa nao wana soko zuri sana.

Mkuu, ni kweli kuwa kuku wa kienyeji ni bomba kweli kuanzia ladha, virutubisho ndani ya mwili hadi kipato, ila tofauti ni muda tu wa kuwafikisha hapo penye tija. Kidogo hao wa kienyeji nilijishughulisha wakati ule nikiwa kijijini mwanakwerere, lakini lipohamia Malindi nikagundua kuwa unaweza kupata nyama ya kuku ndani ya wiki 5 na mayai 5 kwa wiki kwa muda wa miaka 2 kutoka kwa kuku mmoja! Baasi nikaamua kuwaachia wale wa handeni na mwanakwerere waendelee na hao wanaojiokotea wanyewe!

Kuku wa kienyeji ni bora sana kwa lishe, ila ndio hivyo ukiaccumulate faida yake ni ndogo kuliko hawa tunaowaita wa kisasa. Si unajua wengi hatuna mirija ya EPA? Ukisubiri hadi wa kienyeji akomae, utalalabaho!
 
Nono,
Kuku wa kienyeji soko lake likoje sasa hivi ukilenga wateja wenye fedha (forget wauza chips)

Uyoga kwa mfano, una soko zuri japo ni wachache wanafahamu. Nataka kuamini kwamba soko la kuku wa kienyeji lipo. Tena ikibidi unazungumza na mteja na kuingia makubaliano hata kabla ya uzalishaji.
 
Nono,
Kuku wa kienyeji soko lake likoje sasa hivi ukilenga wateja wenye fedha (forget wauza chips)

Uyoga kwa mfano, una soko zuri japo ni wachache wanafahamu. Nataka kuamini kwamba soko la kuku wa kienyeji lipo. Tena ikibidi unazungumza na mteja na kuingia makubaliano hata kabla ya uzalishaji.

LD,

Nakuhakikishia ukiwa reliable supplier, soko la kuku hawa liko kubwa sana mkuu........! Mahotel makubwa wanataka kuku hawa, but can't get a reliable supplier......!
 
Kuku wa kienyeji ni bora sana kwa lishe, ila ndio hivyo ukiaccumulate faida yake ni ndogo kuliko hawa tunaowaita wa kisasa. Si unajua wengi hatuna mirija ya EPA? Ukisubiri hadi wa kienyeji akomae, utalalabaho!​
Mkuu Next Level,
Nilipomsoma Nono karibu ningeingia kingi. Ila utaona kwamba ufugaji wa kuku wa kienyeji inachukua muda kuvuna ila, ni katika hatua ya mwanzo tu unapoanza.
Maana ukiweka kuku 100, halafu baada ya miezi miwili ukaweka vifaranga wengine 100, ukaendelea kufanya hivyo kila baada ya miezi miwili - kuchelewa kukomaa sio issue tena. Utachelewa kuvuna wale wa kwanza tu.

Halafu dhana ya mtu kuwa mjasiriamali, ni kutambua soko limepungukiwa nini. Unahitaji kutumia nguvu kidogo kupata mafanikio makubwa. Sio kulala roho juu; presha inapanda presha inashuka.
 
Nono,
Kuku wa kienyeji soko lake likoje sasa hivi ukilenga wateja wenye fedha (forget wauza chips)

Uyoga kwa mfano, una soko zuri japo ni wachache wanafahamu. Nataka kuamini kwamba soko la kuku wa kienyeji lipo. Tena ikibidi unazungumza na mteja na kuingia makubaliano hata kabla ya uzalishaji.

Soko ni kubwa mno. Tatizo ni wachache mno kutokana na muda anaohitaji kufikia kuwa kitoweo. Bei yake ni zaidi ya mara 2-3 ya broiler, ila muda wa kumwaandaa awe kitoweo ni karibia mara 8 ya broiler. Sasa maswala ya faida yanahitaji muda mkuu!
 
Soko ni kubwa mno. Tatizo ni wachache mno kutokana na muda anaohitaji kufikia kuwa kitoweo. Bei yake ni zaidi ya mara 2-3 ya broiler, ila muda wa kumwaandaa awe kitoweo ni karibia mara 8 ya broiler. Sasa maswala ya faida yanahitaji muda mkuu!
Ni kweli, inabidi kuangalia kipengele kimoja baada ya kingine.

Je, walaji wanasemaje?

Nilikwenda Sinza fast food nikaona kuku wa kuokwa, nikasema kuku si ndio hawa (Tofauti na wale wa kuchemshwa kwenye mafuta) Hata hivyo sikuwapenda maana ni laini utadhani kinda la njiwa. Sikuona tofauti na wale wa kukaangwa kwenye mafuta.
 
Kuku hutoka kwenye kizazi kinachojulikana kitaalam kama gallus gallus, Ufugaji huu nitaoelezea ni wa kienyeji kabisa ila huu umeboreshwa kidogo ili kuleta faida zaidi, kwanza itabidi uwe na eneo lakutosha kama ekari mbili (70m *140m) banda la kuku liwe linalohamishika na liwe limejengwa juu juu, hii husaidia kupunguza maambukizi ya magonjwa kwa sababu kinyesi cha kuku kikilundikana huweza kubeba vimelea vya magonjwa

BANDA BORA LINALOHAMISHIKA

Banda liwekewe viota vya kutagia na unaweza kuwafundisha kuku kuvitumia mapema kabla ya kuanza kutaga kwa kuchelewa kuwafungulia asubuhi. Kwa kawaida kuku hupenda kulala bandani wakiwa juu juu kwa hiyo uweke baadhi ya fito au mbao nyembamba zikining'inia pia kuwe na vyombo vya chakula nje ya banda

Hakikisha banda halivuji na wanyama wakali hawaingii lakini liwe na hewa ya kutosha na lisiwe na joto wala baridi kali, ni vizuri ukiliweka chini ya miti

Ili kuboresha ufugaji huu inashauriwa kutumia majogoo ya kisasa ambayo yana patika kwa mazalishaji wa kuku kote nchini, pia unaweza kutumia majogoo ya kuku aina ya KUCHI wanaopatikana zaidi miko ya Singida na Shinyanga. Majogoo ya kisasa huweza kuhudumia wastani wa majike 20-25 na kuchi huweza kuhudumia majike 10 -15 kwa sababu ni wavivu kidogo.
MAJOGOO YA KISASA INA YA CORNISH


Andaa na banda la kukuziA watoto ambalo litawakinga na wanyama wakali na mwewe, banda linakuwa wazi juu hukulikizuiwa na waya kwa 75% na 25% iwe imezibwa kwa mbao ili kuwapatia kivuli wanapohitaji, banda hili lina hitaji kuhamishwa hamisha angalau mara 5 kwa siku kutika mahali pamoja hadi pengine, hakikisha banda la watoto lina maji na chakula muda wote, pia kumbuka kuwawekea mabaki ya mboga za majani kama mchicha, kunde, kisamvu n.k


FAIDA

(A)
Mfumo hauhitaji chakula maalum kama kuku wa ndani
(B) Wadudu kama utitiri na virobot hushambulia kuku mara chache
(C) Kuku hupata muda wa mazoezi kwa kutembea tembea
(D) Gharama za uendeshaji ni kidogo
(E) Hautumii muda mwingi
(F) Kiasi cha uchafu ni kidogo

HASARA
(A)
Vifaranga huweza kuliwa na mwewe au wanyama
(B) Mayai huweza kupotea yakitagwa nje ya banda
(C)Kuku huweza kula mbegu zilizopandwa mashambani
(D)Vifo vya kuku ni vingi

CHANJO
Kuku wapewe chanjo ya kideri/mdondo kila baada ya miezi mitatu chanjo hii hupatikana nchini kote ukifika dukani ulizia chanjo ya newcastle, utapata maelekezo ya jinsi ya kuwawekea kuku kwenye maji ya kunywa, chanjo hii wapewe kuku wazima tu na wagonjwa watengwe mbali

MINYOO
Kuku hunyweshwa dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu, kuna dawa kama piperazine na nyinginezo ambazo huwekwa kwenye maji

CHAWA NA UTITIRI
Unaweza kutumia dawa za kuogeshea mifugo kama ecotix au dawa ya unga unga ya kunyunyuzia kama akheri powder, dawa ya akheri unaweza kuimwaga bandani na kisha kumnyunyuzia kuku mwilini ukiwa umemning'iniza kichwa chini miguu juu ili mayoya yaacha nafasi ya dawa kuingia

MAGONJWA YA MAPAFU
Kuna magonjwa mengi yanayoshambulia mfumo wa hewa, dawa ya tylosin inauwezo mkubwa wa kupambana na magonjwa karibu yote, wape dawa hii mara tu unapoanza kuona dalili za mafua

Source: Mitiki.blogspot.com
 
LazyDogy,

Hii nondo ya Mama Joe ndo niliyokuwa naitafuta sana, mkuu umeshaanza hii ufugaji? mimi nimekuwa nikifuga kama hobby not for business...at a time nakuwa nao kama 50 hivi.....! Now nataka ni commercialize kama project ya waifu.....! Nitawapa feedback project inavyoendelea!
 
banda hili lina hitaji kuhamishwa hamisha angalau mara 5 kwa siku kutika mahali pamoja hadi pengine,
Ningependa kufahamu kwanini banda la vifaranga lihamishwe mara 5 kwa siku. Hii inasaidia nini?

Pia imeelezwa kwamba moja ya hasara ni kuwa "Vifo vya kuku ni vingi". Ufafanuzi unahitajika hapa.
Katika kuku 50, wangapi wanaweza kufa? Au hapa inazungumziwa uwezekano wa kuku wote kufa kwa mkupuo kutokana na magonjwa ya mlipuko?
 
LazyDogy,

Hii nondo ya Mama Joe ndo niliyokuwa naitafuta sana, mkuu umeshaanza hii ufugaji? mimi nimekuwa nikifuga kama hobby not for business...at a time nakuwa nao kama 50 hivi.....! Now nataka ni commercialize kama project ya waifu.....! Nitawapa feedback project inavyoendelea!
Hapana, sijawahi kufuga. Ila uzoefu umenionyesha kwamba kina mama wengi wanaweza sana shughuli hii kuliko wanaume, na hii imetokana na kwamba they have more passion kwa miradi ya namna hii. (Mwanaume atataka akaburuzane na ng'ombe dume).

Tatizo hawapati ushirikiano kutoka kwa waume, watoto au kaka. My mother was so enthusiastic kwenye ufugaji wa kuku na nilikuwa nikishindwa kuelewa vizuri. Siku moja mzee akamletea mbao za kujenga banda. Kuku waliotoka hapo sikutarajia. We need to add value to our mothers and sisters' projects.
 
Hapana, sijawahi kufuga. Ila uzoefu umenionyesha kwamba kina mama wengi wanaweza sana shughuli hii kuliko wanaume, na hii imetokana na kwamba they have more passion kwa miradi ya namna hii. (Mwanaume atataka akaburuzane na ng'ombe dume).

Tatizo hawapati ushirikiano kutoka kwa waume, watoto au kaka. My mother was so enthusiastic kwenye ufugaji wa kuku na nilikuwa nikishindwa kuelewa vizuri. Siku moja mzee akamletea mbao za kujenga banda. Kuku waliotoka hapo sikutarajia. We need to add value to our mothers and sisters' projects.

LD, hii project ni nzuri coz kwanza haihitaji gharama kubwa ukishakuwa na eneo la kutosha....pili, ni nzuri kwa diet mazee.....!

Off topic: Shapu naona unachungulia chungulia hapa......nenda class...utaliwa kichwa.......! tuachie ss na miradi yetu ya miti, kuku.....! ukipitia pale home kijana naweza pata mmoja kitoweo na my wf wako....! anyway how is it going there?
 
Nimetembelea blog ya Mitiki.blogspot.com
Kadiri muda unavyokwenda ndivyo itakavyokuwa rahisi zaidi ku-share information kwenye Internet kuliko ilivyo leo.

Itategemea speed ya mtu kujisomea - kuna watu watakuwa masikini kwa kasi kubwa, na wengine watatajirika kwa kasi ya ajabu! Miaka hii ni ya tofauti kuliko uwezo wa binadamu kutambua hilo. Miaka mitano ikipita, ndipo unapogundua mambo ambayo kabla, hukuwahi kutabiri au kuyawaza.
 
Ningependa kufahamu kwanini banda la vifaranga lihamishwe mara 5 kwa siku. Hii inasaidia nini?

Pia imeelezwa kwamba moja ya hasara ni kuwa "Vifo vya kuku ni vingi". Ufafanuzi unahitajika hapa.
Katika kuku 50, wangapi wanaweza kufa? Au hapa inazungumziwa uwezekano wa kuku wote kufa kwa mkupuo kutokana na magonjwa ya mlipuko?
Kuhamisha banda kunasaidia vinyesi visifanye ubichi kwa kawaida kuku wale wa kisasa wanajengewa banda lenye nafasi ya kutosha na pia maranda(taka za mbao) zinafanya carpet hivyo kinyesi kinajichanganya hakuna ubichi, sasa hawa ni banda dogo, chini udongo hivyo inasaidia kuondoa unyevu (kuku hawatakiwi kuwa na ubichiubichi)
Pili sehemu ya chini kuwa wazi ni kuwasaidia kupata wadudu, minyoo ambayo ndio source of protein kwao, kwa wale wa kisasa wanaipata kwenye dagaa na damu ya ng'ombe, hivyo ni kama tu unavyowahamisha mbuzi au ng'ombe wakiisha kula baada ya muda unawahamishia sehemu nyingine, wakubwa wanaachwa kula nje isipokuwa wanarudi kulala kwenye hilo banda lao.
Pia hawa kuku huwa wanamwaga maji sasa kwenye wa kisasa utaondoa maranda yaliolowa ila kwa hawa unavuta tu hiyo banda lao, unaangalia mwenyewe sio lazima sana kama ni wachache na unawapa vyakula kiasi pia sio pabichi unaweza acha, pia angali kiasi cha joto kama ni jua ni kali sana ardhi pia inapata joto unawapeleka kwenye upande wenye vivuli na upepo. lakini hiii ni kwa vifaranga tu ambao wanagusana na udongo ila wale wakubwa nadhani ni baada ya kinyesi kuanza kurundikana chini ya banda kwani kina uwezo wa kubeba magonjwa
kama anavyosema Next level nami niliwafuga for home and recreation lakini walipofikia 20+ nikashindwa kuwadhibiti pia nikawa na commercial interest na kuhamia kwa broilers.
Vifo ni kama hujui magonjwa mfano sijui mdondo ndio nimejua kuwa ni Newcastle! hivyo fuata masharti kama ya wakisasa kila baada ya miezi 3, huu ugonjwa ndio unawaua sana
Pili wengi wanawafuga simple: banda linaruhusu vicheche, paka shume, mbwa, kunguru hivyo unakuta mama akiangua 12 watapona 8 - 6 kama sio careful sasa hii ni wastani wa 50% cf wale wa kisasa kwa banda la 200 sana wanaweza kufa 4-6.
Na kwa vile mabanda haya hayana security sana wezi pia wanaweza kukuharibia kwa kuku wakubwa.
Vifo kwa kweli kama unawapa chanjo ya Newcastle kwa wakati au ni mzoefu na uko nao muda wote uweze kung'amua magonjwa hasa mafua na kuwatibu haraka sio vingi sana hadi kuleta hasara.
Ni wazuri sana nami ninataka kuwarudia tena ila mahali kwenye nafasi.
 
Nimetembelea blog ya Mitiki.blogspot.com
Kadiri muda unavyokwenda ndivyo itakavyokuwa rahisi zaidi ku-share information kwenye Internet kuliko ilivyo leo.

Itategemea speed ya mtu kujisomea - kuna watu watakuwa masikini kwa kasi kubwa, na wengine watatajirika kwa kasi ya ajabu! Miaka hii ni ya tofauti kuliko uwezo wa binadamu kutambua hilo. Miaka mitano ikipita, ndipo unapogundua mambo ambayo kabla, hukuwahi kutabiri au kuyawaza.

Ni kweli LD Kujisomea na kukubali kubadilika, pia kuhusu vifo vingi kuna hii survey ya Msami hapa chini inaelezea:

STUDIES ON THE STRUCTURE AND PROBLEMS OF FAMILY POULTRY PRODUCTION IN
TANZANIA.
In order to identify the major disease conditions and factors limiting family chicken production in Coast
and Dar-es-Salaam regions of Tanzania a survey was undertaken in six villages in two zones involving a total of
43 households. Field data were collected through identified farmer interviews in the wet and dry seasons of
1999/2000. During farm visits, the birds were clinically examined, sick and dead ones autopsied. Blood smears,
serum and faecal samples were collected for laboratory examination. There was significant variation in the flock
size and structure in the interviewed households. The 43 households kept 1099 chickens with an average of 25.5
per household in the wet season while in the dry season the numbers were 1352 and an average of 31.4. The ratio
of chicks:growers:adults was 10:10:14 in the wet season and 11:10:10 in the dry season. The cock:hen ratio was
1:3.5. Average numbers of clutches per year ranged from 2.80–3.02 (average 2-94). The average number of eggs
per clutch was 12 and consequently the number of eggs was 36 per hen/year. Hatchability was recorded to be
84.5. Chick mortality was found to be 30% and resulted mainly from diseases and predation. Out of 43
households interviewed, 23 kept their chickens in the chicken house, 12 within the family house, four in the
kitchen/store, three kept their birds perched in trees and one used a woven basket. In all the households,
scavenging was the system of feeding and sometimes supplemented by household scraps and other feeds. Poultry
movement into the household’s flocks resulting in mixing of birds from different flocks was rampant. Several
diseases and in particular Newcastle disease were mentioned by farmers in both zones as the major constraints
restricting rural chicken development. Other diseases included coughing/sneezing, fowl pox and parasitic
diseases (helminths, external parasites, protozoa).
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom