Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,675
- 698,690
Kuna kundi katika jamii wanaopinga uwepo wa uchawi na ushirikina hii si dhambi wala si kosa ni haki yao kutokana na makuzi uelewa imani na mazingira yao.
Lakini hili jambo lipo Sana kwenye kila nyanja ya maisha yetu, kwenye dini zetu biashara zetu,maisha yetu mitaani nk
Sehemu ambako uchawi na ushirikina vimetamalaki hasa ni sehemu zetu za kazi na bajeti kubwa huenda kwa waganga wa kienyeji ili tu;
-Kumuondoa fulani kwenye nafasi aliyonayo
-Apate cheo fulani
-Apate upendeleo fulani kazini
-Apate ajira
-Alinde ajira aliyo nayo
-Apate mamlaka na nguvu fulani za kiutawala na mamlaka
Ni katika michakato ya namna hii waganga hudanganya kuwa anayezuia hili au lile ni mfanyakazi Fulani au fulani ndio kaziba nyota yako.... mambo mengi ya jinsi hiyo...!!! Nafasi zenye hayo mambo sana ni ukurugenzi, secretary, transport officer, procurement public relations nk nk.
Ni wachache sana katika hao ambao mikono yao ni misafi na hawajawahi kushiriki hizi mambo. Vifo vingi vinavyotokea makazini sio kwa Mapenzi yao Mungu bali ni kurogana na kufanyiana, ushirikina, naamini kabisa wengi wetu hapa jamvini wana habari ya kusimulia kuwahusu haya vyovyote viwavyo.
Mungu ndie anayegawa riziki, na kila mtu ana kipimo chake, kufanya ushirikina na uchawi kwa ajili ya maslahi ya kazi ni kujitafutia laana isiyofutika.