Uchaguzi wa 2020 Hayati Magufuli alisema utakuwa huru na haki, yaliyotokea baadae sote tunayajua

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,457
2,281
Hili Neno la kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki linanikumbusha wakati wa uchaguzi wa 2020 Rais Magufuli aliwatangazia Watanzania kuwa Uchaguzi wa 2020 utakuwa huru na haki.

Yaliyojitokeza katika uchaguzi ule Watanzania wote tunayajua na Dunia nzima iliyajua.Wapinzani walikamatwa wakajazwa Magerezani Wabunge wa CCM wakapita bila kupingwa.

Magufuli akapita kwa Asilimia zaidi ya 85. Bunge likajaa kijani mpaka CCM ikajisahau kuwa Wafadhili watasitisha Misaada kwa kutokuwa na Kambi ya Upinzani Bungeni ndipo kina Halima Mdee na Wenzake Wakapewa Ubunge fake wa viti maalumu tukio ambalo lilipelekea Chama chao CHADEMA kuwafukuza uanachama na kuweka historia ya Bunge lenye Wabunge wasio na Chama kinyume na KATIBA.

Kutokana na utawala uliopo kushindwa kuwapatia Wananchi KATIBA waitakayo kwa wakati na kuishia Kubadili Jina la tume ya uchaguzi na kuiita Eti tume huru ya uchaguzi bila kubadili upatikanaji wa Viongozi wake na kubaki na utaratibu ule ule wa mgombea Urais kuteua Viongozi wa tume ni wazi uchaguzi wa 2025 hautakuwa huru wala wa haki.
 
Back
Top Bottom