Ubaya wa Kujifanya Mume Mwema

AljuniorTz

JF-Expert Member
Jan 6, 2009
544
17
Mke wa Kelvin anajivunia mume mtulivu, hashindi baa na hatongozi mademu. Akitoka kazini huenda kucheza basketball na kurudi nyakati za dinner. Siku moja mkewe akamhurumia kwa kuwa anachoka na kazi, je ni mtu gani asiyependa starehe japo kidogo?
Mke akamlazimisha mtoko (outing), Kelvin akabisha lakini kabla hajajenga vizuri hoja yake akashtukia taxi imefika na wakaelekea Gonga Club & Lodge.

Walipofika mlangoni tu, mlinzi akaita..., “Mambo Kelvin”! Akajibu; “Powa tu…”

“Nilidhani huwa huji club, inakuwaje mlinzi anakufahamu”? mke akauliza
Kelvin akajibu “yule mgambo mchana analinda ofisini kwetu, usiku anapiga part time hapa club...”

Wakachagua meza ya kukaa…, mara tu tayari mhudumu ameshaleta Castle lager.
Mhudumu akamuuliza… “mama anakunywa nini...”
Mhudumu baada ya kujibiwa akandoka na mke akamuuliza mume, “amejuaje unakunywa castle kama hakufahamu?”

Wakati Kelvin anajikanyaga aanze vipi kujitetea kwa soo lile.., mhudumu wa vyumba akawa amefika na kuuliza “mkuu kama kawaida nimekuandalia namba tano, nendeni tu vinywaji nitawaletea huko huko”

Kufikia hapo mke akawa hana simile tena, akanyanyuka akitukana kama chizi, akatoka nje mbio na kuingia katika taxi iliyokuwepo pale.

Wakati anapatana bei na dereva, Kelvin naye akaingia. Mke yakamporomoka matusi kibao na kilio juu. Alipovuta kamasi na kupiga kwikwi akamsikia dereve anasema. “Duh, eee bwana eeeehh!!! Kelvin huyu malaya uliyeokota leo balaaaaaaaaaaaaaaa!”

Mke akazimika….zzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii


 
Tusifiche tabia zetu kwa matarajio ya kulinda ndoa, uhalisia wa tabia ndio hulinda ndoa maana partner atakuwa anakujua nje ndani. Atachagua kusuka ama kunyoa....
 
Enuff already!Kama ni mgeni embu jaribu kuangalia angalia yaliyopita kidogo maana hii ilishabandikwa zaidi ya mara tano!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Back
Top Bottom