UEFA EURO 2024: Special Thread.

Dr Restart

JF-Expert Member
Jul 15, 2021
3,434
17,894
Naam, ni Hakika!
images.jpeg


Wakati ligi mbalimbali duniani zikielekea ukingoni, mashabiki kote duniani wanatarajia kwa hamu kuanza kwa tukio kubwa zaidi la soka barani Ulaya, UEFA EURO 2024.

Mashindano haya ya kusisimua, yanayofanyika mara moja kila baada ya miaka minne, yataanza kutimua vumbi Ijumaa, tarehe 14 Juni, na kumalizika Jumapili, tarehe 14 Julai.

Mwaka huu ni marudio ya 17 ya mashindano haya tangu kuanzishwa kwake mwaka 1960, na ni tukio la kihistoria kwani Ujerumani inaandaa kwa mara ya kwanza tangu kuungana tena. Hata hivyo, mashindano haya yaliwahi kuandaliwa na Ujerumani Magharibi mwaka 1988.

Mashindano ya EURO 2024 yanatarajiwa kuwa ya kipekee, yakifanyika katika miji kumi tofauti na kwenye viwanja kumi tofauti. Miji ikiwemo Berlin, Cologne, Frankfurt, Dortmund, Dusseldorf, Hamburg, Leipzig, Munich, na Stuttgart.


Jumla ya timu 24 zitashindana katika makundi sita, kila kundi likiwa na timu nne. Timu mbili za juu katika kila kundi huelekea hatua za mtoano. Huku best loosers wanne nao hupita katika hatua inayofuata.
20240415_234809.jpg


Kwa mara ya kwanza, timu ya taifa ya Georgia itashiriki katika mashindano haya, jambo linaloongeza msisimko zaidi.

Kwa taarifa kamili na maelezo zaidi kuhusu UEFA EURO 2024, jiunge nasi kutoka mwanzo hadi mwisho tunapokuletea matukio yote ya kusisimua ya mashindano haya ya kipekee.
 

FUSSBALLLIEBE​

Hili ni jina la mpira maalum utakaotumika katika mashindano ya UEFA EURO 2024.
F9969_00-ecommerce.jpeg


Jina hili linatoka katika lugha ya Kijerumani, ikimaanisha Mapenzi ya Mpira.

Mpira huu umebuniwa na kampuni ya Utengenezaji wa vifaa vya michezo, Adidas. Mpira huo ulizinduliwa mnamo November 15, 2023.

Mpira huu maalum umenakishiwa kwa rangi nne katika umbo la pembetatu. Rangi hizo ni nyeusi, kijani, nyekundu na njano. Pamoja na maana nyingine, rangi hizo zipo katika bendera ya taifa la Ujerumani, ambapo michuano hiyo inafanyika.

Mpira huo pia umeundwa kwa teknolojia ya hali ya juu (Connected Ball Technology). Teknolojia hii hufuatilia mwenendo wa mpira na vipengele vingine vingi na hivyo husaidia katika maamuzi ya VAR. Hii huongeza usahihi pamoja na ufanisi.
 
Albärt
Hili ni jina maalum la UEFA EURO 2024 mascot.
images (1).jpeg


Katika michuano mingi, kumekuwa na ushereheshaji wa aina yake na pia kutangaza michuano au matukio husika na kuifanya kuwa maarufu baina ya makundi mbalimbali.

Ili kuvutia zaidi watoto kupenda soka, Mascot Albart amechaguliwa kuwa mascot maalum wa michuano hii.

Huyu ni katuni mwenye muonekano wa Dubu. Katuni hii huwavutia sana watoto na kuwahimiza kupenda michezo. Katuni hii nchini Ujerumani ilitengenezwa na Richard Steiff, miaka ya mwanzo katika karne ya 20.
 
Tayari baadhi ya timu zimeshaanza kutaja vikosi vyao vya awali kuelekea fainali za EURO 2024.

Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps ameshatoa orodha ya awali ya Wachezaji 25 watakaoiwakilisha Ufaransa katika Michuano hiyo.

Katika kikosi hicho wachezaji hodari Christopher Nkuku pamoja na winga hatari Michael Olise wameachwa.

Katika hali ya kushangaza, Ng'olo Kanté amejumuishwa katika kikosi hicho. Ufaransa ambayo ipo katika kundi D pamoja na Austria, Uholanzi na Poland inategemea kutupa karata yake ya kwanza tar June 17, dhidi ya Austria.

Kikosi hicho ni kama ifuatavyo;
MAGOLIKIPA
1
. Brice Samba (Lens)
2. Mike Maignan (AC Milan)
3.
Alphonse Areola (West Ham)

WALINZI
4
. Ibrahima Konate (Liverpool)
5. William Saliba (Arsenal)
6. Jules Kounde (Barcelona)
7. Dayot Upamecano (Bayern Munich)
8. Jonathan Clauss (Marseille)
9. Benjamin Pavard (Inter Milan)
10. Theo Hernandez (AC Milan)
11. Ferland Mendy (Real Madrid)
VIUNGO
12.
N'Golo Kante (Al-Ittihad)
13. Eduardo Camavinga (Real Madrid
13. Adrien Rabiot (Juventus)
15. Warren Zaire-Emery (PSG)
16. Youssouf Fofana (Monaco)
17. Aurelien Tchouameni (Real Madrid)

WASHAMBULIAJI
18.
Olivier Giroud (AC Milan)
19. Kylian Mbappe (PSG)
20. Antoine Griezmann (Atletico Madrid)
21. Randal Kolo Muani (PSG)
22.Ousmane Dembele (PSG)
23.
Marcus Thuram (Inter Milan)
24. Bradley Barcola (PSG)
25. Kingsley Coman (Bayern Munich)

Hicho ni kikosi cha awali. Kinaweza kuongezeka hadi kufikia wachezaji 26, idadi inayoruhusiwa. Pia kocha anaweza kukibadilisha kwa kadri ya itakavyompendeza kabla ya June 7.

Ufaransa kwa jina la utani Le Bleus, inatazamiwa kuleta upinzani mkubwa na pengine kuwa mabingwa. Kikosi hicho almanusura ishinde Kombe la dunia 2022 nchini Qatar, kabla ya kuchabangwa na Argentina katika mikwaju ya penalty.
 
Viwanja vitakavyotumika katika Michuano hii ya Euro 2024 ni Viwanja 10, katika miji kumi tofauti.

Hapa chini nitaelezea uwanja mmoja baada ya mwingine.

Olympiastadion Berlin

Huu ndiyo uwanja mkubwa zaidi katika michuano hii. Uwanja huu una uwezo wa kubeba watazamaji sabini na moja elfu (71,000).


Olympiastadion_Berlin_Sep-2015.jpg

Uwanja huu hutumika na timu ya Hertha Berlin katika mechi za nyumbani ligi kuu ya Ujerumani, Bundesliga.

Uwanja huu ulishachezewa fainali mbili kubwa. Moja ni fainali ya ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA CL) kati ya Barcelona na Juventus, huku Barca ikitawazwa mabingwa mwaka 2015.

Lakini pia, ulichezewa fainali ya kombe la dunia 2006 kati ya Italia na Ufaransa. Hapa ndipo mtukutu Zinedine Zidane alimparamiza kichwa cha haja Materazzi na kulimwa kadi nyekundu.

Mtanange ulitamatika kwa sare ya mabao 1-1, Italia ikishinda kwa mikwaju ya penalty 5-3 na kutawazwa mabingwa. Hata hivyo Zidane alikuwa mchezaji bora wa michuano hiyo.

Katika fainali za Euro 2024, uwanja huu utatumika kwa michezo mitatu ya hatua za makundi, mchezo mmoja wa hatua ya 16, robo fainali moja huku ukitumikaa katika mchezo wa fainali tar 14-07-2024.
Olympiastadion_Berlin-Marathontor-msu-2020-3139.jpg

Uwanja huu upo katika mjini Mkuu Berlin ukimilikiwa na Serikali ya Ujerumani. Ulianza kujengwa tangu 1934 na kufunguliwa 1936. Umekuwa ukifanyiwa ukarabati mara kadhaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom